Aina za watu katika mafanikio

zelski

Member
Feb 20, 2024
13
12
Katika kuyatafta mafanikio na kufikia ndoto , kuna vitu vingi unaweza kujifunza .Ningependa ujue aina ya watu na jinsi watu hufanikiwa hii itakupa moyo, ujasiri na nguvu ya kuendelea kupambania ndoto na hatua ya mafanikio unayoyahitaji kabla hujaondoka duniani.

Kuna aina tatu za watu na jinsi watu hawa hufanikiwa;

I. Rules creator (Genius)
Hawa ni watu ambao hugundua mifumo na kanuni flani ambazo hua kama pattern ya kufanya mambo na wakafanikiwa au kufikia ndoto katika maisha, ni watu wenye vipaji vya kipekee ambavyo si kila mtu anavyo .Hawa ndio huseti kanuni bila kujijua ni wenye natural ability.
Uwezo wa kufikiri na kupima mambo kwa maono na kufanya maamuzi sahihi ni sehemu ya maisha yao.

II. Rules follower
Hawa ni watu ambao wanahitaji kujifunza mara kwa mara na kwa kila hatua wanayoipiga ni watu ambao hufuata kanuni na mifumo ya kufanikiwa wakiwa wanajua .
Ni kwa kufuata hii mifumo tu ndio hufanikiwa mfano kanuni kama kufanya kazi kwa bidii , nidhamu katika kazi na matumizi mazuri ya Pesa.

III. Rules Breaker
Hawa watu ni ambao kanuni au mifumo ya kufanikiwa hai define namna ambavyo watafanikiwa au wamefanikiwa, ni wenye bahati. Watu hawa hawahangaiki sana wala kujitesa sana lakini hufikia malengo na ndoto zao.

Si rahisi kujua uko wapi kati ya aina hizi za watu. Amini kilicho ndani yako (intuition) kitakuongoza mahari sahihi ya wewe kufanikiwa.

Kila mtu huwa na kipindi flani chenye nafasi ya yeye kufanikiwa katika maisha kutoka kuzaliwa adi kufa, issue ni kuwa si rahisi kujua kuwa nafasi ipi au wakati upi ni ya/wa kufanikiwa. Unachotakiwa ni kufanya kilicho sahihi muda wote, usipoteze muda kwa kusubiri vitu vitokee , fanya juhudi, pambania ndoto yako muda wote, fanya kilicho sahihi wakati wote, don’t waste a chance, jua unachokitaka pambana siku zote kukipata.
 
Back
Top Bottom