Abuse..( Dhuluma)

Hii topic ina mambo mengi sana my dia
Yaani ni kama umekusanya mafaili ya ofisi tatu za Mamlaka za Kodi nchi za USA, China na Brazil halafu umeweka ktk kajidude kamoja kadogo (flash)

Kwanza naomba nikurekebishe kwamba Sexual Abuse tunatafsiri kwa kiswahili kama Unyanyasaji wa Kijinsia

hatari.jpg

Naomba sasa nielezee kisa kimoja cha Unyanyasaji wa Kijinsia.

Kuna mdada ana mtoto mmja ameolewa, ana miaka minne katika ndoa yake, alizaliwa miaka 24 iliyopita.
Yeye na mume wake walikua wana pendana sana na mpaka sasa mdada anasema bado anampenda tena sana mume wake.

Ananiambia, " Yaani CPU, siku hizi mume wangu kabadilika sana kiasi najuta hata kuolewa yaani kidogo kanitukana mara mshenzi mara mjinga mara ananitisha kunipiga kwa kusema mimi simjui vizuri ndio maana nashindwa kufanya atakavyo.

Ukweli ninachanganyikiwa mume wangu anakuwa kigeugeu anaweza akakwambia "mimi sipendi uvae nguo ndefu", ukivaa fupi kwa muda huo aliosema anafurahi sasa itokee siku nyingine akuambie tutoke ukivaa hiyo nguo fupi anaanza
" . . . . unaenda kumuonyesha nani? Unatakautongozwe kwani mimi sikutoshi? "
Ukivaa ndefu au suruali ananyamaza.

Juzi simu yangu ilijizima nikiwa salon iliyo nje ya uzio wa nyumba tunayo ishi. Akampigia rafiki yake akaja mpaka saloon nikaongea naye kupitia simu ya rafiki yake. Jamani hakutaka kukata simu mpaka muda wa kazi uishe, karudi home hakuna salam ananiambia "utanieleza uliko kuwa" huku anatafuta mkanda aanze shunghuli. Mimi nikamwambia mimi sijatoka hata gengeni sikwenda.

Siku hiyo ndipo alipo mwita mtoto wake mwenye miaka minne nilimkuta naye akamuuliza, ndipo mtoto akamwambia "mama leo hajaenda mahali zaidi ya saloon anako sema" mume wangu akaona aibu akaondoka.

CPU, hata sasa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananiambia nisimkumbushe anakasirika mpaka nashindwa hata kuendelea kumuuliza. Ni mengi lakini naomba unisaidie "
Mkuu CPU mlikuwa mnahadithiana haya wapi? tehetehetehetehe ila nimeona tu kwa kusoma huyo mume ana wivu sana hadi inapelekea kutokujiamini kabisa,inaonekana huyo bibie ni mrembo wa haja. Mke anatakiwa amwelewe huyo mumewe vizuri ili kuepusha mambo kma hayo, akitoka mwenyewe avae nguo ndefu akiwa nae avae hizo fupi. Mh ndoa hizi zina vijimambo haswa
 
  • Verbal abuse (matusi),
  • Physical abuse (kimwili),
  • Sexual abuse(unyanyasaji wa ki jinsia,)
  • (Neglect)kutelekezwa)
  • Hate (chuki)
Ni vitu ambavyo viko sana kwenye jamii yetu
ni vitu ambavyo vinatokea kila saa, tonaona jinsi watoto wetu
wanavyo danganywa na wazee wazima, tunaona jinsi mama zetu
wanavyopigwa na kutukanwa, tunaona jinsi watu wanavyotengwa na jamii
sababu ya vitu wanavyofanya au jinsi walivyo na ambayo ipo kila sekunde
ni sisi kwa sisi kuchukiana .

wandugu ningeomba sana leo tuongelee hizi Dhuluma..
Nini kinampeleka mtu kufanya haya mambo??

Je kila afanyaye haya mambo ni mtu mmbaya??

na ni vipi tunaweza kuwasaidia waliokuwa kwenye hizi
situation
.... You are more than welcome to share anything....

(samahani wakuu ningeomba sana tutumie lugha ya kiswahili na English kidogo)
(ili kila mtu aelewe )
AD

...Naaamini asilimia kubwa wanao abuse wenzao nao ni waathirika (victims) wa aina moja au nyingineo ya abuse.
mfano;
  • alinajisiwa(bakwa) iwe ni mtoto wa kike/kiume
  • alilawitiwa au,
  • alipitia msukosuko (psychological torture) ambayo imemuachia kovu kwenye akili yake.
...kwa kiwango kikubwa, utapomshawishi mhusika kuwa muwazi kuelezea yaliyomsibu,
yanayomsibu na anayohisi yatamsibu ndio njia pekee inayoweza kumsaidia
kutuliza 'maruhani' wake.

Tahadhari; Trust ndio kitu pekee kitachomshawishi mtu huyu kuwa muwazi.
Atapokuamini, nawe jiaminishe kutunza siri yake.

Mfano; Kwenye ndoa/mapenzi, Abusers hutumia mwanya wa 'kuwaumiza' victims wao kujaribu 'kufidia' pengo la machungu/aibu ya waliyopitia...

asilimia kubwa ya waliopitia misukosuko ya mapenzi wanakuwa na vijichembe vya 'abusing behaviour' - ndio maana hata kwenye JF, wengi wetu tunapojadili matatizo ya wenzetu hukimbilia judgments za haraka haraka bila kuangalia upande wa pili 'wa shilingi' na kuulinganisha na Ukweli.
 
mhh...uji wa ugali??
wa-respond vipi tena wakati mie ndio boss wao!

mmmhh
naona unaanza kuni twanga mdogo mdogo mmhh
na mimi ndo best employee wako sasa we lete za kuleta
mmmmhhh...hahahah lol
 
unaweza sema asilimia 75
ya ndoa zina unyanyasaji hasa kwa wanawake......
na athari zake ni mpaka kwa watoto.....
tanzania...

Nakubaliana nawe kabisa
nadhani kubwa zaidi ya unyanyasaji hapa
kwetu TZ ni utekelezwaji ( Neglecting) ..
hata ile ya baba kwenda bar naku furahia maisha
yake wakati mama na watoto wamebaki nyumbani
ugali na sukumawiki a nyama ya dagaa.. mimi naona ni
neglecting.. au we unasemaje??
 
AD,

Hii topic imenigusa sana. Labda kwa vile mimi ni victim kwa namna moja au nyingine wa domestic violence na pia kwa vile mimi nachukia haya mambo. Nadhani haya matatizo yanajitokeza sana kwenye familia zetu kwa sababu watu wanatanguliza ubinafsi zaidi. Iweje mtu amtendee mwenzie yale ambayo asingependa kutendewa?

Kuna jamaa yangu alikuwa mpenzi sana wa vibinti vidogo. Ila watoto wake (girls) walipofikia umri wa puberty alipiga marufuku vijana wa kiume hata ndugu zake wa karibu kuja kukaa kwake!!!

Nitarudi tena baadaye.

Mzee DC.

Mzee DC pole sana my dear
kwa aina moja au nyingine hii topic imewagusa wengi
na wengine wameni PM na kuniambia samahani hawataweza
kuchangia sababu is to personal na zinawakumbisha mbali
na mi nawashukuru wote na samahani sana kama nimewagusa
vidonda ambavyo vilikuwa vinakaribia kupona.. na Poleni sana..

Binafsi nimepitia mengi tu lakini mimi tiba yangu ni kuviongelea
na kupokea ushauri na kutoa ushauri ..

samahani Mzee DC
Hapo kwenye red kama mtu anajua kabisa
hiki ni kitu kibaya kumfanyia mtu na mimi sintopenda
mwanangu afanyiwe hivi Je ni kwa nini bado anafanya??
Nway nasubiri umalizie hiyo story asante sana Mzee DC.
God bless.
 
Upo sahihi ila yanasababishwa na ubinafsi,kukosa elimu,umasikini na magonjwa kama kichaa

kwingine nakubaliana nawe kwa kiasi fulani
hapo kwenye umasikini labda sio sana
hapo kwenye ubinafsi nakuunga mkono 100%
magonjwa ya ukicha pia ni ukweli lakini
wengi hutumia hilo kama kisingizio..
lakini hapo kwenye RED nakataa kabisa kabisa
maana watu wenye elemu na waliosoma ndo utashangaa
ndo number one ikija kwenye Domestic Violence...
siniulize kwa nini lakini ndivyo ilivyo ..
 
Baada ya kusoma comments nyingi hapa, najihisi na mimi nina abuse sehemu flani, ngoja nijitizame
 
Wamama wengi wanavumilia hii dhuluma sababu ya kipato, maisha magumu na mwanamme anachukua advantage hapohapo na kuanza kumnyanyasa, utakuta mwanamke hajajaliwa kupata watoto anaambiwa unajaza choo, unafikiri hii ni sababu ya nini? hii yote nayo ni dhuluma na unyanyasaji wa hali ya juu

Mtoto hana kosa maskini ni sababu tu mzazi wake mmoja alifariki akaanza kuishi na baba/mama wa kambo hapa wamama ndio mara nyingi wananyanyasa watoto hawa, nafikiri ni ile hali ya kuona kama vile huyu mtoto anashare nae mapenzi ya baba yake. anahisi kama hastahili tena kupata yale mapenzi sababu tu mzazi wake mmoja kafariki.

Ajabu ya yote hii dhuluma, unyanyasaji, unyanyapaaji wote tunafanya sisi sisi wanadamu tunaojiuliza ni kwa nini, sasa basi kwa vile tunafanya sisi ni rahisi kila mmoja wetu ajiangalie, na ajichunguze kama kwa namna moja au nyingine anamnyanyasa mke/mume/mtoto/ndugu yake? tukiweza kubadilika wenyewe na wengine pia wanaweza kubadilika wale wanaotuzunguka na sisi tukawaonyesha mfano bora watoto wetu wanaokua na wao wakiwa watu wazima watafata tuliyowafundisha tangu wadogo
 
Baada ya kusoma comments nyingi hapa, najihisi na mimi nina abuse sehemu flani, ngoja nijitizame
Badilika Elia hailipi hata kidogo, unajua tunapofanya haya mambo tujiulize kama sie au watoto wetu wakiishi na watu wengine wakafanyiwa hayo tutajisikiaje? tubadilike na wengine wataiga
 
Wamama wengi wanavumilia hii dhuluma sababu ya kipato, maisha magumu na mwanamme anachukua advantage hapohapo na kuanza kumnyanyasa, utakuta mwanamke hajajaliwa kupata watoto anaambiwa unajaza choo, unafikiri hii ni sababu ya nini? hii yote nayo ni dhuluma na unyanyasaji wa hali ya juu

Mtoto hana kosa maskini ni sababu tu mzazi wake mmoja alifariki akaanza kuishi na baba/mama wa kambo hapa wamama ndio mara nyingi wananyanyasa watoto hawa, nafikiri ni ile hali ya kuona kama vile huyu mtoto anashare nae mapenzi ya baba yake. anahisi kama hastahili tena kupata yale mapenzi sababu tu mzazi wake mmoja kafariki.

Ajabu ya yote hii dhuluma, unyanyasaji, unyanyapaaji wote tunafanya sisi sisi wanadamu tunaojiuliza ni kwa nini, sasa basi kwa vile tunafanya sisi ni rahisi kila mmoja wetu ajiangalie, na ajichunguze kama kwa namna moja au nyingine anamnyanyasa mke/mume/mtoto/ndugu yake? tukiweza kubadilika wenyewe na wengine pia wanaweza kubadilika wale wanaotuzunguka na sisi tukawaonyesha mfano bora watoto wetu wanaokua na wao wakiwa watu wazima watafata tuliyowafundisha tangu wadogo
Gaga umenena cha maana sana
Specially your conclusion..
Kwamba sisi tujichunguze na kujibadilisha..
Lakini kuna wale ambao tayari wako Sugu..
Unadhani hao watabadilika kirahisi hivyo???
 
Hoja yako ni ndefu sana na kwa mtazamo wangu haiwezi kujibiwa kwa upana wake. nadhani inabidi kuchagua eneo la kujibu kwa sababu hizo abuse ziko tofauti na inawezekana kabisa zinakasabishwa na vitu tofauti na hata namna ya kuzitatua ni tofauti from each other. kwa upande wangu ntachangia kuhusiana na phyisical abuse i.e. kupiga/kupigwa mwili.

ntaanza na mfano wa familia yangu. sie tuko wanane kwa baba na mama. 7 wanaume. tuna dada mmoja. katika maisha yetu, mimi ni wa 6, sijawahi kumwona baba akimpiga mama hata siku moja. mama mwenyewe hulikiri hili kila cku. hali kadhalika, hatujawahi kupigwa na baba hata cku moja. ni kaka yetu mmoja ambaye aliwahi kupigwa na bb na ni kwa vile alimpiga mama! nadhani kwa malezi hayo, hata nasi hatujawahi kuwapiga spouses na watoto wetu hata siku moja! hapa nilipo kuinua mkono wangu kumpiga mtu, hata kama ni mwanaume mwenzangu, ni ngumu sana. nasikia kabisa mkono ni mzito.

nadhani hali ingekuwa tofauti kama tungekua kwenye familia ambayo kupigwa/piga ni hali ya kawaida. so kwa ufupi malezi yanaweza kusababisha abuse, walau za aina hii (physical abuse). Nadhani mchango wangu unatosha kwa sasa
 
Gaga umenena cha maana sana
Specially your conclusion..
Kwamba sisi tujichunguze na kujibadilisha..
Lakini kuna wale ambao tayari wako Sugu..
Unadhani hao watabadilika kirahisi hivyo???
Wengi wetu tukibadilika watabakia wachache mwishowe wataona aibu, ila kwa kiukweli hili tatizo halitaweza potea kabisa ila tunaweza lipunguza kwa kiasi kikubwa sisi wenyewe
 
Hoja yako ni ndefu sana na kwa mtazamo wangu haiwezi kujibiwa kwa upana wake. nadhani inabidi kuchagua eneo la kujibu kwa sababu hizo abuse ziko tofauti na inawezekana kabisa zinakasabishwa na vitu tofauti na hata namna ya kuzitatua ni tofauti from each other. kwa upande wangu ntachangia kuhusiana na phyisical abuse i.e. kupiga/kupigwa mwili.

ntaanza na mfano wa familia yangu. sie tuko wanane kwa baba na mama. 7 wanaume. tuna dada mmoja. katika maisha yetu, mimi ni wa 6, sijawahi kumwona baba akimpiga mama hata siku moja. mama mwenyewe hulikiri hili kila cku. hali kadhalika, hatujawahi kupigwa na baba hata cku moja. ni kaka yetu mmoja ambaye aliwahi kupigwa na bb na ni kwa vile alimpiga mama! nadhani kwa malezi hayo, hata nasi hatujawahi kuwapiga spouses na watoto wetu hata siku moja! hapa nilipo kuinua mkono wangu kumpiga mtu, hata kama ni mwanaume mwenzangu, ni ngumu sana. nasikia kabisa mkono ni mzito.

nadhani hali ingekuwa tofauti kama tungekua kwenye familia ambayo kupigwa/piga ni hali ya kawaida. so kwa ufupi malezi yanaweza kusababisha abuse, walau za aina hii (physical abuse). Nadhani mchango wangu unatosha kwa sasa
Umeona eee Manumbu! ndio maana nikasema tunaweza anza generation yetu kulimaliza hili kwa kuwalea watotot wetu na ndugu zetu kwa upendo bila manyanyaso na ubaguzi na watoto wetu kuiga hili kama wewe
Manumbu unajua michembe?
 
Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom