Search results

  1. K

    Je, unafahamu dawa ya huu ugonjwa.

    Pamoja na salamu kwa wana JF wote ! Naomba kama kuna mtu anafahamu dawa ya kutibu au kutuliza "FLATULENCE". Kuna jamaa alinipa e-mail ya mtu mmoja ambae inasemekana anauza vitabu ambavyo vinaelekeza tiba ya hilo tatizo nimejaribu kuwasiliana nae haonyeshi kutoa ushirikiano ( hanijibu), e-mail...
  2. K

    Matokeo ya kidato cha pili

    Wana JF, Naomba mnisaidie kunijulisha jinsi gani nitapata matokeo ya kidato cha pili mwaka 2011, nasikia yametoka najitahidi kutafuta ili niangalie matokeo ya mtoto wangu bado sijafanikiwa. Kama kuna yeyote mwenye kujuwa yanapatikana kwenye web site ipi naomba anijulishe. Natanguliza shukurani.
  3. K

    Naomba ushauri

    Habari zenu wana JF, Hivi karibuni nilimshitaki mtu kwa kosa la kuiba mali niliyomkabidhi kuiuza dukani kwangu. Baada ya kesi kuisha mahakama / Hakimu alimuhukumu mtuhumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja nje ya gereza pamoja na kulipa pesa anazodaiwa kwa kulipia mahakamani kiasi...
  4. K

    Msaada tafadhali

    Habari zenu wana JF. Naomba mnisaidie. Mimi nina mdogo wangu wa kike ambae anasoma kidato cha tatu, ameyakimbilia maisha hivyo amepata ujauzito. Aliyempa ujauzito alipoona hali imekuwa ngumu kwake akamshawishi yule msichana wakaitoa ile mimba, kwa bahati mbaya zilijitokeza 'complications' ikiwa...
  5. K

    Nini maana ya utetezi kisheria .

    Habari zenu wana JF. Rafiki yangu anatuhumiwa katika kesi, jana baada ya kufika mahakamani na kusikilizwa kesi yake kwa mlalamikaji kuleta shahidi Hakimu wakati anaahirisha kesi alimwambia mtuhumiwa siku inayofuata atakapokwenda awakilishe UTETEZI WAKE, je ina maana gan ?.
  6. K

    Kubanwa na haja kubwa kila ninapokuwa katika chombo cha safari

    Naomba msaada, kila ninapopanda katika basi au kukaa pamoja na watu zaidi ya watatu nahisi kubanwa na haja kubwa(stool). Nikienda chooni kakitoki kitu na nikiwa katika usafiri baada ya kushuka hali hiyo huwa inapotea. Nimekwenda hospitali hali hii hawaifahamu wananipa dawa za kuharisha tu...
Back
Top Bottom