Kabla hatujazungumzia AMANI kwanza tuzungumzie HAKI. Penye HAKI, AMANI lazima itakuwepo, kwanini tunawasiwasi kuwa AMANI haitakuwepo kwenye na baada ya uchaguzi? Jibu ni rahisi, Kuna dalili za kutokuwepo kwa HAKI. Je kwanini kwanza tusiimbe wimbo wa HAKI? kwanini tusimuombe Mungu ili HAKI iwepo? kwasababu AMANI ni tunda la HAKI
Watawala na wagombea wanaonyesha dalili zote za kutokuwa na HAKI. Huku wakihubiri AMANI.
- Goli la mkono
- hatuko teyari kuwaachia wakinafulani nchi.
- Rais hawezi kutoka katika upande fulani wa nchi.
- Lazima tutashinda (pande zote mbili wanazungumza hili).
- Unaandaa kikosi kazi cha kuratibu mambo baada ya kuwa rais, je ikiwa tofauti?
- Unapowaambia wananchi wajiandae kushangilia ushindi, je matokeo yakiwa tofauti?
Je, sasa kuna AMANI? je kabla ya sasa kulikiwa na AMANI? Je AMANI ndio UTULIVU?
Katika etymology ya neno peace kwenye wikipedia kuna mstari huu (Peace including justice, good health, safety, well-being, prosperity, equity, security, good fortune, and friendliness). Je tumevifikia kwa kiwango gani hivi?