chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mbunge wa Ilala Azzan Zungu ameunga mkono kodi ya makato kwenye mihamala ya simu na kusema serikali inapoteza mapato makubwa sana, amedai makampuni yana lobby kuwa wananchi wataumia kumbe watakoumia ni wao, amewataka wananchi kuacha kulalamikia kodi kwani serikali inategemea kodi kufanya shughuli zake.
Pia amezungumzia fedha zinazopotea kwenye madini kwa makampuni ya madini kudanganya thamani ya mzigo, na wasimamimizi kukosa uelewa, amesema serikali imepoteza trilioni 18 kutoka 2002 mpaka 2011 kutokana na kudanganya bei na ameshauri hiki ni chanzo kingine kikubwa ambacho serikali inaweza ikatumia kama ikisimamiwa vizuri.
Namnukuu (kama alivyonukuliwa kwenye Hansard za Bunge):
======
UPDATE:
Zungu amerudia kauli hii 2021: Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania
Pia amezungumzia fedha zinazopotea kwenye madini kwa makampuni ya madini kudanganya thamani ya mzigo, na wasimamimizi kukosa uelewa, amesema serikali imepoteza trilioni 18 kutoka 2002 mpaka 2011 kutokana na kudanganya bei na ameshauri hiki ni chanzo kingine kikubwa ambacho serikali inaweza ikatumia kama ikisimamiwa vizuri.
Namnukuu (kama alivyonukuliwa kwenye Hansard za Bunge):
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali wai-revisit hii kodi mpya kwa kutazama namna gani ajira zitaathirika katika nchi yetu. Yako malalamiko wananchi wanasema sisi Wabunge tunasema kodi hii ya simu, mimi nasema ni sahihi iwepo na ndiyo njia peke yake ya Serikali ya kupata mapato ya ziada. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, transaction ya M-PESA nchini mwetu kwa mwaka ni trilioni 50, trilioni 50 transaction ya pesa zinazozunguka kwa mwananchi na mwananchi mwenzio ni fifty trilioni kwa mwaka. Makampuni haya yana-lobby kuona kuwa wanaoumia ni maskini, si kweli watakaoumia ni wao. Kwa hiyo, kodi hii naiunga mkono, Serikali iendelee na kodi zingine na kukamata mapato kwenye simu, we are losing a lot of revenue kwenye maeneo haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye simu kuna non voice revenue, haya ndiyo maeneo Serikali inatakiwa ikae iyatazame. Pesa nyingi sana zinapatika kwenye non voice revenue ambayo sheria zetu hai-capture, inafanya makampuni haya yanaondoka na hela nyingi. Mfano mdogo, Kenya walilalamikia wananchi, lakini Kenya they put their foot down kodi ile ye transfer imewekwa na leo M-PESA, Safari com peke yao wameongeza wateja 21 percent kama hii inaumiza wananchi Kenya wangesema.
Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wetu na sisi tubadilishe minding setting zetu, Waheshimiwa Wabunge tusiwe na tabia ya kizamani ya kuona tukilipa kodi watu wanaumia, bila kodi Serikali hii haichapishi note. Simu hizi unakaa Dar es Salaam unapeleka pesa Jimboni within second hivi kulipa hata shilingi 400, 500 kwa kila transaction tatizo liko wapi? Ukienda Ulaya Dollar to Pound shilingi ngapi tunakatwa, ukienda Ulaya Dollar to Euro shilingi ngapi tunakatwa, commission za bureau de change, kwa nini tunaogopa kulipa kodi za Serikali? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kenya, Safari com peke yake imepata faida ya six hundred billions kampuni moja, sisi Makampuni yetu miaka yote yanapata hasara. Kwa hiyo, Serikali put your foot down, kamata hizi kodi ili wananchi wapate huduma. Pia regulator TCRA lazima wajue teknolojia inavyobadilika business as usually imekwisha, wawe on their toes kuhakikisha makampuni haya yanalipa hizi kodi. (Makofi)
======
UPDATE:
Zungu amerudia kauli hii 2021: Azzan Zungu ataka uwepo wa kodi ya uzalendo itakayokatwa kwenye Mitandao ya simu kwa kila Mtanzania