Zuio la kutumika kwa uwanjawa bandari kwa mashindano ya Ndondo Cup 2017

abdulrahim

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
408
286
Habari wanajamii!

Binafsi sio shabiki wa mchezo wa miguu ila ni mdau mkubwaa wa maswala ya michezo kwakuwa mashindano ya michezo yanaleta burudani, Afya njema na kutoa ajira na kuinua vipaji kwa vijana wetu.

Nimesikitishwa saana na Barua ya M/Kiti wa mashindano ya Sports Extra Ndodo Cup ya trh 15.07.2017 ikiwajulisha wapenzi na mashabiki wa mashindano hayo kutofanyika kwenye viwanja vya Bandari Temeke.

Hili limeniuma saana, Limenikwaza saana na limenikereketa saana wallah!

Kwa kumbukumbu yangu Bw. Shafii Dauda wiki iliyopita alitoa taarifa kwamba mechi zote zitafanyika baina ya viwanja viwili kwa kuzingatia maeneo ambapo team zinatokea. Alibainisha ni kiwanja cha Kinesi( Kinondoni ) na Bandari (Temeke) ambacho ukarabati wake umekamilika na tayari kwa matumizi.

Ukaguzi wa uwanja ulikwishafanyika na walikubaliana mpaka kufikia hatua ya kujuzwa sisi wanajamii.

Taarifa ya leo imenitia mashaka saana na kunipa dhana hasi juu ya aina ya watu wanaosimama kwaajili ya wengi tulio chini.

Mimi ni mwanachama na mpenzi wa chama cha mapinduzi pia ni Mkereketwa mkuu na mpenzi we serikali ya awamu ya tano. Noamba yafuatayo yafanyike kwa haraka ili kunusuru hili;

1. Kufanyika mashindano ya Ndondo CUp uwanja wa bandari uliokarabatiwa na kuwa na hadhi yake kwasasa ni mwanga wa kuonyesha kwamba soka la mchangani limepanda thamani, hivyo wahusika wakuu wa michezo ngazi ya wilaya temeke mpaka Taifa wanahitajika kutupa majibu ya ni kwanini mashindano hayo hayatafanyika kwenye uwanja huo?

2. Binafsi zuilio hilo nalihusisha kwa karibu saana na upinzani/kupishana kwa waandaaji(Clouds media) na aliyesimamia na kutafuta wadhamini wa ukarabati wa uwanja huo ( Ndg. Paulo Makonda). Mamlaka za juu zinazosimamia michezo( Wizara ya Habari,Utamaduni na michezo) zitolee ufafanuzi zaidi juu ya hilo kwani kwenye hili kila mmoja amekamilisha wajibu wake..Mkuu wa mkoa kutafuta wadhamini wa kuukarabati uwanja ndio ni kazi yake alipaswa kulifanya hilo na waandaji pia wamefanya kwa eneo lao.

3. Kwa hali yeyote ile zuio hilo halina nia njema kwa ukuaji wa mchezo wa mpira nchini Tanzania bali ni kukwamisha na kurudisha nyuma jitihada za wanopenda kuona soka ya Bongo inanyanyuka. Hivyo Mamlaka husika zisisite kutuma wataalamu wake na kuruhusu haraka uwanja ule kutumika kwa mashindano haya pendwa mtaani.

4. Michezo ni kinga dhidi ya madawa ya kulevya. Eneo la TMK ni eneo moja wapo ndani ya mkoa wa Dar es salaam lilioathirika zaidi na madawa ya kulevya hivyo kuondoa burudani hii ni kuondoa fursa za vijana wengi kwenye eneo hilo kiasi kwamba muda ambao wangeutumia kupata burudani hiyo na wengine kuudha bidhaa zao halali wa watazamaji basi wengi watautumia kufanya yale yasiyofaha.

Mwisho Kabisa.. Serikali ni baba na Mwananchi ni mtoto, Baba hahitaji kusifiwa wakati analea mwanae ila baba husifiwa pale mwanaye anayemelea anapotoa matokeo chanya kwa jamii..

Wenu Mkereketwa!!
CEO ChailoCoffeeShop

CC; Anko @EdoKumwembe @ShafiiDauda mwakyembe
 
Halafu bado mtu anajiita mlokole tena ananena Kwa lugha kabisaaa....roho imejaa visasi...
 
Sasa ni zamu yao clouds kuungua kwa kidogo wakati wanafurahia watu wanachafuliwa waliona raha dunia bhana inazenguka usimtendee mtu ubaya kisa masilahi yako siku yakikufika nawe utajua maumivu yalivyo.ila nachoweza kusema mkulu kama anataka kuweka historia iliyo safi kwake na kizazi chake bas hana jinsi kumtupilia mbali Mbali Bashite asiangalie ni mishe ngapi alimpa na siri ngapi anazijua ukiamua kumchinja kuku usiwaze amekula chakula chake kiasi gani.

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna kiapo hapo ndani yake.
 
Ccm isipoondoka madarakani msitegemee lolote zuri katika soka

Ovaaaa

CCM haiusiki na swala hilo ndugu... Swala ni Je sisi binafsi tunatambuaje [HASHTAG]#MAPINDUZIYAKIFIKRA[/HASHTAG] Nafsi zetu zinapoamua kuchukua uongozi/utawala basi ziwe tayari kwa hali yeyote chini/juu lakini tutimize wajibu wetu..

Watanzania/Waafrica yatupasa tujifunze nafsi za kusimamia maslahi ya wengine na kwa ushuhuda wa ubinafsi wetu chunguza ni waafrica wangapi wamejitolea kwenda kujifunza kwa wenzetu (Volunteering). Hawa wazungu wanaokuja africa sio kwamba ni matajiri wengine wakikuhadithia wameipataje pesa mpaka kuja Africa wewe unayeshindia dagaa utajiona ni tajiri.. Ni ubinafsi ndio unaotusumbua.
 
Mambo ya kijinga hufanywa na mwenye akili za kijinga

Sent from my D6633 using JamiiForums mobile app
 
CCM haiusiki na swala hilo ndugu... Swala ni Je sisi binafsi tunatambuaje [HASHTAG]#MAPINDUZIYAKIFIKRA[/HASHTAG] Nafsi zetu zinapoamua kuchukua uongozi/utawala basi ziwe tayari kwa hali yeyote chini/juu lakini tutimize wajibu wetu..

Watanzania/Waafrica yatupasa tujifunze nafsi za kusimamia maslahi ya wengine na kwa ushuhuda wa ubinafsi wetu chunguza ni waafrica wangapi wamejitolea kwenda kujifunza kwa wenzetu (Volunteering). Hawa wazungu wanaokuja africa sio kwamba ni matajiri wengine wakikuhadithia wameipataje pesa mpaka kuja Africa wewe unayeshindia dagaa utajiona ni tajiri.. Ni ubinafsi ndio unaotusumbua.
Mleta mada nashukuru kwamba umeuona mchango wangu

Akili na nafsi yangu iko huru and the same applies to you.

Ukweli ni kwamba viwanja vyote nchini ni Mali ya chama ambapo chama ni serikali.

Simba na Yanga ni mali ya chama na chama ndo serikali.

Chama na serikali hawako tayari kuona simba na Yanga wanacheza nje ya viwanja vyao na nje ya scope yao kiutawala na kiuchumi.

Na hapo nimekupa observation ambayo ni underground, go deep for yourself.
 
Back
Top Bottom