Zuckerberg aelezea 'Mauaji ya mubashara kwenye Facebook'

abudist

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
850
781


Bosi wa Facebook ametoa rambirambi na masikitiko yake kuhusu mauaji ya Robert Godwin ambayo yaliwekwa kwenye mtandao wake. Na kwamba Facebook itaendelea kujitahidi kuzuia vitendo hivyo kwenye mtandao wake.

_95691923_3f4f115100000578-4416996-stevens_posted_a_photo_of_himself_and_joy_who_he_seems_to_partia-m-5_1492420715102.jpg

(Muuaji na rafiki yake wa kike ambaye alimpiga chini jamaa akapata wazimu wa kuua)

Kama mnakumbuka jana polisi walikuwa wanamtafuta jamaa mmoja Steve Stephens, 37 kwa mauaji ya risasi ya babu mmoja Robert Godwin, 74 Cleveland, Ohio. Alimuua wakati mzee huyo akitembea kuelekea nyumbani akitoka kwenye hafla ya Pasaka. Halafu jamaa akarekodi tukio hilo, na pia kuliweka tukio la mauaji mubashara kwenye Facebook. Hivyo watu wamekuwa wakiishutumu Facebook kwa kuchelewa kutoa video hizo kwenye mtandao wake. Sababu hii mara kadhaa sasa watu wanonyesha mauji mubashara kwenye mtandao wa Facebook. Ingawaje matokeo haya yanaripotiwa mapema kwa Facebook.

_95693709_capture.jpg

(Marehemu Robert Godwin na mtoto wake wa kike Debbie Godwin)

Hapa chini inaonyesha ni jinsi gani na muda gani tukio liliripotiwa:

11:09AM PDT (19:09 GMT) - video ya kwanza, yakuonyesha dhamira ya kuua, ilitumwa mtandaoni Facebook. Kwanza haikuripotiwa kwa Facebook.

11:11AM PDT - video ya pili, Ya kuua, ilitumwa mtandaoni Facebook

11:22AM PDT - Muuaji kakiri mubashara kwamba kaua , ilionekana mtandaoni Facebook kwa dakika 5

11:27AM PDT - Mubashara imekwisha kuonyweshwa, na video ya mubashara inaripotiwa kwa Facebook baada ya muda.

12:59PM PDT - video ya mauaji mwanzo ikaripotiwa.

1:22PM PDT - Facebook wakaizima akaunti ya mtuhumiwa; Video zote hazikuonekana tena kwa umma.

Hata hivyo muda mchache uliopita msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo umeishia ukingoni baada ya kumkuta bwana Steve Stephens akiwa kwenye gari yake kajiua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom