Zouzoua ang’ara tuzo ya mwezi Juni NBC premier league

Zouzoua ang’ara tuzo ya mwezi Juni NBC premier league

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Kiungo wa Young Africans, Peodoh Pacome Zouzoua, ametangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwezi Juni katika Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025. Zouzoua aliwashinda Clatous Chama wa Simba na Kibu Denis wa Yanga, baada ya kuisaidia Yanga kushinda mechi zote tatu alizocheza mwezi huo, akifunga mabao matatu na kuhusika kwa kiasi kikubwa katika dakika 242 alizotumika uwanjani.

Kwa upande wa Kocha Bora, Miloud Hamdi wa Yanga alinyakua tuzo hiyo baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo mitatu mfululizo dhidi ya Tanzania Prisons, Dodoma Jiji na Simba, na kufanikisha kutwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Aidha, Meneja wa Uwanja wa Tanzanite Kwarara, Jackson Mwendwa, alitangazwa kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Juni kwa usimamizi bora wa miundombinu na matukio ya michezo.
1752329643545.png
 
Back
Top Bottom