Zomea zomea, piga piga.......... Nini chanzo chake na nini kitafuata?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zomea zomea, piga piga.......... Nini chanzo chake na nini kitafuata??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sawabho, May 20, 2011.

 1. s

  sawabho JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Ni muda sasa kumekuwepo na hulka ya wanachi katika baadhi ya maeneo katika mikutano ya hadhara kuwazomea baadhi vingozi wa kisiasa au Watendaji pale ambapo hawaridhishwi na majibu au maelekezo yanayotolewa. [/FONT]

  [FONT=&quot]Nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini siku/mika ya hivi karibuni watu waanze kuwaazomea viongozi wao tofauti na miaka ya 80 au 90 nilipokuwa nikienda na Baba yangu kwenye mikutano ya namna hii, kiongozi akianza kuongea watu wote kimya. Akiongea jambo la maana utasikia makofi na vigele gele, [/FONT][FONT=&quot]kama[/FONT][FONT=&quot] hawajaridhishwa na jambo alilosema wanatulia tu. [/FONT]

  [FONT=&quot]Baada ya kutafakari na kuongea na baadhi ya wazee wa miaka hiyo, nikagundua kuwa viongozi wa siku hizi wanapuuzia matatizo ya wananchi, hawayashughulikii kwa wakati, na yakishughulikwa nguvu kubwa inatumika au baada ya kujitokeza tatizo kubwa lilisababishwa na hayo ambayo wamekuwa wakiyapuuzwa. [/FONT]

  [FONT=&quot]Nikitolea mfano wa mambo yanaendelea Tarime; mgogoro baina ya mgodi wa North Mara na wananchi walio karibu na mgodi huo ni wa siku nyingi. Kampuni ya Afrika Mashariki Gold Mine (AMGM) ilipoingia Nyamongo mwanzo mwa miaka ya 90 (1990s) iliwakuta wanavijiji vya Kewanja, Matongo, Kerende, Mrwambe, Nyabigena, Nyamwaga, Genkuru, Nyarero, Mrito, Nyakunguru wakitegemea dhahabu katika maeneo ya Nyabilama na Nyabigena katika kuendesha maisha na wengine wakiishi na kulima katika maeneo hayo, achilia mbali vijiji vingine ambavyo viko mbali. AMGM ikawalipa fidia lakini bila wananchi kuandaliwa kimawazo na maeneo ya kuhamia. (NITOE HONGERA KWA KAMATI YA KURATIBU MAAFA YA MABOMU - GONGO LA MBOTO KWA KUAMUA KUWAJENGEA WAATHIRIKA). [/FONT][FONT=&quot]Hilo[/FONT][FONT=&quot] ndilo lingefanyika Nyamongo. AMGM ikauza Mgodi kwa Barick Gold Mine North Mara, hawa nao wakakuta hali hiyo hiyo. [/FONT]

  [FONT=&quot]Wananchi wakalalamika kuwa fidia haikutosha, maji yenye mercury katika mto Tigete kubabua watu na kuua mifugo, baadhi ya wananchi wanaozunguka mgodi wakawa na tabia ya kwenda kwenye kifusi kinachomwagwa kuokota mawe ya dhahabu, baada ya wenzao kuona kwamba wanapata pesa idadi ikakongezeka na wakati mwingine badala ya kuokota kwenye kifusi kilichotupwa wanaingia usiku mgodini kuchimba. Kundi lilipokuwa kubwa wakajaribu kuvamia ili wachimbe mchana kweupe wakati mwingine wakifanikiwa, wakati mwingine Polisi wakiwadhibiti, kuua au kuumiza baadhi. [/FONT]

  [FONT=&quot]Wakati yote hayo yakitokea na kuendelea, hakuna jitihada za makusudi zilizofanyika kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa kudumu unapatikana. [/FONT]

  [FONT=&quot]Sasa idadi ya watu wanaotaka kuokota dhahabu kwenye kifusi imeongezeka na kufikia zaidi ya 800 na ndio hao waliopambana na askari wanaolinda mgodi, na badaye "kumrudi" Mwakilishi wao pale alipoenda kutafuta suluhu kwenye hadhira iliyogoma kuchukua na kuzika miili ya marehemu 5. [/FONT]

  [FONT=&quot]Sasa Wana JF, tafakari kosa ni la nani? Mimi naona ni viongozi husika kuchelewa kutatua matatizo ya wananchi. [/FONT][FONT=&quot]Na baada ya zomea zomea, imekuja piga piga, ni kitafuata................... [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Chanzo ni dhuluma na mpango mzima wa kujikomboa.
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Nawahimiza wananchi wa Nyamongo wakusanyike wawe kama elfu kumi wakavamie tena huo mgodi ili kudhibiti rasilimali zao. ABG ni wezi na wanalindwa na serikali ya ccm. Dawa ni kuwavamia tu hakuna namna nyingine ya kukomesha dhuluma. Kumbukeni haki haiombwi inatafutwa na kupiganiwa hadi ipatikane
   
 4. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hili neno la hekima sana, kwa kweli ningekuwa huko nyamongo, naamini sasa hivi stry ingekuwa nyingine
   
Loading...