Zombe ni zaidi ya muuwaji-CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zombe ni zaidi ya muuwaji-CHADEMA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BASIASI, Aug 14, 2011.

 1. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,116
  Likes Received: 351
  Trophy Points: 180
  [h=2]Chadema yang`ang`ania kumwanika Zombe katika mauaji[/h]


  Na Thobias Mwanakatwe  14th August 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni
  [​IMG]
  Abdallah Zombe


  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoa wa Mbeya kimeanzisha mkakati wa kumwanika aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe kwa kuwaeleza wananchi katika mikutano ya hadhara jinsi anavyodaiwa kushiriki mauaji ya wafanyabiashara wa mkoa wa Morogoro kama hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilivyotolewa na Mbunge wa Arusha, Godbless Lema hivi karibuni Dodoma bungeni.
  Mkakati huo wa kumshambulia Zombe umeanza rasmi jana ambapo Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigija, aliwasomea mamia ya wananchi wa kata ya Ruanda jijini Mbeya walioshiriki mkutano wa hadhara wa chama hicho, hotuba ya kambi ya upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani.
  Akisoma hotuba hiyo kwa wananchi ambayo alidai imeletwa mkoani Mbeya ikitokea Dodoma, alisema Zombe hana sababu za kuanza kumshambulia Mbunge wa Arusha, Lema kuhusu yeye (Zombe) kushutumiwa kuhusika na mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro.
  Mwambigija alisema Zombe anapaswa kutambua kuwa Lema alisoma hotuba hiyo siyo kwamba yalikuwa ni mawazo yake binafsi bali yalikuwa ni ya kambi ya upinzani ambapo yeye (Lema) aliiwasilisha kwa sababu ni Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
  Mwenyekiti huyo wa Chadema alidai yeye (Mwambigija) alishaishi Dar es Salaam na kwamba alimfahamu Zombe jinsi alivyokuwa na mtandao wa majambazi na kwamba kwa kuwa Zombe alikuwa mfanyakazi wa Jeshi la Polisi na alifahamu kuwa Godbless Lema alikuwa katika mtandao wa wezi wa magari je alichukua hatua gani.
  Alisema Chadema inamheshimu sana na Watanzania wapenda amani wanampenda Mbunge wa Arusha, Lema na ndiyo maana alichaguliwa kwa kura nyingi na kushika nafasi ya pili kitaifa nyuma ya mbunge wa Ubungo, John Mnyika aliyeshika nafasi ya kwanza.
  Mwambigija ambaye wakati akihutubia wananchi wa kata ya Ruanda huku akisoma nakala ya hotuba ya bajeti ya Kambi ya Upinzani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya mwaka 2011/2012, alisema katika mikutano yao yote watakayokuwa wakiifanya katika mkoa wa Mbeya watahakikisha wanamwelezea Zombe kuwafahamisha Watanzania jinsi anavyodaiwa kushiriki katika mauaji ya wafanyabiashara wa Morogoro hata kama ameshinda kesi.
  Mapema Julai 31, mwaka huu Mkuu wa Upelelezi wa zamani wa Mkoa wa Dar es Salaam, Zombe ameibuka tena na kutoa kauli kwa kudai kuwa siku Chadema kikiingia madarakani yeye atajinyonga na kumshutumu Mbunge wa Arusha, Lema kwamba alikuwa kwenye mtandao wa wizi wa magari.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. P

  Parachichi JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 22, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  huyu zombe naona amechanganyikiwa!damu za watu zinamsuta anaanza kubwabwaja ovyo!
   
 3. J

  Joseph Isaack JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Ye zombe amejitenga na jamii..na anatumia umaarufu wa chadema kama ngazi ya kujirejesha kinyemela...atasema mengi kwani mfa maji haachi kutapatapa.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,947
  Trophy Points: 280
  karusha jiwe kwenye mzinga wa nyuki anategemea nini?
   
 5. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #5
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  sioni sababu ya CHADEMA kuanza kuvutana na Zombe na kwa vile kasema ushaidi anao nazani kinachoitajika ni kumuomba aende mahakamani.
  Pamoja na hayo binafsi naona bado tunasafari ndefu kama mtu aliyekuwa na dhamana ya kupeleleza na hatimaye kupeleka ushaidi mahakamani, leo hii anatuambia anaushaidi ambao amekaanao muda mrefu????
  Binafsi sio mzuri kwenye mambo ya sheria ila nazani huyu alikua anapaswa kufunguliwa kesi ya kutotimiza wajibu, kwa kuwa ifahamike kuwa katika upelelezi huo fedha za umma zilitumika ambazo ni kodi za wananchi ambao walikuwa wanafanyiwa huo uharifu.
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  napita wakuu
   
 7. z

  zamlock JF-Expert Member

  #7
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  mbona ya zombe yana fahamika sana na hizo ni damu za watu zinakula naye sahani moja
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Aug 14, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Nasikia Zombe kaomba uteuzi kupitia ccm kugombea jimbo la Igunga.
   
 9. s

  sirghanam JF-Expert Member

  #9
  Aug 14, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 289
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huyu mzee aya mambo ya kusema atajinyoka anahitaji psychologist haraka, tunafanya utani ila inawezekana kaanza kuchanganyikiwa, genge la ujambazi enzi zake na mahita lilikuwa linajulikana, na polisi walikuwa ni sehemu ya genge hilo. Mzee piga kimya subiri adhabu kwa mungu kwa roho za watu mlizotoa kwa ulafi wenu
   
 10. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #10
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Waswahili husema.Damu nzito kuliko maji, so damu ya watu wasio na hatia inaanza kumrudi sasa Zombe ameanza kuweweseka!
   
 11. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #11
  Aug 14, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zombe aliposema Chadema wakiingia ikulu yeye atajinyonga alimaanisha nini? au kwakuwa anajua wazi kuwa alitenda makosa mengi ambayo hao jamaa kwakuwa anajua hawataki kuleana watayafufua na yeye ataozea jela ama kunyongwa hivyo ni bora ajiwahi?
   
 12. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #12
  Aug 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Zombe au Zombie?
   
 13. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 14, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Bosi wake Mahita alitafuta majambia na kuyaweka nembo ya CUF, aliyaonyesha kwa waandishi wa habari.
  Aliapa CUF hawawezi kutawala, ni kweli?
   
 14. aye

  aye JF-Expert Member

  #14
  Aug 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  dhambi inamtafuna uyo
   
 15. 3squere

  3squere JF-Expert Member

  #15
  Aug 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 928
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Jamani zombe hanatumia masaburi kuwaza sio jamani
   
 16. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Anachezea sharubu za simba.
   
 17. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Amini usiamini!DAMU ya mtu haiend bure.Siku si nyingi mtamsikia ikila kwake.
   
Loading...