Zombe na 5bln.

Don Alaba

Senior Member
Nov 3, 2010
167
18
Serikali yetu haileweki haki ya Mungu, Zombe leo hii naye anadiriki kusema hakutendewa haki wakati anakamatwa na kupelekwa mahakamani hatimaye gerezani, wakati akiwa mkuu wa polisi hakuyaona haya wengine wakitendewa kama yeye na bado yanaendelea, kweli sheria msumeno, na mkuki kwa nguruwe binadamu mchungu.
 
Ifike mahali serikali iwe inawachunguza wanaodai fidia kama kweli hizo pesa wanazoomba kama fidia ndio thamani kweli ya huo utu wao uliodhalilishwa. Kwa kuwa huwezi kuomba pesa ambazo hazifanani na kiasi ulichojilimbikizia au ulichopoteza kutokana na kudhalilishwa. Kama ndio hivyo huyo Zombe atuambie hizo 5bn yeye anaziomba kwa misingi gani.
 
Serikali yetu haileweki haki ya Mungu, Zombe leo hii naye anadiriki kusema hakutendewa haki wakati anakamatwa na kupelekwa mahakamani hatimaye gerezani, wakati akiwa mkuu wa polisi hakuyaona haya wengine wakitendewa kama yeye na bado yanaendelea, kweli sheria msumeno, na mkuki kwa nguruwe binadamu mchungu.

Sijakupata ndugu, hapa Zombe kavunja Sheria ipi hasa au tuseme ulitaka adai fidia ya TSh ngapi hasa?
 
Back
Top Bottom