Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 2,144
- 3,459
KUBEHNELA AU KUPUTILA
👉 Pichani hapo inaonesha zoezi la kubehnela ama kuputila. Ni njia za asili na jadi kabisa walizokuwa wanatumia wazee wetu.
👉 Njia hii ilitumika kuondoa degedege kwa watoto tena haraka tu ndani ya siku moja, kuunga sehemu iliyovunjika, kuondoa mapepo mabaya ambayo mtu amerushiwa au yamemvaa kwa bahati mbaya, kuondoa majini ya uwanga kwa wale wanaotolewa kichawi usiku bila wenyewe kujua, kutoa laana mbalimbali kwa mwanadamu.
👉 Huwa panatumika madawa mbalimbali ya miti, mafuta ya nyonyo katika kuunga mifupa hata kama umekanyagwa na wanyama wenye uzito mkubwa, nyungo za asili, vipeo, vyungu, nk.
👉 Leo hii tiba hizi zimepotea katika jamii na kuonekana hazifai, zimepitwa na wakati, ushirikina, imani potofu na kila aina ya neno lisilofaa.
👉 Matokeo ya usasa tuliotaka na kudharau asili yetu tumekuwa mateja wa madawa ya kisasa kwa kila kitu, hatujiwezi wenyewe, tumekuwa dhaifu kimwili na kiroho, kitu kidogo tayari mtu ameshakimbilia madawa ya kizungu, tumepoteza jicho la 3.
👉 Tumepoteza sana ubora wetu kiasi cha kuwa mazuzu tunaoendeshwa na wengine na tunaona ndio ujanja.
👉 Leo magonjwa mbalimbali yanatengenezwa ili kutunyanyasa, kutunyonya, kutuendesha, na kututawala.
👉 Mwafrika ukirudi kwenye asili yako hakuna ugonjwa wa kukutisha. Tuwakumbuke wazee na tuwaenzi hakika kuna mengi tutayapata.
👉 Hakika asili ina majibu juu ya maswali yetu mengi, tiba, kinga, maono, nk.
👉 Tumepoteza uono wetu wa asili (jicho la tatu/third eye) ambao haukuhitaji nguvu kubwa katika kujua mambo yajayo, yaliyopo, na yaliyopita, kujua ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba jamii, leo tumekuwa wakiwa dhahiri.
👉 Utashangaa jambo likitabiriwa na mzungu au kwa kutumia vifaa vya kizungu basi linakubalika na kuonekana la msingi, ila likitabiriwa na mtu mweusi kwa njia za asili linaonekana la uongo na halifai.
👉 Mpaka sasa kuna watu hawaamini kama mtu anaweza kuyaona yatakayotokea kesho au mwakani au miaka kadhaa ijayo. Lakini mambo haya yalikuwepo na bado yapo kwa baadhi ya jamii.
👉 Kwa jinsi tulivyopotezwa kuna baadhi ya watu wanakuambia wao hawana asili wala jadi eti kisa tu yeye na wazazi wake ni wakristo au waislamu. Ujinga mkubwa.
"TUSIDHARAU WAZEE