TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Kwa Chama chochote cha siasa kufanikiwa kinahitaji kuwa na Viongozi wenye mapanzi ya kweli na Chama husika.Mapenzi ya kweli kwa Chama husika huja pale MwanaCHAMA anapokuwa amekitumikia Chama kwa muda mrefu sana tangu utotoni (Chipukizi) hadi utu uzima wake.Kukitumikia Chama muda mrefu hivyo kunakufanya uwe hisia za upendo juu ya Chama hicho.Kuna aina flani za hisia unazitengeneza juu ya Chama kwa vile umekuwa nacho kwa muda mrefu.Zitto alishawahi kusema kuwa hataweza kuondoka Chadema kwasababu ana mapenzi nacho ya dhati,Najua kuna baadhi ya watu walichukulia kauli ya Zitto kama mzaha flani hivi ila kwa sisi tuliosomea Organizational behavior study tumemuelewa vizuri sana.Zitto anafaa sana kukiongoza Chadema kwasababu hajawahi kuwa Mwanachama wa Chama kingine.Mbowe,Dr Slaa,Tundu Lissu na wengieo wote hawa walitokea CCM na wana unasaba na CCM kwa asilimia kubwa.MwanaCHADEMA jiulize kwanini baada ya Zitto kutimuliwa na Chadema hawa CCM hawaonekani kumchangamkia kama ilivyokuwa kwa akina Mwampemba?Kaa tafakari.