Domo Kaya
JF-Expert Member
- May 29, 2007
- 531
- 60
Na Aristostariko Konga
Raia Mwema.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anawaona wanaombeza uteuzi wake kwenye kamati ya kuchunguza mikataba ya madini wanacheza na uelewa wake wa mambo. Zitto, Mbunge wa Chadema ameiambia Raia Mwema katika mahojiano maalumu yatakayochapishwa wiki ijayo, kuwa uteuzi huu wa Rais Jakaya Kikwete hauwezi kumfunga mdomo kama ambavyo wasioupenda wanavyodhani.
" Ninaweza kudiriki kusema kwamba nipo compfrtable (Ninia amani, Nimeteuliwa) na uteuzi wa Rais, sidhani kama imekuwa ni njia ya kuninyamazisha, siamini hivyo. Nadhani watu wanacheza tu na suala hili muhimu kwa taifa.
"Inawezekana kuna wana CCM ambao wanadhani uteuzi wangu ni njia ya kuninyamazisha. Kamwe siwezi kunyamaza. Hao kuwa na wazo hilo ni kuchezea tu maslahi ya nchi.
"Kama kuna watu wanadhani kuwa kamati hiyo ni mtego wa kisiasa, bado wako wrong. Kama wanadhani kuwa uamuzi wa Rais kuniteua mimi ni njia ya kuninyamazisha, basi hao wanacheza tu.
"Inabidi watu wafahamu kuwa suala la uchunguzi wa mikaaba ya madini ni la ,maslahi ya taifa. Sijui ni la kisiasa. Ni suala la ulinzi wa maslahi ya taifa letu anasema Zitto.
Habari zaidi zimesema kwamba kati ya Makundi ambayo hayafuhahishwi na ujumbe wa Zitto katika kamati hiyo ni baadhi ya wenzake kwenye chama na baadhi ya makampuni yenye kumiliki migodi.
Raia mwema imehahamishwa kwamba kampuni moja ya migodi ilipata kuwasiliana naye ili atembelee moja ya migodi yake mara baada ya kuwa imeibua hoja ile ya Buzwagi lakini baadaye safari hiyo ikashindikana kwa kuwa yeye alitoa masharti magumu.
Wakati tukienda mitamboni kulikuwa na habari kwamba Kamati kuu ya chadema inakutana Jumamosi pamoja na mambo mengine, kujadili suala la ujumbe wake katika kamati hiyo.
Alipoulizwa jana jumanne kuhusiana na mkutano huo wa kamati kuu, Zitto alisema "Nitaheshimu maamuzi ya kamati kuu. Hiki ni chama nilichohusika kukijenga tangu nikiwa na miaka 16 na mwanafunzi wa kigoma sekondari. Sioni kuwa chama kinaweza kufa eti kwa kuwa mimi ni mjumbe wa kamati ya madini.
" Kuwa mjumbe katika kamati mimi si wa kwanza ndani ya chadema.. Mbona nimepata kuteuliwa na Kamati ya Africa Mashariki? lakini pia mbona pia kuna wabunge wa chadema ambao ni wajumbe kwenye kamati mbalimbali?
"wacha kamati mbona wabunge wetu wanaandamana na viongozi wa Serikali nnje, na hivi tunapozungumza wengine wako na safari?
:Muasisi wa chadema, ambaye mimi namheshimi sana mzee Edwin Mtei ameteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utafiti wa Kahawa, sasa ukiangalia yote hayo sioni mantiki ya yote hayo ambayo yanaibuka sasa" alisema Zitto.
Alisema katika mahojiano kwamba anuhakilishi ummna kuwa hawezi kufunga kinywa chake kutokana na uteuzi huo wa wajumbe wa kamati hiyo.
Alisema suala hilo si ushindani wa CCM na CHADEMA, ingawa amesikia baadhi ya watu wengine wasikisema kwamba baadhi ya wajumbe wa kamati hii ni marafiki wa Waziri wa Nishati na Madini Nazir Karamagi, ambaye alishiriki kutia saini Mkataba wa Buzwagi, ambao ndio ulioibua mjadala ktk Bunge, na kupelekea Zitto kusimamishwa ubunge hadi January mwakati.