Zitto vs Kafulila(CAG Report Part III)

Besta Mlagila

Member
May 29, 2018
82
150
#Zitto : Serikali inaficha madeni ya mifuko ya hifadhi.

#Kafulila : Hoja yako Zitto ina Matobo matatu, Kwanza ni changamoto ya madeni yenyewe kwa namna yalivyopatikana. Sio siri kwamba kabla ya JPM, mifuko ya hifadhi iligeuzwa shamba la bibi na mali ya genge fulani.Huu ni ukweli unaothibitishwa na taarifa ya taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya E& Y ya Disemba 2015 na habari za uchunguzi za majarida makubwa ya kimataifa kama Africa Confidential na Africa Research Institute.

Kwa mfano, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, mifuko ilikuwa ikidai jumla ya TZS 5.3Trilioni lakini baada ya ukaguzi deni halali likakutwa TZS.3.2Trilion sawa na deni hewa la zaidi ya TZS.2.1Trilion....sasa wewe Kiongozi unayesisitiza deni lilipwe kama lilivyo including "Deni Hewa" hapo utasema kweli una mapenzi na watanzania walipa kodi? Hata kama huna mapenzi na walipa kodi wa nchi hii vema uwe japo na huruma basi!

#Zitto : Serikali ya JPM ina kesi nyingi kwa kuvunja mikataba.

#Kafulila: kesi hizo ni matokeo ya mikataba mibovu ya zamani ambayo JPM amerithi kutokana na udhaifu mkubwa huko tulikotoka na sio mikataba ndani ya awamu ya tano...mfano uamuzi wa Serikali kufuta mkataba wa kampuni ya kufua umeme ya Symbion iliyorithi mitambo ya Dowans/ Richmond, imepunguza mzigo wa kinachoitwa tozo ya gharama ya uwekezaji ( capacity charges) kwa mwezi kutoka dola milioni 16.35( zaidi ya bilioni 37.6)mpaka dola milioni 9.75 ( sawa na bilioni 22.4) kwa mwezi( Rejea CAG report 2017).

Inahitaji ukatili sana kwa Taifa lako kumlalamikia JPM kufuta mikataba mibovu kama Symbion kwani kinachoitwa tozo ya ya gharama za uwekezaji ni mfano wa mbaya wa mikataba ya hovyo ambapo mwekezaji analipwa bila kujali amezalisha umeme au la eti kufidia gharama alizotumia kuwekeza... zama za Serikali kulipa madeni ya mikataba mibovu tumeshavuka. Huko tulikotoka Serikali iliwahi kulipa deni la Dowans kinyemela kiasi cha dola milioni 94 ( zaidi ya bilioni 200 wakati huo).Hakika inahitaji roho ya kikatili kuzitamani tena zama hizo, ni Taifa la 'wapumbavu' tu linaloweza kupigania Serikali yao ilipe madeni ya aina hii!

#Zitto : Serikali imeshindwa usimamizi wa uchumi.

#Kafulila : Nikupe Pole ndugu yangu Zitto kwa kupoteza Memory, ktk kuijibu hoja hii Mfu hapa sitagusa mapinduzi makubwa sekta za miundombinu, maji, Elimu na Afya...twende na ripoti za Tafiti tu;, Mwaka 2017,kwa mara ya kwanza katika historia Tanzania ilifanyiwa uhakiki kuhusu uthabiti wa kiuchumi kuweza kukopesheka ( Credit rating), kazi hii ilifanywa na Taasisi ya Moody's ambayo ni ya kwanza kwa ukubwa duniani katika kazi hizi( inamiliki asilimia 45% ya soko), ilitoa matokeo yake mwezi Machi2017, kuonesha kwamba Tanzania ina daraja la B1 juu ya Kenya, Uganda ambazo zilikuwa na B2. Ripoti hii ilizua mjadala mkali sana Kenya( Business Daily, 4th, March2017).

Mwaka 2018, Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa uchumi jumuifu( Inclusive Economy) , na ya tatu kwa bara zima ikitanguliwa na Algeria na Tunisia( World Economic Forum 2018).Sikatai kwamba kuna mengi ya kufanyia kazi zaidi, lakini rekodi hizi ni kubwa na fahari kwetu kama Taifa kwamba tunakwenda vizuri katika maeneo mengi kuhusu ujenzi wa uchumi
Mwaka 2017, IMF, iliitaja Tanzania kuwa miongoni mwa Mataifa manne ya Afrika yanayoelekea safari ya Vietnam katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. Nchi zingine ni Nigeria, Kenya na Ethiopia. Rejea mahojiano ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( IMF), Bi Christine Lagarde, alipohojiwa na Jarida la Quartz akiwa Addis nchini Ethiopia alipotembelea Tume ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika( UN- Economic Commission for Africa).
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,237
2,000
David Kafulila! Moja ya vichwa adimu sana kuwahi kutokea kwenye lile Bunge la awamu ya nne pamoja na wenzake akina Mkosamali, nk. Ila ndiyo hivyo tena, hana namna! Angekua bado yuko upinzani, huenda angeiongelea kwa namna tofauti kabisa hiyo ripoti ya CAG!

Siyo mbaya. Siasa ni Sanaa, ni Sayansi.
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
5,597

Nampongeza Kafulila kwa uchambuzi huu makini..hii mtu yoyote akiisoma atakubali kichwa kimeandika, na sio ule utumbo wa Zitt
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,635
2,000
Unamuuliza Nani jomba Sasa, kwani viwanda vinabebwa mgongoni watu wanatembea navyo..nenda kavitafute vinapofanya kazi..hapa hakuna wa kukupa jibu..
Tunajua US, China, UK nk wana viwanda na hutajawahi kwenda kwenye hizo nchi. Iweje hivi vya hapa kuvijua ni mpaka ukavitafute?
 
Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
5,597
2,000
Tunajua US, China, UK nk wana viwanda na hutajawahi kwenda kwenye hizo nchi. Iweje hivi vya hapa kuvijua ni mpaka ukavitafute?
Tanzania Ina zaidi ya vuwanda 4000 mpaka Sasa..huna haja ya kwenda kuvitafuta Kama unavyosema
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,635
2,000
Tanzania Ina zaidi ya vuwanda 4000 mpaka Sasa..huna haja ya kwenda kuvitafuta Kama unavyosema
Unaongea utoto gani we dogo? UK yenyewe haina idadi hiyo ya viwanda na inaitwa nchi ya viwanda, kisha Tanzania iwe na hivyo viwanda na bado iwe chini ya Kenya kwa viwanda?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom