Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,111
- 34,943
Naona machozi yako yako karibu hata kudondoka.Kwa ujumla ni kwamba pale ambapo maslahi ya wanene yanakuwa in jeopardy usitegemee transparency! I guess we gt to live with that until when we will be able to demand an account from what they do! I dare to say natamani tungekuwa kama Indonesia ambao wakotayari kufa kwa maslahi ya nchi yao au Ukraine walipiga kambi mwezi mzima kwenye baridi wakidai haki yao! Watawala wote duniani wana tabia moja "Hujifanya miungu wadogo" hutiisha na kuadabisha, na pale ambapo watawaliwa watanyamaza na kusubiri miujiza wao hushangilia huku wakituvisha vilemba vya ukoka!
Siioni Tanzania ya watanzania ambao wako tayari kulala barabarani wakiumwa mbu kwa maslahi ya Taifa lao! Wakati ambapo mtanzania anakandamizwa kwa kulipishwa nauli mpaka mtoto mdogo wa chekechea, wawekezaji wakubwa wanapewa misamaha mikumwa ya mafuta! Hivi kweli inaingia akilini unatoa msamaha wa bil 96 halafu ili upate mrabaha wa bil 28 for God sake! I mean where is their brain! Hivi ubinafisi ndo uko hivi kweli! Wapi tulipokosea mpaka watu wanasahau maadili ya utu na utumishi mwema!
Wana JF - tatizo langu na huyu Mbunge controversial ni kwamba ana uthibitisho gani kuwa hizo Sh 70 bilioni zilirudishwa na wezi, au ni maneno tu ya akina JK and Co? Ametumwa kupiga debe kuwa hizo hela kweli zilirudi physically? naye akiwa kama Mwenyekiti wa hiyo Kamati yake, aliziona nyaraka kuonyeshas kweli zilirudi. ni akina nani hao waliorudisha? Ni hao wale ambao hawakupelekwa mahakamani, kama vile akina RA? walirudisha zote au nusu nusu tu na kusamehewa mahakama?
Zitto anaweza kutuambia majina ya waliorudisha kila mmoja na kiasi gani? Au ameamua kusaidia kuimba wimbo wa akina Mkullo na Hosea, kutuvunga eti hela zilirudi na kununulia pembejeo?
Je watanzania hatustahili kuhakikishiwa hilo kimaandishi?
Ndugu wana JF,
Kwa kitambo nimekuwa siandiki humu ila ninasoma kila siku na kila kitu katika Jukwaa letu. Napenda kumwuliza Zak Malang hapa aonyeshe wapi mimi nimesema pesa za EPA nilirudishwa.
Kuna kundi la watu humu ndani lina Zittophobia. Hawaoni raha bila kusema kitu kuhusu Zitto na hata kufikia kubumba masuala ili tu kujiridhisha roho zao kwa kumsema Zitto. Hainishughulishi sana hata hivyo, ila ninaomba muwe na chembe ya ukweli basi.
Habari hii ya gazeti la Mwananchi inahusu kiasi cha fedha za EPA ambazo hazijafanyiwa uchunguzi (42bn) na tulitaka nazo zifanyiwe uchunguzi. Juhudi zote za kufanya hivyo zimegonga mwamba. Katika habari hii hakuna hata sehemu moja inayoni nukuu nikisema fedha za EPA zimerudishwa. Kama kuna sehemu hiyo naomba nionyeshwe!
EPA ilikuwa ina sehemu mbili - 91bn na 42bn. 91bn ndio taarifa yake kwa umma ilitolewa na hata hizo kesi mnazoona. 42bn kamati ya Rais ilishindwa kujihakikishia uhalali wake na ilitakiwa wataalamu wa masuala ya forensic audit waweze kufanya uchunguzi. Mpaka sasa serikali haijafanya uchunguzi huo.
Kuna kosa Mbunge kukumbusha? Au mwandishi wa thread hii ana interest na hataki uchunguzi huo? Maana tunajua kuna watu walifaidika katika hili kundi wanataka habari ife na wanachukizwa tunapoiibua.
Wachangiaji nao wameingia katika bandwagon ya Zitto bashing kwa ujinga wa kutojua suala lenyewe na wengine kufurahisha nafsi zao.
Hebu muwe fair basi!
Na Ramadhan Semtawa
[COLOR=Navy[COLOR=red]]"MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe amesema kuna ugumu katika kuzipata Sh42.6 bilioni zilizobaki katika uchunguzi wa fedha za EPA kwa kuwa hadi sasa haijulikani zilipo[/COLOR]".
Huu mwanzo wa hii habari peke yake hauko safi sana kwako na inaonyesha kama huu ni uandishi wa kihuni basi Mh Zitto unatakiwa kuwaeleza waombe radhi la sivyo kulishtaki gazeti hili. La sivyo inatakiwa basi kutuelimisha kuwa apart from the 42.6bln mentioned umemaanisha nini basi kuwa hizo nyingine zimepatikana? Au zimesamehewa? Au ndiyo zinawahusu washitakiwa? Je zilizorudishwa hata kama ni miln moja ziliwekwa akaunti gani na zimetumikaje?