Zitto:Uchunguzi wa EPA kiini macho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto:Uchunguzi wa EPA kiini macho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Apr 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Na Ramadhan Semtawa

  MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe amesema kuna ugumu katika kuzipata Sh42.6 bilioni zilizobaki katika uchunguzi wa fedha za EPA kwa kuwa hadi sasa haijulikani zilipo.

  Fedha hizo ni kati ya Sh139 bilioni zilizochotwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), ambazo wizi wake ulibainika katika mahesabu ya kati ya mwaka 2005 na 2006. Tayari Sh70 bilioni zimesharejeshwa na wezi baada ya kuahidiwa msamaha huku zaidi ya watu 20 wakifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kuiba, kushiriki au kula njama za kuiba fedha hizo.


  Uchunguzi wa wizi huo mkubwa haukuweza kubaini fedha hizo kutokana na mpango wa kuzichota kuhusisha mitandao iliyovuka mipaka, tatizo lililomfanya Rais Jakaya Kikwete kuunda kikosi kazi cha kuchunguza fedha hizo mwaka mmoja uliopita.


  Kiasi hicho cha Sh42.6 bilioni kinatajwa kuchotwa na makampuni 9 ambayo nyaraka nyingi za kughushi zinaonyesha kuwa kampuni hizo zinatokea nje ya nchi, ikiwemo kampuni ya Marubeni ya Japan.


  Akizungumza na gazeti hili jana, Zitto alieleza kuwa tatizo kubwa linaweka wingu katika upatikanaji wa fedha hizo ni kampuni ya M/S Lazard Freres kutopewa hadidu za rejea za kushughulikia wizi huo.


  Agosti mwaka juzi Rais Kikwete alikiongezea muda kikosi kazi hicho kuendelea kutafuta kiasi cha Sh42.6 bilioni ambazo kumbukumbu zake nyingi ziko nje ya nchi hivyo kuhitaji ushirikiano wa nchi husika, ikiwa ni pamoja na polisi wa kimataifa, maarufu kama Interpol.


  Hata hivyo, Zitto anaona hakuna matumaini tena ya kurejeshwa kwa fedha hizo baada ya kuona ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma, alisema tatizo kubwa ni kampuni ya Lazard haikupewa hadidu za rejea kukagua kiasi hicho.


  Lazard, ni kampuni iliyo na makao yake nchini Ufaransa na ambayo imeingia mkataba na BoT kwa ajili ya kukagua deni halisi la EPA na kama kuna wadai halali wanaopaswa kulipwa na au taasisi hiyo kuu ya fedha ya nchini isilipe madeni hayo, na athari zinazoweza kutokea kama isipolipa.


  Zitto anaamini kuwa Lazard ni kampuni ambayo ina utaalamu ambao ungeweza kusaidia kubaini fedha hizo zilipo kama ingekuwa imepewa hadidu za rejea za kufanya hivyo.


  "Hadi sasa mambo yanaonekana kuwa magumu... unajua Lazard ndiyo ilipaswa kukagua hizo fedha lakini katika hadidu za rejea haikupewa kufanya hivyo, kwa hiyo kuna tatizo," alisema Zitto akionyesha wasiwasi.


  Takwimu za awali zinaonyesha kuwa hadi mwaka 1999 deni ambalo serikali ilitakiwa iwalipe wadai wake kutokana na fedha zilizotengwa EPA lilifikia dola 623 milioni za Kimarekani, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni za Kimarekani.


  Mwaka jana, kamati hiyo ya Zitto iliitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuipa kazi kampuni ya Lazard kukagua wizi wa kiasi hicho cha fedha ikisema kuwa ina uzoefu na uwezo wa kitaalamu, tofauti na kikosi kazi kilichoundwa na rais.


  Hata hivyo, Waziri wa Fedha na Uchumi alisema mamlaka ya kugeuza uchunguzi huo yalikuwa ni ya rais ambaye tayari aliunda kikosi kazi chini ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Johnson Mwanyika, ambaye kwa sasa amestaafu.


  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu aliwahi kuliambia gazeti hili kuwa taasisi hiyo isingeweza kuipa Lazard kazi ya kukagua kiasi hicho kwa kuwa tayari rais alishaunda kikosi kazi


  Chanzo: Gazeti la Mwananchi
   
 2. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa ujumla ni kwamba pale ambapo maslahi ya wanene yanakuwa in jeopardy usitegemee transparency! I guess we gt to live with that until when we will be able to demand an account from what they do! I dare to say natamani tungekuwa kama Indonesia ambao wakotayari kufa kwa maslahi ya nchi yao au Ukraine walipiga kambi mwezi mzima kwenye baridi wakidai haki yao! Watawala wote duniani wana tabia moja "Hujifanya miungu wadogo" hutiisha na kuadabisha, na pale ambapo watawaliwa watanyamaza na kusubiri miujiza wao hushangilia huku wakituvisha vilemba vya ukoka!

  Siioni Tanzania ya watanzania ambao wako tayari kulala barabarani wakiumwa mbu kwa maslahi ya Taifa lao! Wakati ambapo mtanzania anakandamizwa kwa kulipishwa nauli mpaka mtoto mdogo wa chekechea, wawekezaji wakubwa wanapewa misamaha mikumwa ya mafuta! Hivi kweli inaingia akilini unatoa msamaha wa bil 96 halafu ili upate mrabaha wa bil 28 for God sake! I mean where is their brain! Hivi ubinafisi ndo uko hivi kweli! Wapi tulipokosea mpaka watu wanasahau maadili ya utu na utumishi mwema!
   
 3. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hii ilishatabiriwa!

  Hivi kuna mtu alitegemea lolote kutokana na zile kesi tangu mwanzo! Hayo ni mazingaope tu waliona upepo mbaya wakaamua kuanzia maigizo hayo! In real sense kwa mtu mwenye akili tangu mwanzo ilikuwa ni uigizaji tu!
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Naona machozi yako yako karibu hata kudondoka.
  Nji hii ndivyo ilivyo. Ukiiangalia wakati mwingine unajikuta machozi yanadondoka yenyewe.
  Iko siku!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wana JF - tatizo langu na huyu Mbunge controversial ni kwamba ana uthibitisho gani kuwa hizo Sh 70 bilioni zilirudishwa na wezi, au ni maneno tu ya akina JK and Co? Ametumwa kupiga debe kuwa hizo hela kweli zilirudi physically? naye akiwa kama Mwenyekiti wa hiyo Kamati yake, aliziona nyaraka kuonyeshas kweli zilirudi. ni akina nani hao waliorudisha? Ni hao wale ambao hawakupelekwa mahakamani, kama vile akina RA? walirudisha zote au nusu nusu tu na kusamehewa mahakama?

  Zitto anaweza kutuambia majina ya waliorudisha kila mmoja na kiasi gani? Au ameamua kusaidia kuimba wimbo wa akina Mkullo na Hosea, kutuvunga eti hela zilirudi na kununulia pembejeo?

  Je watanzania hatustahili kuhakikishiwa hilo kimaandishi?
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umenena Zak. Bado hatujafafanuliwa nani alirudisha kiasi gani, lini, na vipi alishughulikwa. Ni vungavunga tu ambayo Zitto anaiendeleza kwa niaba ya wanaoumtumia. Kama vile alivyoingilia kupiga debe mitambo michakavu ya Dowans inunuliwe na serikkali.

  By the way, nashangaa kwa nini wasiendeleze vunga zao kwa kusema kwamba kati ya hizo Sh 70 bn zilizorudishwa, zimo pia zile za Kagoda Sh 40 bn (au sehemu yake kubwa). Wanaogopa nini, kwani tumeshazoea vunga.

  Na yujko wapi yule mama wa CCM wa mapambano dhidi ya ufisadi, Mbunge Anne kilango aliyesimama Bungeni na kusema kuwa atahakikisha feddha zinarudishwa physically kwa viroba, na siyo kwa matamshi tu au makaratasi?
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Tatizo la Tanzania ni kuendekeza siasa za uwongo
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Pia inawezekana kabisa gazeti la Mwananchi linamfanya Zitto aonekane silly. Naye kaingia kichwa kichwa! That's what I gather kwani gazeti hilo ni experts kwa shughuli hiyo!
   
 9. Y

  Yetu Macho JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamaa katika hili anachemsha kwa mara nyingine tena. Ni dhahiri kama mbunge wa pande pinzani alitakiwa asimame kudai umakini zaidi katika uchunguzi na kuitaka serikali ihakikisha recoverability ya hizo pesa leave alone watoe visibitisho vya hizo wanazodai wamerecove.

  Kuonyesha kwake kukata tamaa na kuridhika na hali ya serikali kutofuatilia ipasavyo suala hili, kunazidi kumuondolea sifa yake ya umachachari na kunazidi kuwaongezea wadau wasisasi juu ya mabadiliko ya misimamo ya huyu bwana.
   
 10. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Tanzania ni WATANZANIA WENYEWE.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Yetu macho na siasa za Bongo
   
 12. R

  Ronaldinho Member

  #12
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto as many other Tanzanian politicians,he is just an opportunitist!there was a time i though i like him only to realise he has no thrust for change
   
 13. h

  housta Senior Member

  #13
  Apr 14, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tukumbuke kuwa wote hawa ni wanasiasa.Bado sijaona mtu ambaye kweli ametokea kuwa mwanasiasa na akasimamia kiukweli maslahi ya nchi.Kila mtu ana price yake.Kama Truman alinunuliwa itakuwa Zitto?Porojo nyingi zinazosemwa ni kwa ajili ya uchaguzi.Huyo Mhe. Kilango alikuwa nguvu ya soda na pia ipo kama alikuwa anatumiwa tu.Mafisadi wote wanajua kuwa hakuna mtu kwenye serikali hii anaweza kuwasemesha chochote.Nguvu itatoka kwa wananchi.Wananchi ndio wanaowaweka hawa viongozi.Chagueni watu makini.Your votes count!
   
 14. G

  Godwine JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2010
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  tatizo si viongozi wa siasa tatizo ni wananchi
   
 15. Zitto

  Zitto MP Kigoma Urban

  #15
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 2, 2007
  Messages: 1,197
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana JF,

  Kwa kitambo nimekuwa siandiki humu ila ninasoma kila siku na kila kitu katika Jukwaa letu. Napenda kumwuliza Zak Malang hapa aonyeshe wapi mimi nimesema pesa za EPA nilirudishwa.

  Kuna kundi la watu humu ndani lina Zittophobia. Hawaoni raha bila kusema kitu kuhusu Zitto na hata kufikia kubumba masuala ili tu kujiridhisha roho zao kwa kumsema Zitto. Hainishughulishi sana hata hivyo, ila ninaomba muwe na chembe ya ukweli basi.

  Habari hii ya gazeti la Mwananchi inahusu kiasi cha fedha za EPA ambazo hazijafanyiwa uchunguzi (42bn) na tulitaka nazo zifanyiwe uchunguzi. Juhudi zote za kufanya hivyo zimegonga mwamba. Katika habari hii hakuna hata sehemu moja inayoni nukuu nikisema fedha za EPA zimerudishwa. Kama kuna sehemu hiyo naomba nionyeshwe!

  EPA ilikuwa ina sehemu mbili - 91bn na 42bn. 91bn ndio taarifa yake kwa umma ilitolewa na hata hizo kesi mnazoona. 42bn kamati ya Rais ilishindwa kujihakikishia uhalali wake na ilitakiwa wataalamu wa masuala ya forensic audit waweze kufanya uchunguzi. Mpaka sasa serikali haijafanya uchunguzi huo.

  Kuna kosa Mbunge kukumbusha? Au mwandishi wa thread hii ana interest na hataki uchunguzi huo? Maana tunajua kuna watu walifaidika katika hili kundi wanataka habari ife na wanachukizwa tunapoiibua.

  Wachangiaji nao wameingia katika bandwagon ya Zitto bashing kwa ujinga wa kutojua suala lenyewe na wengine kufurahisha nafsi zao.

  Hebu muwe fair basi!
   
 16. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2010
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Zitto heshima mbele, Hope unaendelea vyema Bucerius. Mungu akutangulie.

  Well, nadhani ni vema wewe uelewe nafasi yako katika jamii. Wengi humu tunategemea MEDIA kama vyanzo vya habari. NA kama ulivyosema waandishi wetu wengi hawako makini katika kujenga habari inayoeleweka.

  Lakini vile vile lazima ujue kwamba watu hapa "they have too much expectations in you" sasa sijui kama hilo ni kosa lao au lako wewe uliyewajengea hayo mazingira. Mimi my point is: EPA imekuwa nuksi and most Tanzanians we feel cheated kwa sababu its all talk talk..no body is doing what we common people can feel kwamba we are being taken into account.

  Zitto, wala usiwaite watu kwamba ni wajinga. No. Ni kwa sababu wanakuona wewe ndo mtetezi wao wa kuaminiwa, sasa ikitokea habari kama hii ya mwananchi (ambayo wengi wetu ndo source ya information) ni rahisi kuelewa kwa nini mleta mada kaja na speed aliyokuja nayo. By the way, wewe ndo unaelewa hizi details za EPA na who did what and not..common people tunaelewa tuu kwamba EPA ni mabilion yaliyoibwa na wakulu. Sasa ni jukumu lako kuwaelewesha wananchi hapa..usifikiri kila anayeandika humu ana uelewa wa kisomi kama wewe au Mwanakijiji.

  Just take your time, compose yourself and inform wananchi. Thats politics. Usiwe na hasira kama wananchi wako sisi. Sisi tuknaweza kuwa frustrated na maisha. Sasa kama kiongoi wetu wewe inabidi..u-calm down..utupe hatua swala lilipofikia.


  Masanja
   
 17. consigliori

  consigliori JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 390
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Kweli umeshambuliwa bure katika hili Mheshimiwa, Zak Malang alitakiwa kuwauliza Mwananchi maswali yake kwa sababu badala ya kuandika tayari mil 70 inadaiwa zimerejeshwa wao wanaandika tayari mil 70 zimerejeshwa. Sasa uhakika huo Mwananchi wameupata wapi, kama si upotoshaji wa wanahabari wetu.
   
 18. M

  Myamba Senior Member

  #18
  Apr 14, 2010
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli kwamba hizi kesi hazina mbele wala nyuma. Wewe tazama tu ushahidi unaotolewa pale hujui shahidi yupi ni wa serikali na yupi ni wa defendant!! Utata mtupu wandugu zangu!!
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jamani jamani Zitto zitto watu wanakutumia bila ya wewe kujua NDO UNAKUFA KISIASA
   
 20. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
   
Loading...