Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Kiongozi Mstaafu wa Chama cha Act Wazalendo Zitto Kabwe, amesisitiza kuwa chama hicho kimejipanga kikamilifu kupambana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi ujao, kwa lengo la kuhakikisha demokrasia ya kweli inatamalaki nchini.
Zitto ameyaeleza hayo Septemba 29, 2025 akiwa Same Mashariki Mkoani Kilimanjaro, katika muendelezo wa ziara ya Mikoa 4 aliyopangiwa na chama kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 12, 2025.
Soma > >
- Zitto Kabwe: Wanamuogopa sana Luhaga Mpina, ndio maana wakamuweka vizingiti
- Zitto Kabwe: Wale ambao viongozi waliosekwa ndani, Luhaga Mpina ndiye rais atakaye waachia huru
Kuhusu mgombea wa Urais, Luhaga Mpina, Zitto amesisitiza kuwa chama kitaendelea kupigania haki yake hadi pale atakaporejeshwa rasmi kuwania nafasi hiyo. Wakati huohuo, ACT Wazalendo inaendelea kuimarisha kampeni zake za kuwania viti vya Ubunge na nafasi nyingine za uongozi.