Zitto: Sitagombea uongozi CHADEMA


kwenye red tu ndo mashaka yangu yalipo. kama angekuwa makini kama enzi zile za kutimuliwa bungeni ningeunga kwa nguvu ya tano, lakini kwa sasa ningependelea awe mwanachama tu, kwa kwa sasa Zitto hana tofauti na mimi ninayetoa maoni yangu nikiwa nyuma ya pazia.

Kimsingi amebadirika, kuna baadhi ya mikakati ya kichama hakubaliani, kwa mfano tangu ianzishwe M4C, sidhai kama amewahi kuizungumzia kitu hii. Sasa akiwa mwenyekiti halafu haipendi M4C, si atatuangusha chini huyo?
 
mbowe aendelee tu kuwa mwenyekiti mpaka chadema itakapoingia madarakani ila Dr.Slaa awe mgombea urais,Mnyika awe katibu,zitto waziri wa mambo ya nje,Lema waziri wa mambo ya ndani
 
vyama vingine watu makini wachache mpaka inakuwa shida kupanga safu ya uongozi
 

Mbona Unamkimbilia ZITO KABWE? Si yeye Kasema hataki UONGOZI ndani ya CHADEMA ila tu Nafasi ya Kugombea

URAISI tu... Hapendi Kuwa MTU wa kusimamia ITIKADI za CHAMA anataka awe FREE kuwa MASHUHURI yeye

Mwenyewe Sasa UKIMPA Uongozi Ndani ya Chama - Kila asemacho kitaenda kuwa sifa kwa Uongozi wa Chama Chake

Ni Selfish na Umimi ndio MAPENZI YAKE...
 

Safi sana kamanda Zitto.Kumbe ulishakuwa na mawazo mazuri kama haya ya kupunguza baadhi ya majukumu yako.
 

Hayo mawazo yako mazuri ila yawe baada ya 2015,mbowe abaki kuwa m/kiti,slaa abaki palepale,zito sijui tumweke wapi,labda nafasi ya zito tumpe HECHE
 

Wana-CHADEMA wataamua kidemokrasia nani awe M/kiti na katibu wao
 
kwa maoni yangu nafasi zibaki vile vile isipokuwa nafac ya zitto apewe henche
 
hahahaha!!,mwanasiasa kijana machachari na mwerevu kutoka moja ya chama cha upinzani pande za Tanzania aendelea kuwajambisha mahasimu wake ndani ya chama baada ya kuonyesha kua mtata(haelewek) chezea zitto weye!
 

napenda mtazamo wa Ipande na mtoa mada. chama cha siasa si mali ya mtu bali. tulisikia mala nyingi ccm wakisema chama hicho kinawenyewe na matokeo yake leo tunayaona. nivyema viongozi wetu na wananchi wakaliona ili. kwamba uongozi wakupokezana na kujengeana uwezo ktk hilo ni muhimu. reference nzuri ni Nyerere na mandela kwa upande watu afrika. Lakini pia ushauri wangu kwa chadema: viongozi wote wa chama wapimwe kwa uwezo wao na mapenzi ya kulitumikia taifa lao.

Leo hii najiuliza sana kuhusu uwezo(kiakili)na na jinsi (style) viongozi wetu wakubwa serikalini. mmoja wetu hapa jf husema 'hakili ndogo kuongoza hakili kubwa' . hili halikubaliki. Bilashaka katiba ya chama chama chadema na katiba inayokuja ya Tanzania vitakuwa na dira sahihi ya upatkawa viongozi ktk taifa wetu.
 

napenda mtazamo wa Ipande na mtoa mada. chama cha siasa si mali ya mtu. Tulisikia mala nyingi ccm wakisema chama hicho kinawenyewe na matokeo yake leo tunayaona. nivyema viongozi wetu na wananchi wakaliona ili. kwamba uongozi wakupokezana na kujengeana uwezo ktk hilo ni muhimu. reference nzuri ni Nyerere na Mandela kwa upande watu afrika. Lakini pia ushauri wangu kwa chadema: viongozi wote wa chama wapimwe kwa uwezo wao na mapenzi ya kulitumikia taifa lao.

Leo hii najiuliza sana kuhusu uwezo(kiakili)na na jinsi (style) viongozi wetu wakubwa serikalini. mmoja wetu hapa jf husema 'hakili ndogo kuongoza hakili kubwa' . hili halikubaliki. Bilashaka katiba ya chama chama chadema na katiba inayokuja ya Tanzania vitakuwa na dira sahihi ya upatikanaji viongozi ktk taifa letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…