Zitto: Siondoki chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto: Siondoki chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mungi, Dec 25, 2010.

 1. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  [​IMG] Awataka wanachama waendelee kukijenga chama chao
  [​IMG] Afafanua yanayotokea ni tofauti za fikra, mawazo  [​IMG]
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe


  Hatimaye Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema kuwa hatakihama chama hicho licha ya mambo mengi yanayozungumzwa juu yake.
  Tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu, Zitto amekuwa akilalamikiwa kutokana na matukio kadhaa kwa madai kuwa anakihujumu chama hicho.

  Moja ya malalamiko dhidi yake, ni hatua yake ya kutoa kauli mbalimbali nje ya vikao vya chama kuhusiana na tofauti zilizojitokeza wakati wa kuamua kama wabunge wa chama hicho wasusie hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya kulizindua Bunge la Kumi mjini Dodoma Novemba 18, mwaka huu.

  Zitto na wabunge kadhaa hawakuingia bungeni siku hiyo na baada ya hapo amekuwa akitoa kauli kupitia vyombo vya habari kutetea msimamo wake kwamba alikataa kususia hotuba ya Rais Kikwete kwa kuwa anamheshimu Rais.

  Hatua yake iliibua mjadala mkubwa katika jamii na katika vyombo vya habari na mitandao huku mbunge huyo akishutumiwa kuwa anakisaliti chama kwa kauli yake kwamba anamheshimu Rais wakati msimamo wa Chadema ni kutomtambua Rais kutokana na ushindi wake katika uchaguzi mkuu kuwa na utata.

  Baadhi ya wabunge wa Chadema walimlalamikia Zitto katika chama na Kamati Kuu iliunda kamati ya kumsikiliza Zitto, ikiongozwa na Profesa Mwesiga Baregu.

  Baada ya kimya cha siku kadhaa, jana Zitto akiwahutubia wanachama na wapenzi wa chama hicho mjini Kigoma, aliwaeleza kwamba hana mpango wowote wa kuhama Chadema.

  Zitto aliwaomba wapigakura wake kutosikiliza mambo yanayosemwa dhidi yake badala yake waendelee kukijenga chama chao.

  Alisema kuwa kinachotokea sasa katika Chadema ni kutofautiana kwa mawazo na fikra na kwamba hilo ni jambo la kawaida katika jumuiya yoyote.

  “Ndugu zangu, naomba niwaeleze leo. Najua mmekuwa hamuelewi, maana yake mara mnaambiwa Zitto anahama chama mara hivi. Ni kwamba mimi ni Chadema na sitahama kwenda kokote, labda kuna wanaotaka nihame, lakini mimi sihami,” alisema Zitto huku akishangiliwa na umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano huo.

  Aliongeza: “Muelewe wenzangu wa Kigoma mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine, hivyo mambo yote yanayojitokeza kwangu ni kwa sababu ya mtazamo wa baadaye.

  Alisema kuwa tofauti zinazojitokeza ndani ya chama chake zisiwafanye wananchi wa Kigoma kuwa na hofu yoyote na kwamba yale yanayoandikwa katika vyombo vya habari, pia yasiwanyime raha waendelee kukisimamia chama chao.
  “Wananchi wenzangu msiwe na wasiwasi, mimi ni mzima kabisa, yameandikwa mengi katika vyombo vya habari, mara nimepewa sumu,” alisema Zitto na kuongeza:

  “Nataka niwahakikishie hizo habari si za kweli, mimi sijapewa sumu na hakuna binadamu anayeweza kunipa sumu, tuendelee kufanya kazi na kukijenga chama chetu.”

  Katika hatua nyingine, Zitto aliitaka Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi wa Meya katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji ndani ya wiki moja.

  Uchaguzi huo ulisimamishwa na Tamisemi wiki iliyopita kufuatia mkanganyiko wa mgao wa madiwani wa viti maalum ambapo Chadema kilipata viti vinne na Chama Cha Mapinduzi (CCM) viti vitatu.

  Alisema kuendelea kusitisha kufanyika kwa uchaguzi huo katika manispaa hiyo ni uvunjaji wa haki kwa kuwa tayari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imekwishamaliza kazi yake ya kuteua madiwani wa viti maalum ila kinachoendelea sasa ni kuchelewesha maendeleo ya wananchi.

  Alisema chama hicho kimemwandikia barua Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mwenye dhamana na Tamisemi kulalamikia juu ya hatua hiyo na kumtaka aingilie kati.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...