Lingine nataka kuongea nanyi ni suala la Bajeti ya Serikali na Utekelezwaji wake. Serikali ilileta Bungeni Bajeti ya matumizi ya shilingi 29.5 trilioni mwaka 2016/17. Katika hiyo, ilitarajia kupata mikopo na misaada kutoka nje pamoja na mikopo ya kibiashara ya shilingi 5.7 trilioni.
Kutokana na mahusiano mabaya kati ya Serikali na nchi marafiki, mpaka sasa nusu ya mwaka wa Bajeti imekatika na Serikali haijaweza kupata hata thumni katika matarajio hayo. Vile vile Serikali imeanza kukusanya chini ya matarajio kwenye kodi na mapato yasiyo ya kikodi.
Miradi ya Maendeleo imechelewa kutekelezwa kwa sababu Serikali inafanya kazi ya kulipa mishahara na kulipa madeni tu. Ndio maana miradi mingi inayozinduliwa hivi sasa hakuna mradi mpya bali ni miradi iliyoachwa na Serikali ya Awamu ya Nne.
Serikali hii inahitaji kurekebisha mahusiano yake na nchi marafiki zetu ili uchumi wetu usisimame. Masuala haya Rais hawezi kuambiwa na Mawaziri wake kwa sababu amejenga hulka ya kuogopwa. Sisi wa Upinzani ni lazima tumwambie maana ni wajibu wetu.
Katika Barua (letter of intent) ambayo Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu wameandika kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Serikali inasema inataka kukopa mikopo ya kibiashara (syndicated loans and Eurobond) ili kupata fedha. Hata hivyo Mabanki ya Dunia yanataka kujua 'Credit Rating' ya Serikali yetu.
Hiyo pekee itachukua miezi mingi iwapo mfumo wa kawaida wa zabuni utapaswa kufuatwa. Hata hivyo IMF wameiambia Serikali kuwa soko la mikopo ya dunia hivi sasa ni baya maana Serikali itakopa kwa gharama kubwa, mpaka riba ya 9% kwenye fedha za kigeni.
Serikali inataka kuiingiza nchini kwenye madeni ghali kwa sababu tu ya kutaka kufanikisha Bajeti isiyotekelezeka, iliyotungwa kwa sifa bila kuzingatia uhalisia wa nchi yetu. Kwa maoni yetu sisi ACT Wazalendo, Bajeti ya Serikali haikupaswa kuzidi shilingi 24 trilioni.
Ushauri wetu kwa Serikali ni kuitaka ikae chini na kuleta Bajeti ndogo Bungeni ili kurekebisha Bajeti iliyoko kulingana na uwezo wetu kama Taifa ili kujiepusha na mikopo ghali itakayoumiza wananchi.