Zitto ni sauti halisi ya Kijana shupavu wa Kitanzania, Usipomtaja mchana utamtaja Usiku

Faru John II

Senior Member
Dec 27, 2016
134
135
Kwa Wanaomjua vizuri Zitto Zuberi Kabwe tangu alipokuwa akisoma Kigoma Secondary wataungana namimi kuwa Zitto Kabwe ni mwanasiasa wa kipekee sana.

Majaribu kwa Zitto Kabwe yamekamata sehemu kubwa sana ya maisha yake tangu alipokuwa kijana mdogo sana. Uwezo ambao Mungu alimpa wa kubadilika kwa haraka sana kuendana na mazingira kumemfanya azidi kuwa imara na kuwa na hoja na mvuto wa kipekee sio tu alipoingia bungeni. Zitto ni Komandoo ambaye uwezo wake hata adui zake wanaujua vizuri.

Zitto Kabwe kwa wasiomjua vizuri hupenda kuropoka kuwa anatumika na CCM ila kwa Wanaomjua vizuri wanakwambia Zitto Kabwe amekuwa akipingana na Serikali kabla ya mfumo wa vyama vingi kuingia Tanzania.

Tumeona Wanasiasa wengi watata kama yeye akina Chacha Wangwe wakipoteza maisha kutokana na hila ila yeye Mungu alimnusuru na hila hizo and really "Zitto had been a central target ever since ". Huwezi kumvizia Zitto Kabwe hata siku moja ukamkamata waulize wenzio walimshindwa tangu akiwa sekondari na chuo kikuu cha Dar es Salaam ndio kuna habari zake nyingi sana.

Vijana wa Kigoma hupenda kumwita "KIRIKOU" kutokana na umahili wake ktk siasa za Upinzani na heshima kubwa aliyowapelekea watu wa Kigoma ambao kabla yake ilikuwa wanaona aibu hata kujitambulisha kuwa wao wanatoka Kigoma.

Mh. Mbowe amewahi kusikika akisema Zitto ni mwanasiasa mwenye akili sana "Very intelligent politician" kwa kuwa anajuwa kuwa heshima aliyowahi kuileta Zitto ndani ya Chadema hakuna yoyote yule mwenye uwezo wa kuthubutu kushindana naye.

Wapo ndugu zetu wanajidanganya Zitto amefilisika kisiasa, naomba niwahakikishie kuwa Zitto ni zao la Muhogo linastawi hata kipindi cha kiangazi. Kuminywa kwa uhuru wa habari na mazingira magumu ya siasa za Tanzania kipindi hiki ni mazingira mazuri ya Zitto Kabwe kuimarisha mapambano yake dhidi ya mifumo dhalimu na tawala za akina Jammeh wa Gambia.

Zitto ni sauti halisi ya Kijana shupavu wa Kitanzania. Usipomtaja mchana utamtaja Usiku.

HE IS DIFFERENT
 
Tunawasubiri vibaraka wa Mbowe watie neno.

Pale chama kinapobadilisha katiba yake ili kumuwezesha Mbowe aendelee kuwa mwenyekiti, hii ina tofauti gani na NKURUNZIZA

Na usikute watu hao hao wanaopinga ya NKURUNZIZA wanapongeza ya MBOWE, what a hypocrisy....!
 
uko nje ya mada.
 
Uzi unamhusu Zitto wewe umedakia
Mbowe, au ndio kujitoa ufahamu tu.
 
Wewe jipiganie mwenyewe ndugu usijidanganye kuna mtu anakupigania, watu wanapigania matumbo yao na si vinginevyo!!!!
Kila mmoja atumie nafasi aliyonayo kuwakomboa wenzake. Hao Wanasiasa mende tunaopigana nao vita kila siku Wanajipigania wenyewe ndiyo maana hatuendelei. Kuna watu wasiojiweza wengi tunahitaji kuwa sauti zao kaka.

Dunia haina maana kama wachache tu ndiyo watafurahia maisha
 
Back
Top Bottom