CDM hawawezi kumzuia Zitto kugombea urais au hata kuwa rais,come 2015 tutakuwa na katiba inayoruhusu wagombea binafsi!
Hakuna anayemzuia Zitto Zuberi Kabwe kugombea Urais hata chama hakijawahi kusema kuwa hafai au anafaa. Kwa sasa Chama hakitaki kuingia kwenye malumbano ya Uraisi kwani kuna kazi kubwa chama inakifanya ili ikimsimamisha mgombea wake aweze kushinda. Zito kama kweli nia yake ni kushika nafasi ya juu ya chama na taifa inabidi ajishughulishe kujenga chama aachane na siasa tamaa. kama ni Uraisi anaweza kuwa au asiwe who knows about tmrr.
mpaka leo sijafahamu kwa nini mtu mwenye elimu kama ya zitto afanye mistakes za kitoto kwenye bajeti mbadala namna ile.Mbowe i think u need to do something, coz madhara yake ni kuwa huku kuzunguka nchi nzima mkikitangaza chama ni useless.
Makosa ya bajeti asilaumiwe Zitto, kwani kama zile bajeti na Upinzania zinazosomwa bungeni ni kazi binafsi za wasomaji ni hatari. Mimi ninaamini kila bajeti ya kambi ya upinzani ni bajeti ya chama husika. Naamini kama chama lazima kukubali yale makosa ni ya chama. Ni wajibu wao wabunge wote na kamati za chama kupitia na kuandaa bajeti mbadala na kuzi readproof na kujiridhisha. Chama kina wachumi wengi waliobobea na waandishi. Hivyo msalaba wa makosa wa bajeti ya kambi ni makosa ya kambi sio msomaji.
mim ndo semtawa. nimefuatilia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu kuhusu story ya zitto na urais, taarifa zote kuhusu mim asilimia 99 ni cooked! some stupid guys wanaotumiwa na mafisadi wanadhn wataniyumbisha! jukwaa hli si la great thinkers bali most of them are so stupid! the home of stupid thinkers-jf! haiwezikan jukwaa la great people lijadili watu na ktoa taarifa za uongo, kiwendawazimu na kipuuzi.
Nimesoma post za wengi na Tuhuma juu yako, ni kweli kwamba waandishi wanatumiwa na wanasiasa , wafanyabiashra , wakuu wa serikali na dini-Jibu ni KWELI. Je wanapotumiwa kwa mazuri au kwa mabaya yanaleta mwangi kwa jamii ni kweli. Kama unafanya kazi yako kwa weledi wa kikazi na maadili ya kazi na kutimiza wajibu hunahaja ya kutoa lugha kama hizo hapo juu. just do your job.
Ni kweli kbs zitto huwa haonekani hata kwenye mikutano ya chama chake kama wenzake,hapo utasikia yupo kwenye shughuli nyingine za kichama!.kweli zitto 'huyu'siyo yule.
Zitto amekuwa ni kati ya makada maarufu sana wa CDM ni kweli muonekano wake au kutokuwepo mahali ni rahisi jamii kufahamu, ila ikumbukwe ana majukumu mengi ya kichamam na kibunge, naibu katibu, naibu kiongozi kambi ya upinzani, mwenyekiti wa tume ya kudumu ya bunge, mbunge, nk. Ninaamini anakuwa ama anamajukumu mengine au yuko sehemu nyingine kichama.
Yes ni ukweli kila mtu anaona kupwaya kwake katika chama ila sijui kama ndio mbinu za kukimbia matope kwani kuna msemo unaosema kama unataka kugombea Uraisi lazima uwekwe mambo ya nje ili usisiginishane na wananchi ukija wakuone mpya.
NB:
Zitto ana karama sana ila kwa mwendo wa kikwetu madaraka hulevya na hufikia hatua husahau malengo. tusitukane wakunga wala tusidharau jamvi.
Zitto alipendwa akiwa Chadema na alipendwa na vijana na wazee wote waliona matumaini kwani alifanana nao leo nina wasi wasi kama anafanana na wale aliowaamsha. Siasa inavipindi hata hiki ni kipindi na akiweza kupita anaweza, ila siasa za Kitanzania zenye mizengwe na makundi zinaangamiza sana nyota nyingi zinazoashiria kung'ara. yuko wapi Lamwai, Kaburu, Mrema, Ringo Tenga, seif Sharifu, Nk Mategemeo yetu sio nia zao. Utawajua ukiwapa fedha na madaraka.