Zitto na Wabunge, Zitto na CHADEMA, Zitto na Urais... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto na Wabunge, Zitto na CHADEMA, Zitto na Urais...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Jul 25, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Kijana Zitto Zuberi Kabwe kapata umahiri mkubwa sana kwenye medani ya siasa, anayo mengi ya kujivunia mafanikio ya kisiasa kiuongozi na kiuchumi.

  Zitto ameweza kuwa chachu ya vijana wengine kujiunga na siasa na kushiriki kwenye uongozi bila kujali ni chama gani wengi wa vijana walivutiwa na Zitto na kuona nao wanaweza.

  Ndani ya CDM ameshawishi wengi na wengi wameshawishika kwa ajili ya kauli zake, vitendo vyake ndani na nje ya bunge uwezo wake wa kujenga hoja na mafanikio ya kijana mwenzao ambaye hajatoka kwenye jamii na familia za (Sliver spoon)

  Mategemeo yamekuwa makubwa sana kwa Zitto kushika nafasi kubwa ndani ya chama yakiwa ni maandalizi ya kuandaa viongozi wa sasa na baadaye wa chama na Taifa.

  Kinachotokea sasa mpaka kila mmoja anaogopa kauli za wenzake hata kama zilikuwa na nia njema tu ni hulka ya wanasiasa kupenda madaraka, kusahau wajibu na kujipenda zaidi ya wananchi wanaowafanya wawe hivyo walivyo. Binafsi sioni kwa nini Zitto au yeyote aogope au ashtuke kama Zitto ana nia ya kuwa Raisi wa Tanzania kwani hata mimi nina nia hiyo. Ni nani asiyependa kuwa dean kama yeye ni mhadhiri, ni nina asiyependa kuwa CEO kama yeye ni meneja wa kampuni husika?? Ni nina asiyependa mafanikio ??

  Tatizo hapa ni jinsi ya kufikia malengo. Vijana wa leo hawako tayari kufanya kazi wanapenda vya kunyonga vya kuchinja hawavitaki. Vijana waliopo kwenye vyama vya siasa vinavyokuwa wanaotaka kuingia ikulu halafu hawajengi vyama vyao wanastaajabisha sana; unajiuliza watashinda vipi wakati chama kina sehemu kibao hakina mashina?? Kwa nini tusielekeze nguvu nyingi kujenga chama?

  Unaponunua kundi la kukupigia debe nje ya utaratibu uliokubalika wa chama ulichokikubali unamaanisha nini?? Wakati huu viongozi wengine wakikijenga chama kwa kushughulika kufungua mashina matawi baadhi wanaelekeza nguvu kujipigia debe la Urais hii inasikitisha sana. Je ni kweli makamanda waliopo nyikani kila siku wangekuwa na Tamaa kama za vijana wa sasa chama kingekuwepo?? Kina mzee Mtei, Bob Makani nk walianzisha chama wakijua watakifikisha pahala fulani na wengine waendelee nacho, hawakuwa na tamaa kama za vijana wa leo. Wazee hawa wengi wao wamestaafu bila hata ya kuwa wabunge.

  Kifo cha NCCR mageuzi ni uchu wa madaraka, kila mmoja alijiona ana akili sana kuliko mwenzeka.

  Ni vyema kuwaambia vijana wa CDM waliopata madaraka, Taifa haliko tayari kuwaona wanalumbana kwa uchu wa madaraka na tamaa zao za maisha yao na wanaowatuma. Wananchi tunataka mabadiliko ya kiuchumi ili keki hii kila mtu aile.

  Chadema waweke miiko ya viongozi iwe dira hata wakichukua dola. Leo serikali inayumba kwani ina viongozi wa ajabu wengi kila mmoja akiwa analake na maamuzi yake. Haiwezekani kila mara Tatizo ndani ya CDM lianzishwe na mtu yule yule kwa sababu zile zile.

  Busara ya Zitto na hekima ya uongozi inampotea siku hadi siku, tamaa kubwa ya uongozi aliyonayo na makundi anayoyajenga akitumia wale aliowasaidia ama kufanikiwa kisiasa ama ushawishi wa aina zote inamfanya apotee na kujijengea maadui ndani na nje ya chama.

  Naamini kabisa binadamu anabadilika na anaweza kufikia malengo yake akibadili mwelekeo. Zitto saidia kujenga chama wapiga kura wa kumtea mgombea wa Uraisi huanzia ndania ya chama. Ukishiriki kikamilifu kujenga chama wanachama watakupenda na kukuteuwa kupeperusha bendera, ila kama una nia nyingine endelea.

  Zitto hatuhitaji Raisi anayetumia fedha, makundi, wahariri nk kushinda madhara ya Raisi kuingizwa ikulu na kakundi kadogo kwa watu tayari tunayaona. Utawalipa nini ?? Wanawekeza ili wapate nini??? Tamaa ikizidi huuza utu wa mwanadamu. Unaweza kuwatumikia watanzania bila kuwa Raisi.

  AOGOPWE YEYOTE MWENYE TAMAA YA KUINGIA IKULU. IKULU HAKUNA BIASHARA IKULU NI PAHALI PATAKATIFU. KWA NINI KUTUMIA FEDHA NYINGI ILI KUINGIA IKULU MTAZILIPA VIPI?????

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Tamaa mbaya ndiyo inayoangamiza taifa langu Tanzania
   
 2. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,208
  Likes Received: 3,773
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakuunga mkono miamia katika andiko lako, siongezi wala kupunguza neno ujumbe umefika!
   
 3. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Na hivyo ndivyo CCM wanajihaminisha kuendelea kushinda "milele". Njaa ndio zinatusumbua, hakuna wapiganaji Bali waganga njaa tu.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Watanzania wamejifunza mengi sana tangu 2005. Kwa sasa itakuwa ngumu mgombea (hata wa kata) kusema ni zamu ya wanawake, Makinda katoa somo tosha juu ya umuhimu wa kumchagua mtu kulingana na sifa/uwezo wake.

  Kwenye urais, matumizi ya fedha, mitandao/makundi, umri, muonekano, siasa za kuchafuana na hata ukaribu na vyombo vya habari, yote haya yameshakuwa tested na watu wanajua utamu/ukali wake.

  Naamini watanzania wengi kwa sasa watataka mtu ambaye akipewa suti ya bute atasema NO.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Zitto alikuwa tegemeo kwa walio wengi lakini sasa kabadilika kuwa janga la kichama na kitaifa kiujumla
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Umasikini wa wapiga kura, vyombo vya habari masikini,wanasiasa wanageuka kama vinyonga haya yote ni maanagamizi ya Taifa.

  Binafsi nampenda sana Zitto ila amenikatisha tamaa kwa kiasi kikubwa. Sipendi binadamu asiyeweza kuwa na msimamo. Ukiangalia swala hili la Kigoma na wenzeka huwezi elewa nini hasa kilitokea. Ila kinachoonekana kuna mkono nyuma ya waandishi.

  Vilevile unaona picha ya wazi ya kakundi kanako taka kujiimarisha kwa tamaa ya madaraka. Na unaona weledi wa kumpigania mnyonge imepotea. Huwezi kumjua binadamu mpaka apate fedha.

  Kweli leo tumefika kupigania vyeo wanasahau tulivyowapigania kuwa tu wabunge. Wanasahau kuwa ni sisi tumewafikisha hapo. Kwa nini hizo fedha wasisaidie wananchi badala ya kujenga chuki na uadui.

  Kwa mtaji huu wanaokwenda nao kweli wanajenga chama au wanakiboma. I hate this!!! Tunataka Tanzania yenye viongozi wenye akili timamu, wanaomuogopa Mungu, wacha Mungu na wazalendo wa kweli. Tumechoka kurubuniwa kwa manufaa ya wachache.

  Kazi kubwa tuliyonayo leo ni kuelimisha wananchi juu ya viongozi wasio na uwezo na wenye Tamaa kama Spika Makinda, Jk, na hawa wanaochipukia. Kama kweli mtu anafaa kwa nini asiamini mtandao wa chama mpaka atengeneze wake??? nani mwenye ngvuvu kuliko chama??? Madhara ya Ikulu ya Mtandao JK anamajibu yote. Miaka kumi Nchi haieleweki na hilo linaweza kutokea kwenye chama chochote kama hakuna umakini wa chama.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Anachokifanya Zitto at this stage ni kuweka bayana kuwa Dr. Slaa is not a de facto mgombea wa CHADEMA 2015. Excellent strategy from Zitto as it is obviously resonating.
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Binafsi nimekuwa mpinzani wa Zitto na kukosa kabisa imani naye toka kwenye kampeni za 2010 ambapo alimpigia debe Jk badala ya Dr.slaa, na kubwa zaidi ni pale alijitokeza na kutaka kuondoa concentration kwenye uchaguzi wa arumeru, jamani sio siri tena kwamba yaliyosemwa na saidi kubeneea kuwa Zitto anaumiwa na CCM na kwel yanatimia.
   
 9. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni wapi huko Dr Slaa amewahi kutangaza nia ya kugombea uraisi? Ni kwa nn umsingizie mzee wa watu?
   
 10. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  He has to wait and compete within the party!! Otherwise we can't understand why so early.
   
 11. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Sifa zimeshamharibu sana huyu kiongozi, naweza kuanzia kwenye budget mbadala, sidhani kama kwa jinsi alivyomakini anaweza kukosea kama siyo ilikuwa planned purposely. Ila cha msingi akae akijua watanzania walimwamini lakini badala ya kufanya kile wanachotarajia anaamua kutukimbia!!
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,495
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Mimi kabla hata ya uchaguzi huo....niliona macho yake tu.. anaongea kwa kuigizaigiza hivi..

  Sijawahi kumwona Zitto kama mtu wa maana!! jina tu ndilo lina mpa umaarufu kama lilivyokuwa la Jakaya Kikwete!
  .
   
 13. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  cdm wasipoangalia zitto atakuwa janga lao na taifa kwa ujumla.... Zitto huyu huyu hajishughulishi sana na kampeni za kukijenga chama kama watu wengine tunaowaona kila siku kwenye mikutano yeye kila wanapoonyesha kuwa bize kujenga chama yeye anaibuka na kauli tata za urai. Ebu atuambie nini malengo ya tamasha la kigoma? Imekuwaje liwe sasa hasa chama chake kinapokuwa kwenye kampeni za kujijenga huku yeye akiwa haonekani sana kwenye kampeni hizo?

  ZITTO NI JANGA LA TAIFA...
   
 14. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nakuunga mkono 100% mkuu ,umeandika mambo ya msingi sana.Zitto amesemwa sana humu ila inaelekea yeye ni sikio la kufa.Makamanda walishamwandika kama mtu wenye tamaa na umimi ,walisema tabia hizi alizianza akiwa Tosamaganga .
   
 15. Isalia

  Isalia JF-Expert Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 948
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni vijana wengi wameijua CDM kupitia mgongo wake Zitto lawama mnazompa hazilingani kabisa na alichokifanyia CDM ni kama binaadam anaweza kufanya kosa kwani si anao viongozi wake bac aitwe arekebishwe si vyema kumtupia lawama au kuna kitu nyuma ya pazi
   
 16. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,838
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Siku zote kosa moja huondoa mazuri 100 uliyofanya ama kutenda,huoni utaratibu wa kiutawala.Huwezi kusamehewa kosa eti kwa sababu kuna mazuri, hakuna set off hapa kiongozi lazima siku zote uwe mwadilifu.
   
 17. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Amefanya mengi lakin huyu jamaa hafai,hafai,hafai kabisa.Wenzake wanazunguka huku na huku kukijenga chama,yeye yuko bze na kutangaza nia ya urais,mi nadhani ni kondom ya magamba
   
 18. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,738
  Trophy Points: 280
  Sijui kwa nini Zitto anatulazimisha kumchukia?

  Wassira alisema cdm haifiki 2013 najua walitegemea haya ya Zitto.

  Kamwe Zitto hatoweza kuitawanya cdm!
   
 19. Manyi

  Manyi JF-Expert Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 3,256
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizi ni challenges tu za kwenye mapambano, hata Dr. Slaa alishakumbana nazo sana! Yataisha tu haya Mh. Zitto Kabwe!
   
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,738
  Likes Received: 1,449
  Trophy Points: 280
  Zitto possess one outstanding talent, he never miss an opportunity to create some individual media attention.
   
Loading...