Zitto na UKUTA

Zitto na UKUTA

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria."

Tulisema hayo baada ya kauli ya Rais kuzuia Vyama kufanya Siasa. Wito wetu bado upo pale pale. Hii sio vita ya chama kimoja kimoja. Narudia kutaka wanasiasa wa upinzani, ninawasihi tupigane vita hii pamoja. Tuweke tofauti zetu pembeni.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo.
 
Zito kaoa juzi...mke wake siku hiyo nimuone mbele kwenye maandamano kama mke wa Dr Slaa...Mushumbusi...

Tumestuka...mambo ya kutangaza maandamano kisha mnajifungia majumbani mwenu na familia zenu sisi mnatuweka mbele tudundwe...yamepitwa na wakati...

Wazanzibar tayari wametupa somo zuri...wako kimya wamemgomea ayatollah wa c.uf kuingia barabarani...
 
Tatizo zito wanaona anaweza akawasaliti wenzimake wa upinzani..Lakini wanaweza wakakaa meza moja wakayamaliza.
 
Jamani kwa nini tunarudi kwenye enzi za chama kimoja? Kwa nini tuhofie usalama watu kufanya mikutano ya kisiasa. Kwa nini iwe kwa wapinzani tu. Nashukuru kila tunapowakwanza ndo mwanzo wa kukua kwao. Ni wakati wa kuacha watu kuwa huru kueleza mambo yao ya kisiasa bila kizuizi. Let the democracy take its path. Hofu ya nini wajameni. Chama dola fanyeni mikutano yenu na vyama vingine hali kadhalika.
Mungu atubariki sana watanzania tuweze kutambua democrasia ya kweli.
 
Hii ya Mhe Zitto kuona agenda yake imeporwa na Mbowe, na ametumia siasa nzuri sana hapa. Anajaribu kuisuka agenda yake tena kwa kutaka vyama vya upinzani viunganishwe, alafu atumia jukwaa la chadema kukijenga chama chake.
 
tungekaa tukaambiwa tupiganie katiba mpya atleast madaraka ya rais yapunguzwe nadhani watanzania wengi zaidi wangewasupport,lakini kwa hili mhhhhh,wacha tuone mpaka sasa ninachooamini M4C ndo ilibeba ajenda za msingi kuliko hii kampeni ya kuunga unga isiyo na mbele wala nyuma.......
 
We RG wacha watu wafanye political rallies. Mbona hamjiamini. Hayo ya kuzuia walitufanyia wakoloni. Acha mambo ya kijima hayo!
 
"Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria."

Tulisema hayo baada ya kauli ya Rais kuzuia Vyama kufanya Siasa. Wito wetu bado upo pale pale. Hii sio vita ya chama kimoja kimoja. Narudia kutaka wanasiasa wa upinzani, ninawasihi tupigane vita hii pamoja. Tuweke tofauti zetu pembeni.

Zitto Kabwe, Mb
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo.
What goes around comes around.
Mungu aliumba kusahau. [emoji116] [emoji116]
1469740459614.jpg
UKUTA
 
Zitto acha na hao wakuda, walikuita msaliti, tukahamia wote act, zitto tukijenge chama achana na ukuta.
 
Zito kaoa juzi...mke wake siku hiyi nimuone mbele kwenye maandamano kama mke wa dr slaa...mushumbusi...

Tumestuka...mambo ya kutangaza maandamano kisha mnajifungia majumbani mwenu na familia zenu sisi mnatuweka mbele tudundwe...yamepitwa na wakati...

Wazanzibar tayari wametupa somo zuri...wako kimya wamemgomea ayatollah wa c.uf kuingia barabarani...
Kwani kukiwa na maandamano kuna madhara gani mkuu??polisi si watatulinda??hata kama wakitangulia hao viongozi kwani policcm watawadhuru??(maana hiyo siyo kazi yao)maana naona kama unatahadharisha!hii nchi si ya amani??vitisho vya nini tena??
 
Walishindwa Kuungana Kuitoa CCM madarakani Ili wasipate Huo Udikteta.. leo Mnajiunga Ili ?

Shenzi kabisaaaaa.. Tena Polisi Siku Hiyo watawavunja miguu
Kumbe hiyo ndio kazi ya polisi mkuu???aisee
 
Back
Top Bottom