Zitto na Kitila wavuliwa vyeo vyote ndani ya CHADEMA

Chadema mbona wanataka kuniaminisha yasemwayo kuwa chama chao ni cha kaskazini, Lema na Mwigamba nao hatima yao ni nini?
Bi kilembwe upo? kama cha kaskazini si achana nacho,tatizo liko wapi? nisalimie Giningi waambie nitarudi Giningi siku moja nikiwa full.
Waslaam, M. Mtolewa
 
Leo saa nane mchana ,kamati kuu yote kwa pamoja itatoa tamko la nini kimetokea, Press itafanya ka makao makuu ya Chadema.
 
Ingawa sijafurahia lkn sijashituka kwa uamuzi uliochukuliwa na CC ya CDM dhidi ya Zitto kwani wameonyesha uongozi, uongozi ni uwezo wa kufanya maamuzi hata yale magumu, ambayo CCM hawajaweza.
Zitto amekuwa controvesial sana kwa muda mrefu, hivyo nawashauri Zitto na Kitila (hasa Zitto) watulie na kukubali maamuzi ya Chama. Reaction yoyote dhidi ya maamuzi ya Chama, yatanifanya nikubali kwa 100%, kuwa Zitto alikuwa anahujumu CDM kwa maslahi yake. Nawashauri wafanye kazi za chama kwa bidii kurudisha imani.
 
Wanajamii,

Ni vyema kutambua kuwa ngozi nyeusi ina matatizo kuliko ngozi yoyote duniani.Afrika ndio bara lenye vikundi vingi vya waasi,ndio bara lenye migogoro mingi,ndio bara ambalo kila matokeo ya uchaguzi hupingwa nakadhalika. CCM ina bahati ilizaliwa kipindi kilichohitaji muungano wa wote ili kutokomeza ukoloni lakini hata hivyo baada ya hapo tofauti zilijijenga.

Wakati inaonekana kuimarika kwa upinzani ndio kumepamba moto, nguzo kuu ya upinzani yaani Chadema inavunjika pole pole. Bila kutizama suala hili kwa undani, lazima ikubalike kuwa viongozi waliovuliwa vyeo ni influential hata kama ni negative influence.

Ni dhahiri kwa sasa kuwa CCM haitotolewa madarakani na si kwa sababu ya uimara wake bali ni udhaifu wa wapinzani wake
 
chama kimejaa udini,ukanda na ukabila bila kusahau mizengwe kama simba na yanga na wote huo ni uoga wa zitto kutaka kugombea uenyekiti wa chama...hiyo ni dhambi ya ubaguzi itawatafuna mpaka iwamalize
 
Tulisha zungumza juu ya huyu jamaa muda mrefu na kama kuvumiliwa amevumiliwa sana. Simpendi sana mnafiki katika kazi!!
 
Si kwamba nafurahia yaliyotokea hapana sababu sikuwepo ndani ya kamati kuu ya chama ila kinachonifurahisha ni ukomavu wa chama. Kwanza Mh. Zito hajafukuzwa uanachama bali kavuliwa nyazifa zake ndani ya chama ilo la kwanza
la pili kapewa muda wa kujitetea ambao ni siku 14 autetee uanachama wake ndani ya CHADEMA.
Hii inaonesha ukomavu wa chama hiki na sijutii kua "muumini" wao japo si "mwanachama" wao.
Angalizo..muumini ni kwamba ukiweka mgombea mwenye sifa na vigezo namchagua
.mwanachama...iwe isiwe yoyote uliyemuweka ni lazima nimchague
 
Maamuzi Magumu yako wapi hapo,katika hivyo vyeo Zito na Kitila walikua wanapata nini?hivyo vyeo vinamsaidia Mbowe na Slaa na awala yake!kumuondoa mtu katika nafasi ni maamuzi magumu??????????????????????????????????je sisi CCM ambao kabla ya miaka kumi tumebadilisha nafasi ya Katibu mkuu mara tatu,makamba,mukama,kinana:mbona hatusemi maamuzi magumu,je mkiamua kumtoa Silaa ukatibu mkuu mtaita maamuzi ya nini?fanyeni uchaguzi,hizo Saccos tu kunauchaguzi
Jua ZZK hakuondoka CDM kwa mazuri. Hao uliowataja waliondoka ama kwa kustaafu au kuona kuwa pengine kuna mwingine anaweza zaidi. ZZK ameondolewa kwa uhaini wake kwa CHAMA!!! Kwa hiyo ni maamuzi magumu!!! Hakuondolewa kwa uchaguzi, bali kwa kamati kuu kwa kuona nidhamu yake ni mbovu. Kwanza naona CDM walichelewa sana kufukuza hili nyau.
 
Hongera sana kamati kuu...Haya ndiyo maamuzi magumu tuyayoyaongelea...Hakuna aliye juu ya chama. Nimeridhika na wahusika watekeleze maagizo ya kamati kuu ili tusonge mbele kulikomboa taifa.. Kuhama chama sio uzalendo, bali kutatua matatizo ya chama na kukubali madhaifu yetu ni zaidi ya ujasiri. Kiongozi wangu Zitto na Mwl. wangu Mkumbwa hizo ni changamoto na tunataraji kuona ukomavu wenu ndani ya siasa kwa kutii. Sitarajii hasa kwa uwezo wenu na nguvu ya kitaaluma mtaanza kukimbizana na media.!! Onesheni utofauti na wanasiasa uchwara na muweke historia ya kuonywa na kuonyeka. Najua bado chama kinawahitaji mbali na hitilafu za kisiasa.

Shime Kabwe na Kitila kuweni imara tukaikomboe nchi. Mioyo ya watanzania ipo CDM na haitaweza kubadilishwa kwa ninyi kukihama chama. Kaeni ndani ya chama...huku kutaongeza mshawasha kuelekea kule tunapopataka na kufika kwenye ile safari tuliyoipigania miaka nenda rudi.

Hongera tena kwa Mbowe na kamati kuu kwa maamuzi tofauti na ilivyozoeleka.
Tulianza na Mungu, Tunasonga na Mungu, Tutamaliza na Mungu.
Peeeeeplezzzzz.....Poweeeeerrr....

NAIPENDA CHADEMA!
 
Mapinduz ni kazi ngumu sana,wengi wanayakimbia na wengine yanawagharimu hadi uhai,


Marehemu chacha wangwe alijaribu lakini mungu hakupenda aendelee kuweepo dunian,zitto amejaribu lakin kinachotokea kila mwenye macho anaona sasa,Chadema ilidhan kuwa inaweza kuongoza nchi kwa kigezo cha ukanda na ukabila,lakin muda umewahukumu,

Zitto kabwe hata kama angekuwa ni mchaga bado asingepewa nafasi ya kuaminika ndan ya chadema,unajua kwanin??

JIBU UNALO,LAKIN HAIWASIDII CHADEMA,NA KAMA KWELI WAO WALIKUWA WANAHUBIRI DEMOKRASIA NA UTAIFA UKANDA NA UKABILA WANAOUKUMBATIA NI WA NINI??


VYOVYOTE VILE IWAVYO,MBOWE HIYO NAFASI YA UENYEKITI ATAIACHIA TUH,HATA KAMA ATAENDELEA KUNG'ANG'ANIA HAPO JUU,YEYE NI MWANADAMU,IPO SIKU ATAKUFA NA MWINGINE ATAKUJA KUZIBA NAFASI HIYO NA UHALISIA UTAFAHAMIKA HATA KAMA WANAFICHA FICHA BAADHI YA MAMBO,HAKUNA MAREFU YASIYO NA NCHA
 
Back
Top Bottom