Zitto na Kitila wavuliwa vyeo vyote ndani ya CHADEMA

Hongereni sana cc.juzi niliuliza swali hapa jukwaani who is zzk hapa jukwaani mana kila ukiingia jukwaani hukosi habari za zzk.nafikiri usemi wa wahenga umetimia"ngoma ikivuma sana mwishowe hupasuka"tusubiri majibu yake hapa jamvini tuone atakuja single gani tena.naona taa ya hatari imekwisha washwa

Mkuu subiri baada ya kufukuzwa kama utaona jina la Zito jukwaani,atapotea kama Kafulila alivofulia.
 
Hizo sera zenu ni mfu,mlianza na uraia,ukabila na udini hamumpati mtu labda yale mazuzu yanayotumiwa na magamba bila kujijua...
Safi sanaaaaaaaaaa chadema..

Kosa lenu kuwafanya kanda zingine WAJINGA,wenye AKILI ni nyinyi tu,watu wana macho na wana masikio.
 
Nimepata faraja kubwa sana kwa maamuzi haya ya chadema kwani kama hamuwezi kudhibitiana ndani ya chama basi hata nchi hamuiwezi. Huyu kijana Zitto ilifika mahala akajiona ni maarufu kuliko chama na kuamua kufanya mambo pasipo kukishirikisha chama kwa manufaa binafsi tena yenye nia ya kufurahisha wapinzani wa chama chake. Sasa kuna uwezekano wa kupoteza ubunge, unaibu kiongozi kambi ya upinzani bungeni, uenyekiti wa kamati ya bunge kuhusiana na hesabu za mashirika ya umma nk. Hii itampunguzia platform kadhaa
 
wilbroad slaa,ndiye masterminder wa hili picha lote hadi hapa tulipofikia,

ukitaka kuliamin hili ni pale alipokuwa anawatuma vifaranga vyake kuja kumchafua zitto kisha yeye kutokea hapa hadharani kama katibu mkuu kuja kushngilia uovu ule,hilo amethibistisha kwamba yeye sia ina ya kiongoz anaestahili kupewa dhamana ya kuongoz taifa,,

siku kadhaa zilizopita slaa alitokeza kwenye vyombo vya habari na kuwaambia wananchi kwamba hawana tatzo na zitto ila kuna watu nje ya chama wanawagombanisha,watu hao ni ccm,,sasa leo kiko wapi anageuza gari bila kuwasha indicator na kuja na picha kama hili??chadema lazima itambue kuwa haiwez kuongoza nchi kwa kuendekeza siasa za ukanda na ukabila hata siku moja

nilikuwa namheshmu sana lakini ameshatekwa na siasa za kna mbowe na mhuni lema...huyu babu si bure kaiba mke wa mtu
 
Jana Lumumba FC walikuwa wanasema Zitto ni kisiki cha mpingo leo wanaanza kulialia oh tuelezwe sababu,

Once again nasema ndani ya Chadema hakuna aliye maarufu kuliko chama.
 
Nafikiri we should be realistic je tunajenga au tunabomoa?Hoja haijibiwi kwa vitisho na kufukuzana sasa km atatokea mwingine atahoji matumizi ya fedha nae atafukuzwa?Sidhani km ni fair trial kwa hawa watu wawili!!!
 
Kamati Kuu iliyoketi na kufanya uamuzi wake ni ya CHADEMA.Zitto Z. Kabwe ni mwanachama wa CHADEMA. Atajitetea kwa CHADEMA. Atasikilizwa na CHADEMA. Kama kuachwa au kufukuzwa,ni CHADEMA watakaoamua. CCM yangu inahusikaje na suala la uamuzi wa CHADEMA kwa Zitto?

Leo hata chai hainyweki. Kila kada hapa ni Zitto tu mdomoni. Mara ameonewa;mara haiwezekani;mara lazima abaki CHADEMA. Kwanini? Basi tusubiri afukuzwe CHADEMA ili tumchukue chamani. Kwanini mnataka muopiganie abaki CHADEMA mtu mnayempenda kuwa naye!? Hebu tuache mambo hayo

Tangu asubuhi, Ipad na simu zinzhusika na Zitto tu. Hizi ni mali za chama jamani. Ni amali ya CCM. Kwanini tuongelee Zitto wa CHADEMA? Tafadhali tuendelee na kazi zetu za chama kwakuwa utekelezaji wa Ilani yetu bado unaendelea na wanachi watatuhoji hapo 2014 na 2015 kwenye chaguzi.Hawatatuuliza kuhusu CHADEMA.

Tupige kazi makada wenzangu;ushindi wa 2014 na 2015 ni wetu!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Mkuu hii inadhihirisha kuwa Zito alikuwa muhimu kwa CCM akiwa Chadema kwa manufaa ya CCM. Mhemuko walionao wachangiaje wengi kutoka CCM unadhihirisha hivyo na ndio uliochangia kwa kiwango kikubwa anguko la Zito. VUTA-NKUVUTE, ukiwa na mke ukaamua kumuadhibu au kusudio la kumuacha kwa kumtuhumu ana mahusiano na jirani nawe unataka kumrudisha kwao kisha jirani huyohuyo anapiga kelele " usimwache wala kumfukuza huyo ni mke mwema kaa naye tuu" kama hujashtuka wewe mjinga. Anataka aendelee kukaa nawe ili ampate kirahisi huyo maana hana shida ya kumuoa ila kula kwa ulaini.
Good morning Mzee Tupatupa wa Lumumba.

 
Cdm acheni ukaskazini. Mbona hao wakaskazini wanamadudu mengi lakini hawachukuliwi hatua? Zzk ni Mzalendo wakweli daima nitamheshimu kwa kutoa hoja zenye manufaa katika nchi masikini kama yetu. Katiba ikiruhusu mgombea binafsi Zitto simama. Kuna watu tuna imani kubwa sana na wewe ila hatuna imani na watu ulionao wanaokumbatia udini,ukanda na ukabila.

Kuwaambia chadema wapeleke hesabu sao kwa Msajili ili sifikishwe kwa CAG kukaguliwa!
udini,ukanda na ukabila mmeuleta nyie?. Akiguswa Zitto tu hoja zenu ni hizo.. Kwa unafiki mnashabikia CCM ambayo kabla ya uchaguzi 2015 mtaihama kwa sababu hizo hizo!!! Utakuwaje CCM kisha ukawa mtetezi wa mpinzani kama wewe siyo mnafiki?
 
Wilbroad Slaa,ndiye Masterminder wa hili picha lote hadi hapa tulipofikia,

Ukitaka kuliamin hili ni pale alipokuwa anawatuma vifaranga vyake kuja kumchafua zitto kisha yeye kutokea hapa hadharani kama katibu mkuu kuja kushngilia uovu ule,hilo amethibistisha kwamba yeye sia ina ya kiongoz anaestahili kupewa dhamana ya kuongoz taifa,,

Siku kadhaa zilizopita Slaa alitokeza kwenye vyombo vya habari na kuwaambia wananchi kwamba hawana tatzo na zitto ila kuna watu nje ya chama wanawagombanisha,watu hao ni CCM,,SASA LEO KIKO WAPI ANAGEUZA GARI BILA KUWASHA INDICATOR NA KUJA NA PICHA KAMA HILI??CHADEMA LAZIMA ITAMBUE KUWA HAIWEZ KUONGOZA NCHI KWA KUENDEKEZA SIASA ZA UKANDA NA UKABILA HATA SIKU MOJA
Wewe wajina tu huna hoja...
 
Back
Top Bottom