Shakidinkili
JF-Expert Member
- Sep 28, 2013
- 458
- 174
Hivi karibuni pamezuka malumbano makali kupitia vyombo vya habari kati ya M/kiti wa Kamati ya Bunge ya PAC na baadhi ya vyama vya siasa vinavyopokea ruzuku kutoka serikalini.
Nimefuatilia sana ili kujua kiini cha malumbano na ukweli uko wapi. Nionavyo mimi. Zito alikwepa kuitupia serikali lawama za moja kwa moja, badala yake alichokoza kwa kuvilaumu vyama kwa kutowasilisha mahesabu yao yakakaguliwe. Jana 21/10/2013 usiku studio za Star TV zilikuwa na kipindi chenye mada iliyohusu RUZUKU YA VYAMA VYA SIASA.
Wageni waalikwa waliohudhuria walikuwa Julius Mtatiro wa CUF na Anthony Komu wa CHADEMA. CCM na vyama vingine vinavyotafuna fedha za kodi hawakuwa na wawakilishi, sijui kwa kutoalikwa au wenyewe waliingia mitini kwa kuiogopa mada. Kilichotokea, CUF na CHADEMA wameuthibitishia uma kuwa vyama vyao vimetimiza yote kwa mujibu wa sheria.
Mahesabu yao mpaka Dec 2011 yamewasilishwa kwa CAG ili yafanyiwe ukaguzi lakini Ofisi ya CAG imeshindwa kukagua ati kwa madai wana upungufu wa RASILIMALI WATU NA FEDHA kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Bahati mbaya sana kwangu niliyekuwa ninafuatilia kipindi hicho, ukweli ulipoanza kubainika kuwa matatizo yako kwa watendaji serikalini, tangu 2009 sheria ilipoanza kutumika mpaka leo serikali, yaani Waziri mwenye dhamana hajaweka/ hajatayarisha kanuni za namna ya kutekeleza sheria hiyo nk, star TV ilizimika ghafla na kutoa maandishi (weak signal) na baadaye (scrambled channel).
Siamini kama star TV ilizimika kwa bahati mbaya kwa matatizo ya mawasiliano, kama ndivyo hivyo, star TV kama mlirekodi kipindi hicho, mimi binafsi ninaomba mkirudie ili tuone ukweli mpaka mwisho wa kipindi. Mh. Zito ulichofanya, mimi ninakupongeza kwa sababu ulitupia mpira kwenye viwanja vya vyama vya siasa, CUF na CHADEMA wameupiga huo mpira umekwenda kutua kwenye penalty box la serikali. Tuisubiri serikali tuone itatuambia nini sisi walipa kodi wa nchi hii.
Vyama ambavyo havikuhudhuria kipindi basi Mungu avibariki vifike na vikalale salama huko JEHANAMU.