tunduruboy
JF-Expert Member
- Mar 16, 2013
- 423
- 218
WABUNGE wa CHADEMA; Zitto Kabwe (KigomaKaskazini) na John Mnyika (Ubungo), wame wachochea wabunge wenzao wasihudhuriesemina iliyoandaliwa leo na Wizara ya Nishati na Madini.
Sababu waliyoitoa wabunge hao juu ya ushawishi huo ni kuwa serikali imeanza ugawaji wa vitalu vipya vya mafuta na gesi kwenyebahari kuu na Ziwa Tanganyika Kaskazini.
Hatahivyo, hatua hiyo imeonekana kuwagawa wabunge, ambapo baadhi wamepinga nawengine kuunga mkono.
Kupitia taarifa zao kwa vyombo vya habari walizozituma kwa nyakati tofauti, Zitto na Mnyika wamepinga uamuzi wa serikali wa kuanza mzunguko wa nne wa ugawaji wa leseni za utafutaji na ugunduzi wa gesinchini.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari,Zitto ameonesha kushangazwa na uamuzi huo wa serikali, kwani Tanzania bado haijawa na sera ya gesi asilia nakwamba ndiyo kwanza wabunge wamepewa rasimu ya sera hiyo kwa ajili ya kutoamaoni yao.
"Kesho Jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya gesi asilia. Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo," alisema Zitto na kuongeza;
"Jambo la kushangaza ni kwamba wakati sera yagesi asilia ipo kwenye rasimu na ndiyo kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, serikali tayari imetangaza tena kugawa vitalu vya mafuta na gesi kwenye bahari kuu naZiwa Tanganyika Kaskazini."
Pia katika taarifa hiyo Zitto ameelezea kushangazwa na hatua hiyo ya serikaliambayo alisema inakwenda kinyume cha maamuzi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano waTanzania inayo zuia ugawaji mpya wa vitalu hadi sera ya gesi asilia na sheria ya gesi vikamilike.
"Haraka hii ya serikali kugawa vitalu bilasera wala sheria inatoka wapi? Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho zasemina hii na kuhalalisha maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya taifa kwa vizazi vya sasa na vijavyo," alisisitiza Zitto.
Zitto amewataka wabunge na wananchi kuupingauamuzi huo wa serikali.
"Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanzakuwepo kwa sera na sheria mpya unapaswa kupingwa kwa nguvu zote. Tafuta mbungewako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali. Tumalize kwanza sera nasheria ndiyo tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi," imesisitiza taarifahiyo.
Naye Mnyika amesema kuwa si sahihi kwa serikali kuanza kutoa leseni mpya zautafutaji na ugunduzi wa gesi nchini wakati taifa likiwa bado linaendelea namchakato wa katiba mpya.
"Taifa letu lipo kwenye mchakato wa kuandika katiba mpya huku kukiwa na kumbukumbu chungu za miaka zaidi ya 20 ya kupata hasara kubwa baada ya kufungua mianya ya ufisadi na unyonywaji katika sekta ya uchimbaji madini na rasilimali zingine muhimu," ilisema taarifa yake kwa vyombovya habari.
Taarifa hiyo inapendekeza kuwa ingekuwa vemakwa serikali kusubiri kwanza kukamilika kwa mchakato wa kupata katiba mpya ilikuhakikisha kuwa udhaifu wa kikatiba, kisera, kisheria, kiuongozi na kitaasisiumerekebishwa.
"Hivyo, badala ya kukimbilia kutangazamzunguko mwingine huku tayari taifa likiwa kwenye lindi la ufisadi na unyonyaji kupitia mikataba iliyotangulia ya gesi asili; nguvu za wananchi zielekezwe katika kutaka katiba mpya kuwa na vifungu vitakavyolinda rasilimali muhimu kamamafuta, gesi madini na mali asili nyingine," imesisitiza taarifa hiyo.
Hivikaribuni Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)imetoa taarifa ya kuzinduliwa kwa mzunguko wa nne wa utoaji leseni za utafitina ugunduzi wa gesi asilia nchini.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na baadhi ya vyombo vya habari, na tovuti ya TPDCni kwamba utoaji leseni za utafiti na uzinduzi huo utaanza mwezi Oktoba, mwakahuu.
Kwamujibu wa taarifa hiyo, leseni zitakazotolewa zitahusisha utafiti katika Ziwa Tanganyika lililopo magharibi mwa Tanzania, na ndani ya kina kirefu cha maji ya Bahari ya Hindi kwa upande wa mashariki na kusini mwa bahari hiyo.
Itakumbukwa kwamba hapo awali wizarailitangaza kutokuingia mikataba yoyote ya utafiti na uvumbuzi wa gesi asiliahadi pale sera ya mafuta na gesi itakapokuwa tayari.
Msimamo wa CHADEMA kuhusu sekta ya mafuta nagesi uko wazi ambapo inataka kwanza kuandaliwa kwa sera na sheria ya mafuta nagesi kabla ya kuingia mikataba mipya ya utafutaji na ugunduzi wa nishati hizo.
Baadhi ya wabunge wamelidokeza Tanzania Daima kuwa kutohudhuria semina hiyo ni kujikosesha fursa ya kujua kitakacho wasilishwana serikali.
Walibainisha kuwa wasipohudhuria semina hiyohawatakuwa na uwanja mpana wa kupinga kile wanachokiona si sawa.
Waziri Muhongo anena
Waziri wa Nishati na Madini, ProfesaSospeter Muhongo alisema Tanzania inatumia sheria ya gesi asilia na mafuta ya mwaka 1980.
"Watu waache kupotosha..., si kweli kuwapo maamuzi ya Bunge ya kutogawa vitalu vipya vya utafutaji wa gesi asilia namafuta bali kinachofanyika ni kuiboresha sera na sheria ya gesi asilia ilikuitengenisha na mafuta," alisema.
Alisema kuwa utafutaji huo haukuanza leo nakwamba anayegundua ndiye anatafuta sana.
Profesa alifafanua kuwa kwa sasa wanafanya maboresho ya kulijenga upya Shirika la Mafuta (TPDC) lililoanzishwa mwaka 1969.
"Hawa Watanzania wanaotoa taarifa za uongokwenye mitandano na kutaka kupotosha watu, wanaikosesha nchi maendeleo. Maanahayo makampuni ya mafuta wanayoyapiga vita ndiyo hayo yanatafuta mafutaMsumbiji na Kenya, kwanini sisi tukatae?" alihoji.
Alisema kuwa kamanchi isingekuwa na sera ya gesi na mafuta hata hao wawekezaji wasingekubali kuwekeza kwenye nchi ambayo haina sheria.
WaziriMuhongo alisema kuwa leo watafanya semina kwa wabunge wote mjini hapa kuhususera hiyo ya gesi, na hivyo kuwataka wote wenye dukuduku walete hoja zao wapate ufafanuzi.
Tanzaniadaima