Thubutu. Unadhani Zitto hataki ugali. Yaani Zitto mwenyewe asiseme mtu mwingine aje amsemee?
Nadhani mleta mada, humjui vizuri Zitto.
Hapa chini ni baadhi ya kauli tata za Zitto
1/Sina mpango wa kugombea tena Ubunge 2015
2/ACT siijui ni ya nani na sihusiki na uanzishwaji wake.
3/Sina mpango wa kuondoka CHADEMA na nitakuwa wa mwisho kuhama CHADEMA.
4/Mwaka 2015 nimejipanga kugombea urais na sio ubunge tena.
5/Mara baada ya kuacha ubunge 2015 nitaachana na siasa, nitakwenda chuo kikuu kufundisha.
6/Sina mpango wa kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya ACT.
7/Sijui chochote kuhusu mpango wa siri wa kina Kitila Mkumba na Samson Mwigamba kuhusu mapinduzi ya kisiasa ya uongozi wa CHADEMA ili mimi niwe mwenyekiti.
8/Mimi ni mjamaa ninayeamini na kuishi sawa sawa na falsafa za mwalimu Nyerere za Kijamaa.
9/UKAWA ni wasaka tonge tu, sina muda wa kushirikiana nao.
10/Sakata la ESCROW ni mimi niliyeliibua, kulisimamia mpaka likafanikiwa kuwaangusha mawaziri bungeni, pasipo mimi kusingetokea kitu.