Zitto katika gazeti la Denmark

Sina mengi ya kusema ila Zitto ninayemjua mimi ni mtu safi hawezi kuivuruga CDM labda chama kimvuruge. Mara nyingi sana kazi ya mtu inaposhine kuliko ya viongozi wake, matokeo huwa mabaya. Mtu asikudanganye pamoja na kuwa wapinzani watu bado hawaachi kutazama maslahi binafsi. 'no charity work' sasa mtu anapoonekana kuwa threat kwenye maslahi ya mtu mwingine hasa kiongozi wake, ndipo tatizo hutokea 'anatuvuruga', 'mjuaji' n.k. Imani yangu ni kuwa ili tuendelee, lazima tuongozwe na manabii watu ambao watajitoa kwa dhati kinyume na hapo, ni lazima watanzania wawe wakali kuliko pilipili na kuweka kando upole tulionao sasa. Falsafa yangu ni tofauti kidogo na watu wengine. Inasema ni vigumu kwa mwanasiasa kuleta maendeleo, ni rahisi zaidi wananchi kujiletea maendeleo yao wenyewe kwa kujisimamia, kutambua haja ya kuendelea, kusimamia maendeleo yao wenyewe na kutambua na kuzisimamia rasilimali zao zitakazoweza kuwaletea maendeleo. Kinyume na hapo tutabaki kunyoosheana vidole. Tazama mataifa yaliyoendelea, rasimali zimerudishwa kwa wananchi waamue wenyewe maendeleo yao, mfano mzuri ni Botswana na Rwanda hatuwezi tena kuwakuta..! Wananchi wanawezeshwa ili wawezekutoa vipaombele vya maendeleo yao! Hatujui baadhi ya mahitaji ya watu unaweza kufikiri wanahitaji sana barabara kumbe shida yao kubwa maji..! Siamini sana kwenye siasa ingawa pia siasa nimuhimu kwenye jamii.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom