BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 654
- 1,598
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani humo kuepuka kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani, akisisitiza kuwa hali ya usalama katika mkoa huo ni shwari.
Zitto ametoa wito huo leo Oktoba 28 wakati wa hafla ya kufunga kampeni zake, akieleza kuwa ni muhimu Jeshi la Polisi kutojihusisha na matumizi ya nguvu kupita kiasi ili kuepusha hofu na vurugu miongoni mwa wananchi.
“Hali ya usalama Kigoma ni ya utulivu mkubwa, hivyo si vyema kutumia nguvu zisizo za lazima. Amani tuliyonayo ndiyo msingi wa maendeleo yetu,” amesema Zitto.
======