Zitto Kabwe: Nyerere wangu mimi!

nadhani MBOWE ndiye anastahili kufananishwa na nyerere. watu kama nyie ni aibu kwa taifa hili.
ZZK ni mwanasiasa wa kupigiwa mfano wa nyerere kuliko mwanasiasa yeyote aliye hai hapa tanzania. unalijua hilo, bavicha wanalijua, mbowe analijua, mimi na wengine woote tunajua.
ila tunatofautiana kwa sababu nyie wengine ni walamba vinyesi vya wafalme.
huwezi kujua hili... lakini hata nyerere alikuwa natuhumiwa kuwa anamiliki mabilioni huko USWIS na tulikuja kuamini kuwa haikuwa kweli baada ya kustaafu na kurudi kuishi maisha ya kawaida kabisa. kwa mwanasiasa tuhuma ni kitu cha kawaida kabisa hasa ukiwa mwanasiasa mwenye upeo na tishio kwa wenzako kisisasa kama alivyo ZZK.
zzk ni nembo na ni tishio kwa mafisadi na vibaraka
hapendwi na yeyote kati ya wale wenye malengo mabaya
ila muda ukifika mtatambua ujinga wenu na wooote mtamsujudu
 
Siasa ya Tanzania imesheheni mashabiki wa siasa na siyo wanasiasa, wao wanashabikia watu badala ya kusimamia itikadi ya vyama vyao. Nani asiyefaham kwamba Zitto ndiye chachu ya mabadiliko ndani ya bunge kwa kuonyesha msimamo thabiti wakati wa buzwagi scandel? Baada yake ndipo wengine nao wakafuata njia. Hata sakata la tokomeza pressure ya huyu kijana iliinfluence maamuzi so mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!
 
asante ndugu zzk kwa historia nzuri iliyo shehen sifa kwa sera ya ujamaa. pa1 sana mkuu
 
zitto nikiongozi anayejua shida za watz
huyu ndo anayefa kuwa raisi wa nchi
 
Sasa wewe ukisoma hio post ya Zitto, imemwongelea zaidi Nyerere au Zitto.
Usijibu haraka tulia kwanza.
We jifanye kuelewa sana tu lakini ukweli utabaki palepale kwamba Zitto anamwongelea Mwalimu thru first hand experience!msingi wa hoja yake hapa ni maisha Enzi za mwalimu na ametumia historia yake kujengea hoja .
watu weledi walitakiwa wajikite katika kchambua maisha ya wakati ule dhidi ya sasa si kuchambua Zito yule dhidi yaZitto wa sasa
 
Kuna shule hapo kigoma,Dawati moja wanafunzi 15. Ni aibu mpaka leo hatuna madawati, siasa bado wanapiga poroji tunamuenzi mwalimu!!!!Huu ni ujinga.
 
Kuna shule hapo kigoma,Dawati moja wanafunzi 15. Ni aibu mpaka leo hatuna madawati, wanasiasa bado wanapiga poroji tunamuenzi mwalimu!!!!Huu ni ujinga.
 

Mkuu umenifurahisha...!! mie stori yanngu ingejuwa kali kweli!! Maana kulala njaa siku tatu ilikuwa kawaida sana tena nikiwa darasa la saba!! na nilifaulu!! lkn ya nini hayo ..... Nyerere alikuwa mtoto wa chifu hata kwenda shule alipendelewa kwa sababu ya kuwa mtoto wa chifu!!...lkn hakuwahi kusema vitu wanavyosema hawa vilaza!!!....
 

Mamna kitu .ukikua utaacha utoto tu
 
Kuna mahali kagusia kantalamba hebu wanaoifaham hyo shule waseme kidogo

Ipo Sumbawanga Mjini, ni shule upande chuo cha ualimu TTC, miaka ya 70s ilikuwa ni seminari ya kanisa katoriki, walipita watu wengi hapo mashughuli, akiwepo Mizengo Pinda na wakina Pengo. Sasa inamilikiwa na serikali ni boarding kwa ajiri ya Boys tangu mwaka 2005, mwanzo ilikuwa mchanganyiko wake kwa waume. Ni Moja kati ya shule mashughuli zilizotaifishwa na serikali mkoani Rukwa kutoka kwa RC. Ina sifa y akukusanya wanafunzi wengi kutoka pembe mbalimbali za nchi hii. Kipindi furani ilijaza wakimbizi watusi kwa wahutu(Zzk), wengi wakitokea Mishamo na Katumba (Mpanda sasa Katavi) lakini pia wanakigoma wengi wamesoma hapo ni mashughuri sana. Ukitaka asili ya jina niulize tena asante.
 

Nivizuri kama pia ungenijuza na jina lake lina maana gani.
 
Nivizuri kama pia ungenijuza na jina lake lina maana gani.
Kantalamba ilimekuwa modified tu, matamshi halisi ni katalambwa au pantalambwa("ka" from red, inasimama kuonyesha udogo, " Pa" from red inasimama kuonesha pahala, au mahali). Sasa maana yake ni kwamba maeneo hayo kulichimbwa shimo kama handaki ambamo Majemedari wa jeshi la kifipa walijificha hapo, sasa juu ya hilo shimo lilokwenda eneo kubwa(extended in term of canal like structure) kuliwekwa mfuniko dhaifu( miti midhaifu na kufukiwa udongo). Lengo ilikuwa ni kumshinda adui kirahisi ambao ni Wangoni, maana mfipa na Mgoni wamepigana vita sana , ikiwa kupinga uvamizi wa Mngoni kwenye nchi ya Ufipa. Ikumbukwe kuwa Ngoni Migration ikuwa na njia kuu tatu, Moja ilitua Mngongoma( Songea leo chini ya kiongozi Mbonani na badae Chief Songea nk), Njia ya Pili(route) ilikuwa kuelekea Sumbawanga(Fipa land) chini ya Zwangendaba(Kafa na kuzikwa Mwaka 1845 Matai-Rukwa) ambaye alikuwa adui mlengwa hapa, Njia ya tatu ilikuwa na Mputa Maseko aliyeenda Uhololo-Kati mwa Tanzani. Lengo la huo mfereji ni kwamba adui akikanyaga anatumbukia hivyo mkiwa ndani akiwa amepagawa na ajari then mnaanza kumshambua. Mwisho mngoni alishinda na kilichowaponza wafipa ni ukarimu baada ya kusema tuwakubari adui tuishi nao, wakiwa hawajajiandaa wakashambuliwa. KANTALAMBA SHORTLY MEANS PASIPOVUKIKA NA MALENGO YA HAPO HAYAKUBADILIKA KWANI MKOLONI HASA MJERUMANI ALIDUNDWA HAPO VIZURI SANA KWANI PALITUMIKA PIA KUPINGA UKOLONI. Ajabu serikaLi imeruhusu kujengwa mji pahali hapa mwaka 2000's nakupoteza historia nzima, shimo juzi limefukiwa na mabepari wamejenga mahekalu yao. God Bless RUKWA
 
tabia hii iliendelea mpaka miaka ya 1990's.....sidhani kama sasa ipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…