Zitto Kabwe: Nidhamu ya kazi inahitajika kutekeleza dira 2050

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Leo imezinduliwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Shabaha ya Dira ni kuwa na Pato la Taifa la USD 1 trillion ambapo pato la mtu mmoja liwe wastani wa USD 7,000 kwa mwaka kutoka USD 1,200 za sasa.

Hii maana yake ni kuwa Uchumi wetu (GDP) unapaswa kukua mara 13. Inawezekana, lakini katika Taifa lililo na mshikamano, lisilo na ubaguzi na lenye demokrasia. Msingi wa hayo ni HAKI. Kazi kubwa inapaswa kufanywa kwa NIDHAMU ya hali ya juu sana kufikia shabaha hiyo. Taifa lenye jamii ya uchawa uchawa haiwezi kuwa na nidhamu ya kufikia malengo tajwa. Nidhamu ya kazi inahitajika kwa kila sekta

KILIMO: Kasi ya ukuaji wa Uchumi itapaswa kuongozwa na sekta ya Kilimo, kikue kwa kasi ya 8-10% kwa mwaka. Tunapaswa kuweka nguvu kubwa katika TIJA kwenye Kilimo, angalau tuongeze mavuno mara mbili (doubling) ya sasa katika kila Ekari ya mazao ya Kilimo.

Soma Pia: Rais Samia azindua Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Dodoma Julai 17, 2025

Nina mfano napenda kuutoa, wa zao la Pamba, ambapo ilhali mkulima wa Tanzania anapata kilo 250 - 300 kwa kila ekari ya Pamba, mkulima wa Benin anapata kilo 800 na mkulima wa Burkinafaso anapata kilo 1500. Hali ni mbaya zaidi kwenye Mahindi na Mpunga ambapo wakulima wetu wanapata gunia chache zaidi kutoka kila ekari 1!

VIWANDA NA MADINI: Ni lazima tuongeze ajira kwa kuhakikisha mnyororo wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi unafungamanishwa na sekta yetu ya kilimo. Ni lazima kuongeza tija ya mazao yetu ili yasiuzwe yakiwa ghafi. Zamani niliwahi kuandika ningeanza na nini kati ya Reli ya SGR na Mgodi wetu wa Mchuchuma na Liganga.

Ni jambo zuri tumejenga Reli ya SGR, lakini zaidi ya 75% ya fedha zilizotumika kwenye ujenzi huo zimekwenda nje ya nchi (Japan na Uturuki) kununua chuma na mataruma, ilhali chuma tunacho mchuchuma na Liganga Njombe na Ruvuma, mabehewa ya SGR yamekuja, lakini makochi na viti havijatengenezwa na mkonge wa Tanga wala Pamba ya Simiyu, ama ngozi ya mifugo yetu, tumeendelea kuuza ngozi ghafi, katani ghafi na pamba ghafi. "- Zitto Kabwe, Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo.
 
Hongera Zitto wa ACT kwa kujadlili hoja na kutoa mapendekezo. Kule CHADEMA wanajadili kwanini Mbowe kahudhuria uzinduzi wa dira ya Taifa 2050.!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom