AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 220
- 689
Nimekaa nimetafakari sana kitendo cha Professa Kitila Mkumbo kuamua kujiuzulu uanachama na uongozi katika chama cha ACT-Wazalendo.
Ameelezea sababu iliyomfanya ajiuzulu ni mgongano wa kimaslahi uliopo baina yake yeye aliyepo Serikalini na chama chake, inamuwia vigumu pale anapowaelezea kuhusu mafanikio ya Serikali ,na mipango yake jinsi inavyotekelezwa.
Kwa lugha fupi ni kwamba Zitto Kabwe na ACT-Wazalendo yake hawafurahishwi na kasi na juhudi za Serikali ya awamu ya 5 katika kutatua kero mbali mbali za wananchi hususani kero kubwa ya maji, ambapo Prof.Kitila ndiye aliyepewa dhamana ya kuwa mtendaji mkuu wa
sekta ya maji akihudumu kama Katibu Mkuu wa Wizara ya maji,anayekesha na kuzunguka Tanzania nzima kuhakikisha maji yanapatikana kwa raia wote wa Tanzania.
Walikuwa wanamkwamisha katika kutekeleza kwa ufanisi majukumu yake ya kumsaidia Mh. Rais katika kuleta huduma ya maji safi na salama kwa watanzania wote.
Kiukweli nampongeza Prof Kitila kwa uamuzi wake huu wa kishujaa wa kuamua kuwatumikia watanzania na kuachana na minyororo ya siasa uchwara za wapinzani wanaotaka watanzania waendelee kuumia huku wao wakitumia shida za wananchi kama mitaji yao ya kisiasa.
Yaani Zitto Kabwe haoni mafanikio ya Serikali ya awamu ya 5 pamoja na kwamba miaka ni miezi 3 tu imepita tokea Mh.Rais Magufuli azindue mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Tanganyika pale Kigoma mjini .
Tunaposema wapinzani hawapendi nchi hii ipige hatua ya maendeleo, huu ndio mfano halisi ,kutoka kwa Zitto Kabwe aliyeziita Bombadier zetu "Bajaji" lakini "bajaji" hizohizo alizozinanga leo hii zimeweza kumuwezesha yule Muha mfanyabiashara wa dagaa kutoka Kigoma kufanya biashara kwa urahisi kabisa tofauti na hapo awali.
Tuwe makini na watu wanaosema wako na sisi pamoja lakini tukigeuka nyuma hatuwaoni.
Augustino Chiwinga.