Zitto Kabwe kuzindua kampeni za CHADEMA Mwanza.

Zitto Kabwe kuzindua kampeni za CHADEMA Mwanza.

Idimulwa

Platinum Member
Joined
May 27, 2011
Posts
5,110
Reaction score
2,698
Ni kwenye kinyang'anyiro cha udiwani kata ya Kirumba jijini Mwanza.Ni keshokutwa siku ya Jumapili.

Karibuni.
 
komaeni maana mil 60 zilizoandaliwa tunaomba zipotee bure na pia namtabiria aliyezitoa kufilisika baada ya ubunge wake.Kaingia kichwa kichwa na huenda kwa sababu shule ili DONT
 
Tunawaombea heri wakuu,mfanikiwe sana na tunyakue hicho kiti..Mungu awe nanyi.
 
Hiyo ni ngome ya CDM ushindi ni lazima!
 
zitto kuzindua kampeni za udiwani ni kujishushia heshima yake

Viongozi makini na wenye busara siku zote hujishusha, na jamii yenyewe ndiyo huwanyanyua juu. Hiyo ndio tofauti kubwa iliyopo kati ya viongozi wetu na wenu.

Kanyaga twende kamanda zitto, ccm wameshajaa mchecheto kwakuwa wanaujua moto wako.
 
This is what I wanted.....wewe unayesema anajishusha acha iwe hivo, sisi tunataka ushindi na tumeshauri kata nyingine kama Vijibweni (Dar), Msambani (Tanga), Chang'ombe (Dodoma), Kiwira (Rungwe), Msambani (Tanga), Lizibuni (Songea), Kiwanga (Bagamoyo), na Ligangambili (Bariadi) waende watu wazito...usije shangaa kusikia Lema, Mdee, Mnyika, Mbassa, Msigwa, Heche, na wengine wengi wako maeneo hayo...

Kirumba ni yetu sisi CHADEMA, Zitto atasaidiwa na Wenjeh na Highness,,,upo hapo,,yaani ni full majeshi,,,
 
Ni kwenye kinyang'anyiro cha udiwani kata ya Kirumba jijini Mwanza.Ni keshokutwa siku ya Jumapili.

Karibuni.
Ng'wana Sweke mimi sina wasiwasi kabisa na ushindi wa CDM hapo Kirumba naijua Kirumba nawajua watu wake nimekulia hapo, nawatakia ushindi mnono.
 
zitto kuzindua kampeni za udiwani ni kujishushia heshima yake

niko pamoja nawe mkuu, hivi kweli ndani ya cdm hakuna viongozi wengine wa kusimamia kampeni za udiwani mpaka aende kiongozi mkubwa kama zitto? Siamini hasa kwa chama makini kama cdm.
 
Udiwani ni uwakilishi wa Wananchi,sasa iweje useme Zito Kajishusha!!Mbona Mkapa Anakwenda Arumeru,Na Igunga alikwenda,Kwa nini hukusema Kajishusha,Changia mada Kwakufikiria Bwana usilete mawazo yako finyu hapa,nyie ndo Makada wa CCM msio fikiria!!

Majembe yetu jitaidini kata ya Kirumba ni yetu!!CDM Hatuachi Kitu!!
 
komaeni maana mil 60 zilizoandaliwa tunaomba zipotee bure na pia namtabiria aliyezitoa kufilisika baada ya ubunge wake.Kaingia kichwa kichwa na huenda kwa sababu shule ili DONT

hivi mtu anayewekeza milion sitini simply kwa ajili ya udiwani tu atazi recover vipi?? na ana interest gani na huo udiwani? na anahakikishaje atashinda maana kura ni some sort og gambling??
 
hivi mtu anayewekeza milion sitini simply kwa ajili ya udiwani tu atazi recover vipi?? na ana interest gani na huo udiwani? na anahakikishaje atashinda maana kura ni some sort og gambling??
Huyo atakuwa mwizi tu, na anauhakika zitarudi akishinda hata wananchi wakila mapanki ilimradi pesa yake inarudi. Na ndiyo aina ya viongozi wetu wengi walivyo kwa sasa!! Wako radhi kupiga magoti ili uwape kura lakini wakishapata kura, watakutimulia vumbi, watakumwagia tope na kukuita jina lolote baya!!
 
Back
Top Bottom