Zitto aache kuizungumza Chadema! Yeye apambane na kazi aliyopewa na ccm kupitia chama chake mamluki na kamwe hataiweza Chadema. Mbona hatujawahi kumsikia Mbowe akimzungumza huyo kibaraka Zitto? Viva kamanda Mbowe,songa mbele tulikomboe Taifa letu kutoka kwa mkoloni mweusi.Kiongozi Mkuu wa ACT WAZALENDO, Zitto Kabwe, katika maelezo yake amedai kwamba walifikia Makubaliano na Mbowe ili yeye achukue uenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe, Amezungumza mengi , lakini hakusema yote, wala hakusema kwanini alikuwa anaongozana na Kikwete kwenye ziara za Nje ya Nchi huku akiwa kiongozi wa Upinzani, Zitto alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Bado Zitto hajawahi kusema hadharani namna Kikwete alivyokuwa anamfadhili ili kuua Chadema (Haya tutayasema baadaye).
Bali hoja yetu ya leo ni hii, Atuonyeshe kifungu cha Katiba ya Chadema kinachoelekeza hayo aliyoyasema, vinginevyo hiyo itakuwa porojo kama ile ya Lowassa kwamba alikubaliana na Kikwete kuachiana Urais , huku akijua utaratibu wa Chama chao hauko hivyo.
Kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania, vyama vya siasa ni mali ya Wanachama, ndio maana Leo Lwekamwa alifukuzwa TLP hata kama alikuwa mwanzilishi.