ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,265
- 4,452
Habarini:
Kwanza niombe radhi kwa kichwa cha mada,Pili niweke wazi kabisa kwamba binafsi namuheshimu sana Mh.Zitto na kwamba andiko hili kwa namna yoyote halina maana ya kumdescredit bali natumaini kama atalisoma basi atalifanyia kazi kwa kadiri aonavyo inafaa.
Nimeona nimwambie kabla mwaka haujaisha kabisa ili ajue.
Kwanza kabisa nieleze kwa ufupi ninachomaanisha,Katika ulimwengu wa siasa tunapozungumzia mtu mwenye nguvu ya kuunganisha watu basi tunazungumzi mtu ambaye ana haiba,hamasa na mvuto wa kipekee na hivyo ana uwezo wa kuwaleta karibu watu tofauti na kuwaweka pamoja.Hili silioni kwa Ndugu Zitto.
Sitaki kujadili watu au matukio yanayomhusu Zitto Kabwe ila nateka niweke misingi ya kufuata ili uweze kuwa uniting figure ni ipi.
Wasalaam
PBK

- Kwa mwana siasa anayetaka kukua,Zitto Kabwe hana sababu ya kuchukua credit kwa kila jambo,anapaswa kujifunza ama kuacha wengine wachukue credit na kukua ama basi wachukue collective credit.
- Ni vizuri kwa mwanasiasa kuwa na personal opinions na kuexpress opinions hizo.Lakini kama unataka kuwa uniting figure basi some opinions inabidi uziweke moyoni.Kuna mambo ambayo ni vivid kila mtu anayaona na kama mwanasiasa uliyekomaa huna haja ya kuyatolea opinion isipokuwa tu kama yana direct impact kwenye maslahi yako ya kisiasa
- Ili uweze kuwa uniting figure unapaswa ujifunze kuchagua marafiki na sio marafiki wakuchague.Hauna haja ya kuwa attention seeker,wakati mwingine kwepa kushiriki katika baadhi ya matukio hasa kama hayana maslahi katika safari yako ya kisiasa.
- Ni vizuri mwanasiasa ukasoma upepo kabla ya kulisemea jambo,kulisemea jambo wa kwanza haikufanyi uonekana mwerevu kwani katika safari ya siasa the slow and steady wins the race.
- Kwa kuwa nimesikia tetesi kuwa Zitto Kabwe ana hamu sana ya kugombea Urais.Nitoe tu ushauri kwake aachane na hiyo ajenda kwa sasa.Anachopaswa kufanya kwa sasa ni kuandaa watu watakoweza kugombea nafasi hizo.Yeye kugombea urais basi asubiri akifikisha 50 yrs ila before then ajenge chama kwanza
- Chama Chake kinayumba na yeye anajua sababu kubwa ni yeye,Pamoja na kujaribu kuuaminisha umma kwamba ACT iko imara lakini kitendo cha Mwenyekiti wa Chama ambaye pia alikuwa mgombea wa chama na mwanzilishi wa chama kutoka katika chama katika mazingira ya kutatanisha basi ni dhairi kuwa Zitto Kabwe hajaweza kuwapa watu Tumaini la mabadiliko wanayotaka
Wasalaam
PBK