Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,331
- 33,141
Swali zuro sanakwa upande wa faida ametuingizia shilingi ngapi?
Zitto sasa hivi ni kama debe tupu linalotika vibaya!
Mbunge wa Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa Rais John Pombe Magufuli ameliingizia taifa hasara ya bilioni 36 mpaka sasa toka alipochaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook aliandika kuwa kitendo cha Rais Magufuli kushindwa kuchukua hatua juu ya malipo ya IPTL ambayo yanalipwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kila mwezi yamepelekea sasa hivi kufikia jumla ya bilioni 36.
"Tshs bilioni 8 kila mwezi TANESCO bado wanalipa IPTL. Rais haijampendeza kumaliza ufisadi huu. IPTL nadhani ni Jipu la Mgongoni (kwa kutumia maneno ya Hidaya wa Richard Mabala ). Rais, kwa kutochukua kwake hatua, ameshaliingizia taifa hasara ya tshs 36 bilioni toka aingie madarakani" aliandika Zitto Kabwe.
Wakati Rais John Magufuli anatimiza siku 100 toka kutangazwa kama Rais Zitto Kabwe alitoa tathimini yake na kugusia sakata la Escrow pamoja na kampuni ya IPTL na kusema kuwa pesa ambazo wamelipwa IPTL/PAP kwa siku 100 tu zingeweza kununua CT Scan kwa hospitali zote za mikoa nchini.
"Mkataba wa IPTL bado unaendelea kunyonya Nchi na Serikali inatazama tshs 8 bilioni zinalipwa Kwa matapeli wa IPTL na PAP kila mwezi.
"Katika siku 100 tangu Rais Magufuli aingie madarakani, jumla ya tshs 30 bilioni zimeshalipwa Kwa IPTL/PAP ambazo zingeweza kununua CT scan Kwa hospitali zote za mikoa nchini.
"Fedha hii ni zaidi ya mkopo ambao Serikali imechukua kutoka Benki ya Dunia ili kujenga ' fly over ' ya Ubungo jijini Dar Es Salaam" Alisema Zitto Kabwe.
Chanzo; Sky One blog
Wewe unamsikiliza zitto mtu anayefanya siasa zake kwa maelekezo ya mganga wa jadi naye wakumsikiliza sasa.
Wakati mwingine tujikite kwenye hoja mkuu kama hamna la kuchangia unakaa kimywa, mbona Mwanakijiji hapo juu kachangia vizuri tu bila mhemukoZitto huyu hana madhara na wala hana faida yeye kuongea tu ata kama hatakiwi kuongea.
Aonyeshe umahiri wa kuongoza kwa kutenda sio kwa jambo hili ndio uombe huruma ya ushauri wetu!!!! Ameteua mpaka asiopaswa kuteua, hapo husemi aombe tumkumbushe jinsi ya kufanya, mbona amezuia shughuli za kisiasa bila kuambiwa wala kushauriwa na mtu yeyote, iweje hapa ndio unasema tumshauri "jinsi ya kufomuleti" (makinda style)Si Bunge lipo; wabadili Sheria au wachukue maamuzi ya kushughulikia matatizo yaliyoko kwenye Executive Branch. Ndio maana ya demokrasia. Na pia kama kuna kitu kinafanyika kinyume cha sheria kuna mahakama. Kumlaumu Magufuli kwa kitu ambacho hawezi kukitolea executive decision tu italeta mengine. Rais anaweza kutumia madaraka yake lakini fikiria hayo maneno mengine yatakayokuja.
Binafsi ningependa kusikia pendekezo la Rais anatakiwa kufanya nini na vipi kuzuia malipo haya. Inawezekana ikamsaidia Rais.
Kumekucha hizo pesa ndogo tunataka za Mbowe 1.2 billion.Hii ndio Tanzania.Jamani hesabu zimekosewa mbona hasara ni ndogo kila mwezi ni 8 bilion na miezi toka achaguliwe ni miezi 20 sasa 8 billio ×10 ni bilion 80 mbona mwasema 36 ni hesabu za vipi hizo
Hasara ni 80 bilion hadi sasa
ndugu jifunze kujadili hoja iliyoletwa mezani na zito kama ni ya kweli au sio ya kweli kwa kuleta hoja zako na sio kuleta vijembe ambaavyo havita wasaidia watanzania, acha ushabiki lete hoja au facts tuzitafakaliZitto sasa hivi ni kama debe tupu linalotika vibaya!