Zitto Kabwe amnadi Jamal Malinzi Urais TFF

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, amesema atafanya kila aliwezalo kuhakikisha mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, anashinda nafasi hiyo.

Uchaguzi Mkuu wa TFF unatarajiwa kufanyika Oktoba 27, ukitanguliwa na ule wa Bodi ya Ligi (TPL-Board), Oktoba 25.
Kabwe, mbunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliandika jana katika ukurasa wake wa kijamii (Twiter), kuwa, yeye ni mdau mkubwa wa michezo hususan soka hapa nchini, hivyo atahakikisha Malinzi anakalia kiti hicho.

Aidha, Kabwe alisema kutokana na hilo atahakikisha kwa gharama yoyote Malinzi anachukua kiti cha Rais anayemaliza muda wake, Leodegar Tenga.

Katika hatua nyingine, Malinzi ameahidi, endapo atafanikiwa kuwa Rais wa Shirikisho hilo, atafanya mambo makubwa ya kuinua soka ya Tanzania ambayo inashuka kila siku katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa kujikita katika soka ya vijana, ambao ni hazina ya baadaye.

Source:Tanzania Daima
 
Atahakikishaje? Atapiga kura zaidi ya mara moja? Bora waseme tu anampigia debe sio atahakikisha.
 
Zitto bana!!!Ya huku kwenye PAC na Ruzuku za Vyama vya Siasa hajamaliza mara kaibukia huku kwenye Michezo.Malinzi akimuamini Zitto atajuta,Atuulize sisi kilichotupata na Sakata la Ruzuku,Mshahara wa Pinda pamoja na mshahara wa Kikwete....Ametuacha kwenye mataa wakati bado tukisubiri maelezo ya kina zaidi kutoka kwake kuhusu hayo MASAKATA...Kabwe mtu!!!!???
 
Hivi Tanzania hakuna watu wengine wanaoweza kuongoza TFF? Miaka nenda rudi majina yamekuwa ni yale yale na bado tuko kama kichwa cha mwendawazimu.

Kwa mtazamo wangu, mfumo wa kuwapata viongozi wote wa juu wa TFF unabidi ubadilike- waombaji wafanyie mchujo na professional organisations kama PWC au Delloitte. Huu mtindo wa sasa ni bure kabisa.
 
mambo ya Ngoswe......sitak kuamini kuna ka ajenda ka udini hapo. ...!
 
Kama ni urais wa TFF hata January Makamba unamfaa sana.
 

Mkuu pale TFF ni kisiwa cha kupiga mpunga na sina uhakika kama wanafanyiwa proper auditing hao jamaa. Mechi za Yanga na Simba zinawaingizia mpunga mrefu sana kiasi kwamba imefika hatua wameweka ukuta kwamba huwezi kuwania uongozi pale bila kuwa na uzoefu wa angalau miaka mitano katika klabu au ngazi ya uongozi katika wilaya au mkoa.

Kwa kufanya hivyo wanajaribu kuzuia damu mpya kutoka nje ambazo bila shaka zitakuwa na changamoto mpya na kwakweli naamini kwamba watu wenye clear vision na maendeleo ya soka letu watatoka nje ya kakikundi kalioko sasahivi lakini kwa kanuni hizi za kuwazuia watu wengine kwa kuwaita si wanfamilia wa TFF ni dhahiri kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanya kupata watu wapya watakaoweza kuliinua soka letu.

Lakini kwa sasa hata mimi namuunga mkono Jamal Malinzi kuwa raisi wa TFF kwakuwa angalau aliwahi kuwa kiongozi wa Yanga na alipokuwa promoter wa ngumi hapa Tanzania tuliona vijana wa kitanzania hasa ukoo wa Matumla ulivyoshamiri katika ngumi za kulipwa.

Kwa upande wangu Nyamlani ana uzoefu wa kuwepo TFF tangua akiwa TEFA na baadae DRFA lakini hakuna jambo lolote la mafanikio ama maendeleo analoweza kutuonyesha kwamba amewahi kulifanyia soka la nchio hii.
 
Last edited by a moderator:
Mbona Jamal Malinzi ni Yanga na Zitto Kabwe ni Simba?!

Nijuavyo mimi Bongo UTANI WA JADI ni VISASI na CHUKI. Yanga hawezi kumuunga mkono Simba and the vice versa!

BTW, hivi wagombea Urais wa TFF ni akina nani? Labda Malinzi ndiye ana afadhali kati ya wagombeaji wote. Just thinking aloud.
 
Kwa gharama yeyote? Kila awezalo? Brother zitto come on! Au unataka ba.mkwe akuombee msamaha kwa diva ili muwe kama zamani!
 
hapo udini na ukabila kazini

Ukabila gani hapa? ZK ni Muha, JM sijui kabila lake, ni Mhaya I Presume. Wagombea wote wa urais ni Waislam na ZK ni Muislam pia, ni yupi ambaye angemsapoti usiseme udini? Itikadi ya ZK ni Simba na JM ni Yanga, sasa tatizo liko wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…