Zitto Kabwe alishukia baraza la mawaziri

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,121
Zitto alishukia Baraza Mawaziri
www.ippmedia.com/sw/habari/zitto-alishukia-baraza-mawaziri

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo huyo ‘aligueka mbogo’ dhidi ya baraza hilo bungeni mjini hapa juzi jioni, alipokuwa akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka ujao wa fedha.

Aliishauri wizara hiyo iangalie upya miradi ya ndani itakayowanufaisha wananchi na kuangalia fungamanisho la kusaidia kuchochea kukaza uchumi.
Zitto pia aliishauri wizara hiyo kushughulikia miradi inayotengeza ajira za ndani ambayo anaamini zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda.

"Hivi Mheshimiwa (Charles) Mwijage mnapokaa katika ‘Cabinet’ (Baraza la Mawaziri), mnajadili hii mipango. Kwa sababu mkikaa, lazima kuna mtu atasema 'mimi kuna miradi yangu', lakini tunajenga reli, mabehewa yana viti vya ngozi. Hivi mmefikiria namna gani ya kuendeleza zao la katani kuhusu mradi huu?" alihoji.

"Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu wako, (Prof. Adolf Mkenda) ni mwalimu wangu wa uchumi mwaka wa tatu, amenifundisha sekta zote za uchumi yaani unachukua, unatafuta njia hii na njia hii, ukiingiza unapata kila kitu. Mimi sitaki kumwambia nimrudishie 'degree' (shahada) yake kwa sababu kwa sasa yeye ndiye Katibu Mkuu katika wizara hivyo anawajibika."

Zitto alisema katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Machi 2016 hadi Machi mwaka huu, bidhaa za viwanda ambazo Tanzania inauza nje, zimeshuka kwa Dola za Kimarekani milioni 500 kutoka Dola bilioni 1.4 mpaka milioni Dola 0.9.

"Tunaposimama hapa na kusema kazi inafanyika, waziri atusaidie kwamba, iwapo kazi inafanyika na kuna ongezeko la uzalishaji, ni kwanini mauzo yetu nje yamepungua kwa kiwango kikubwa? alihoji.

"Na haya ndiyo mambo ambayo ni vizuri Waheshimiwa Wabunge wazingatie kwa sababu bidhaa za viwanda vinazouzwa nje zinapopungua ni kwamba, viwanda vyetu vya ndani vimepunguza uzalishaji na maana yake kuna watu wamepoteza kazi na kuna mapato ya serikali yanapotea."

Aliendelea kulieleza Bunge kuwa ndani ya miezi 12, Tanzania imepoteza mauzo ya nje kwa Dola milioni 500 na kufikia 2020 anaamini hakutakuwa na senti moja kutokana na mauzo hayo.

Zitto alisema Tanzania ina tatizo kubwa la kulinda viwanda vya ndani ambalo alisisitiza kutokana na bidhaa nyingi za nje kuingizwa nchini kwa magendo.

"Wanaingiza mafuta ya kula kinyemela katika nchi yetu, wanaingiza betri ambazo zinakuwa za bei ndogo na matokeo yake ni kwamba, viwanda vya ndani vinashindwa kushindana nao katika soko," alisema.

Akifafanua kuhusu betri, Zitto alisema takwimu za Idara ya Wateja ya China zinaonyesha kiwango cha betri ambacho kimeingizwa nchini kutoka China katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka 2016 ni kikubwa, lakini nyingi zimeingizwa kinyemelea.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha kati ya Januari na Septemba mwaka jana, betri kutoka China zilizoingizwa nchini zina thamani ya Dola za milioni 36.5.

"Ukija kuangalia kwa Idara yetu ya Forodha hapa nchini, betri ambazo zimeingia nchini na ukalinganisha na TBS (Shirika la Viwango), betri ambazo wamezifanyia ukaguzi zimeingia nchini Dola milioni 5.3, maana yake ni kwamba kuna betri nyingi sana ambazo zinaingia nchini hazipiti katika njia ya kawaida," alisema.

Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema viwanda vinavyozalisha betri nchini, mfano Panasonic, ambavyo vimeajiri watu, vinashindwa kushindana na vile vya China.

"Tafsiri yake ni kwamba, tutaongea humu kuhusu viwanda na haya ni mambo ambayo tunategemea kuona waziri ukihangaika nayo kwa sababu wahenga walisema bora ndege ambaye unaye mkononi kuliko ambaye yupo juu ya mti," alisema.

"Tuna mradi wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni saba katika reli. 'Material' (malighafi) yake sehemu kubwa ni chuma, unahitaji tani 50 za chuma cha pua kujenga kilometa moja ya reli. Siyo kwamba hatuna chuma, tunacho Mchuchuma na Liganga.

"Tumewapa Waturuki zabuni ya reli. Wataleta chuma kutoka kwao, ajira zitakwenda kwao. Kabla ya kuanza kufikiria kutandika chuma cha reli, ilitakiwa tuwe tayari tumejenga uwezo wa kuzalisha kule ili fedha zote zibaki kule na ndani ya nchi. Mimi nashindwa kuelewa."

Huku Zitto akishangiliwa na wabunge wa vyama vyote kwa kugonga meza kutokana na mambo ya msingi aliyoyasema katika mchango wake, Waziri Charles Mwijage alimpigia saluti mbunge huyo kuonyesha kukoshwa na mchango wake.
 
katuni-20p6x-jpg.511440
 
Tuna chuma hapa nchini lakini chuma ya kujengea reli yetu itatoka nje ya nchi!!

Ndio maana huwa naleta mada kuhusu sisi Waafrika ila wengi najua huwa hamzipendi lakini huu ndio ukweli sisi watu weusi tuna mapungufu makubwa sana.

Tatizo lingine hatutaki kukiri kuwa sisi tuna tatizo la asili.

Huwezi kutatua tatizo kabla kwanza hujalikubali/hujalipokea.
 
Nchi yetu maneno mengi sana!Hivi inadhani viwonda ni kuongea ongea?viwanda ni vitendo na mahesabu halisia.

Eti nikasikia wameingiza 70mil Tshs kufufua General Tyre!Hive kwel inakuja akilini kuwa General Tyre imekufa kwa kukosa mil 70 za kitanzania?Unajenga rail, flyover na kununua ndege halafu utegemee uchumi ukue??

Nchi yetu itafika kipindi itakua haikopesheki kwa sababu tumekosa Siasa Safi na Uongozi Bora.
 
Wanatuibia sana hawa si wachina si wazungu wote wanajali maslahi yao tu na wakishajua tuna mafisadi chungu nzima waliojivalisha ngozi ya viongozi basi wanakwapua kupita kiasi.

Nilimsikiliza Zitto aliongea vizuri sana. The guy is good! Ukifikiria sanaaaaa bomba la gas utajua hawa wachina they are up to business kwani pesa yote ilirudi kwao hahahhh bongolala kwelikweli.
 
Tusipoangalia huko kwenye viwanda tutalose na kwenye kilimo tutalose. Maana kama mauzo ya nje ya viwanda yamepungua inaashiria tunarudi nyuma kwenye hiyo sekta. Unasema unataka uchumi wa viwanda halafu unaenda kununua ndege na kujenga reli. Reli ni muhimu lakini tulitegemea uanze na kuongeza uzalishaji wa umeme. Tulitegemea ufufue na kuanzisha migodi ya makaa na kuongeza umeme wa gesi na maji. Naanza kuamini msemo wa Tanzania ya viwonder.
 
Mkuu ni loose loose situation on both sides. You can't win with MUFILISI policies.

Tusipoangalia huko kwenye viwanda tutalose na kwenye kilimo tutalose. Maana kama mauzo ya nje ya viwanda yamepungua inaashiria tunarudi nyuma kwenye hiyo sekta. Unasema unataka uchumi wa viwanda halafu unaenda kununua ndege na kujenga reli. Reli ni muhimu lakini tulitegemea uanze na kuongeza uzalishaji wa umeme. Tulitegemea ufufue na kuanzisha migodi ya makaa na kuongeza umeme wa gesi na maji. Naanza kuamini msemo wa Tanzania ya viwonder.
 
Wanatuibia sana hawa si wachina si wazungu wote wanajali maslahi yao tu na wakishajua tuna mafisadi chungu nzima waliojivalisha ngozi ya viongozi basi wanakwapua kupita kiasi.
tutaendelea wote kwa kila mmoja kujikita kwenye kuwekeza kwenye fursa zote kubwa na ndogo. Kutegemea mzungu au mchina kutapelekea kuwa masikini wa kudumu na waliodumaa hadi kiyama
 
Watoa hizo fursa ndiyo wamegoma kuzitoa kwa Watanzania. Kumbuka kauli ya Muhongo kwamba Watanzania wanaweza biashara ya Juice tu na hakuna yeyote ndani ya Serikali aliyemkemea na kauli yake ile.

tutaendelea wote kwa kila mmoja kujikita kwenye kuwekeza kwenye fursa zote kubwa na ndogo. Kutegemea mzungu au mchina kutapelekea kuwa masikini wa kudumu na waliodumaa hadi kiyama
 
Tanzania haiwezei kuwa nchi ya viwanda unless warudishe viwanda vilivyotaifishwa mwaka 1967 wakati wa azimio la arusha kwa wenyewe.
Huwezi kuita watu wawekeze wakati ulishataifisha viwanda vya watu wengine.
 
Back
Top Bottom