Zitto, Januari mashujaa dhidi ya wapenda posho! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto, Januari mashujaa dhidi ya wapenda posho!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Feb 23, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]


  Katika mkutano wa sita wa Bunge la Tanzania,ulioahirishwa saa 11 jioni, Februari 10, mwaka huu kinyume cha hali ya kawaida, mjadala wa posho ulifunika karibu kila kitu. Na bila shaka, wito wa ‘laana' dhidi ya wapinzani wa posho mpya ulishika kasi.
  Lakini hata hivyo, ‘laana' hiyo haikuwa na nguvu. Ndani ya kikao hicho, Kabwe Zitto, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) na Januari Makamba, Mbunge wa Bumbuli- Tanga (CCM), waligeuka ngome ya wananchi wengi dhidi ya mashambulizi hayo.


  Kwa lugha rahisi, ni kama vile wananchi wengi wapinga ongezeko hilo walitanguliza kikosi chao hicho kidogo mbele ya jeshi kubwa lenye njaa ya posho mpya. Ni kama vile ndani ya kikao hicho, Januari na Zitto walishindwa ingawa pia, hawakuwa mateka wa kikao hicho, waliendelea na msimamo wao.


  Lakini tofauti na Zitto, taarifa za kina zinaeleza kuwa Januari aliweza kuungwa mkono na kijana mwenzake ndani ya sekretariati ya CCM, Nape Nnauye.


  Hawa walikuwa katika mawasiliano ya karibu ‘kukabiliana' na nguvu kubwa ya wabunge wa chama chao. Lakini mbali na ‘mtandao' huo wa Zitto, Januari na Nnape kwa upande mmoja, Ikulu ni kama ilikuwa nyuma yao .


  Ilibidi Ikulu kujitokeza mbele kusaidia ‘mtandao' huo mdogo lakini wenye kuungwa mkono na wananchi. Baada ya Spika kutaka kuuaminisha umma kuwa Rais ameidhinisha posho mpya, Ikulu ilitoa taarifa fupi, ikieleza Rais hakufanya hivyo, isipokuwa amewataka wabunge kutumia busara katika suala hilo la posho.


  Na hatimaye, Naibu Spika, Job Ndugai, akajitokeza na kusema, hakuna nyongeza ya posho mpya. Lakini wakati wote, mjadala mwingine uliokuwapo ni wapi fedha hizi za ziada za kulipana posho zitapatikana.


  Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini, mpango wa kuchukua fedha hizo kutoka katika mradi wa ujenzi wa nyumba za wabunge ( Bunge Village ) ambao ulipangwa kufanywa kwa kushirikisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).


  Hii haikuwa safari rahisi kwa Januari na Zitto, ambao muda wote ilibidi, hata hivyo, wafanye kazi nyingine za kitaifa na wabunge wenzao wenye uchu wa posho mpya.


  Inaelezwa, posho ziliwaunganisha wabunge wa kambi zote, upinzani na chama tawala, kasoro hao wabunge wachache, ingawa wengine walichagua kukaa kimya, lakini angali mioyo yao ikitamani posho mpya.


  Katika hali ya kipekee, Zitto na Januari wamefanya kazi kubwa kwa niaba ya sehemu kubwa ya wananchi, angalau kuna fedha fulani zitafanya kazi ya maendeleo tofauti na ambavyo uamuzi wa posho mpya ungeidhinishwa, ingawa pia ni vigumu kupima namna matumizi hayo ya fedha iliyookolewa yatakavyokuwa.


  Bunge na mgomo wa madaktari 0Wakati wabunge wakiwa katika mvutano wa kung'ang'ania posho mpya, madaktari nao walikuwa wakidai nyongeza ya posho, mazingira bora ya kazi na kuthaminiwa kama watalaamu muhimu kwa Taifa.


  Ni kweli, kwa muda mrefu, kama ilivyo kwa walimu, madaktari hawakuthaminiwa kama ilivyotarajiwa. Umuhimu wao ulitambuliwa na kiongozi au raia mmoja mmoja, tena baada ya kutibiwa na kunusurika kifo.0Mengi ya madai yao yalikuwa ya msingi. Lakini nao walidai katika njia isiyomuadhibu aliyepaswa kuwa mfano wa kwanza kuwathamini, yaani Serikali. Wenzetu hawa waliwaadhibu waliovunjika viungo kwa ajali au wanaohitaji upasuaji. Kwa ujumla, waliwaadhibu wagonjwa wenye maumivu makali, na hasa wale masikini ambao husaka tonge juani kila kukicha.


  Wakati madaktari wakiwa katika "malumbano ya hoja" dhidi ya maofisa waandamizi wa Serikali, wagonjwa walikuwa wakijigeuza vitandani wodini kubahatisha kama kwa kufanya hivyo, wangepunguza maumivu makali ya ugonjwa unaowasumbua.


  Kwa hiyo, wakati madaktari wakirejea kwenye makazi yao kuungana na familia zao baada ya kutwa nzima kulumbana na Serikali, wagonjwa wenyewe waliendelea kufuta machozi ya maumivu makali na ndugu zao, wakiomba Mungu mgonjwa wao apate uhai wenye maumivu kidogo kidogo hadi mgomo uishe.


  Masikini, macho ya wagonjwa yalizidi kumwagika, wakaanza hospitali ikiwamo ya Rufaa Muhimbili. Sehemu kubwa ya vitanda wodini vikabaki wazi, wagonjwa wengine waliitwa na Mwenyezi Mungu kwenye pumziko la milele, wakiwa na alama za ugonjwa ambao ungeweza kutibiwa na madaktari waliogoma. Wengine ambao hawakuitwa na Mwenyezi Mungu, kwa uchungu waliondolewa na ndugu zao kwenda kutibiwa wanakokujua.


  Kwa ujumla, mawasiliano ya kitabibu kati ya mgonjwa na tabibu yalikatika, yakabaki mawasiliano kati ya viongozi wa Serikali wenye afya na madaktari wenye afya tele.


  Katika wakati wote huo wa wagonjwa kulowesha magodoro ya hospitali kwa machozi ya maumivu, wabunge ambao ni majeruhi wa posho mpya, wakaanza kupata uchungu, wakikumbuka wanaoteseka ni wapiga kura wao, ingawa Uchaguzi Mkuu ni mwaka 2015, lakini lazima kutambua uchaguzi mdogo unaweza kutokea kabla popote nchini.

  Wabunge sita tofauti, walijaribu kutaka muhimili huo wa dola ujadili suala hilo , hao ni pamoja na John Mnyika wa Ubungo (CHADEMA), Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki (CCM) na Peter Serukamba-Kigoma Mjini (CCM). Dhamira ya wabunge hawa haikutimia.

  Bunge likaamua kumpa nafasi kushughulikia kadhia hiyo, Waziri Mkuu Pinda, ambaye mwanzo wa mgumu alitoa tamko madaktari warudi kazini, wasipofanya hivyo watakuwa wamejifukuzisha kazi. Pinda alitoa kauli hiyo, wakati Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, Naibu Waziri, Dk. Lucy Nkya na Katibu Mkuu wa Wizara, Blandina Nyoni, wakiwa katika mvutano mkubwa na madaktari, ikiaminika wao ni chanzo cha tatizo.


  Kwa hiyo, mawasiliano yalikatika kati ya uongozi wa wizara na madaktari. Madaktari walitii agizo la Waziri Mkuu, wakaripoti kazini lakini bila kufanya kazi, wagonjwa wakizidi kulia kwa maumivu.


  Joto la Bunge kutaka kujadili suala hilo likazidi kiasi cha uongozi wa Bunge, chini ya Spika Makinda, ukakabidhi jukumu hilo kwa Kamati ya Huduma za Jamii inayoongozwa na Margreth Sitta. Waziri Mkuu akarudi Dar es Salaam kutoka Dodoma ili kukutana na madaktari Jumatano wiki ya mwisho kabla Bunge kukamilisha mkutano wake wa sita.


  Katika kikao hicho, Katibu Mkuu, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu, Dk. Deo Mutasiwa, wakasimamishwa kazi na Rais Kikwete akaachiwa kibarua cha kuamua hatua ya waziri na naibu wake. Madai ya ongezeko la posho na mazingira mazuri kwa madaktari yakasilizwa na kutolewa uamuzi wa kuridhiwa na Waziri Mkuu.


  Madaktari wakachukua sindano, mikasi ya upasuaji kurejea wodini lakini loo, wagonjwa wengine walikwishaitwa na Mwenyezi Mungu kwenye pumziko la milele kwa kukosa matibabu wakati wengine wakiwa wameamua kwenda kujiuguza nyumbani, yaani, idadi ya madaktari ikawa kubwa kuliko wagonjwa pale Muhimbili kwa mfano. Hapa, tunajifunza kuchukua hatua za haraka kabla maafa, hasa maafa yanayogusa uhai wa Watanzania.


  Shukurani kwa madaktari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliofika Muhimbili kusaidia kazi wakati wa mgomo, inawezekana wameokoa maisha ya baadhi ya Watanzania wenzetu, Mungu awajaalie.
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 3. M

  Molemo JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wewe mleta mada ni mtu mnafiki sana
   
 4. M

  Molemo JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Wewe mleta mada ni gamba tena la kobe.Kuna kitu unakitafuta kwa unafiki wako.Kalambe miguu ya magamba wenzako
   
 5. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwanini unaniandama sana mzee?hapa unafiki wangu uko wapi sasa?kueleza kilijiri dodoma bungeni au nini?mzee unanichukia mpaka najua kwamba unanichukia bwana..!zuia kidogo chuki zako kwangu maana hamna jema nitakaloweka hapa ina mana hutaki nishiriki mijadala humu ndani au?
   
 6. M

  Molemo JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Sipendi mada zako za kinafiki.Kuna kitu unachokitafuta kwenye hii mada.Ni juzi tu ulileta mada hii hii ya posho na ukamlaani Mbowe kwamba eti yeye anapanga foleni kuchukua posho.Watu tuliijadili ile mada na ukaonekana unataka kupandikiza vurugu kwa hila ndani ya CDM.Leo tena unaleta mada hiyo hiyo kama si unafiki ni nini? Sikuchukii wewe kama mtu bali nachukia hila zako chafu za kuiandama CDM kupitia mtandaoni.
   
 7. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo kumsifu mbunge wa chadema ni kuiandama chadema??!!kuna nini huko chadema lakini,maana katika hali ya kawaida ilitakiwa mtembee kifua mbele kwa mbunge wenu kuonyesha ushujaa au mbunge huyu hamumkubali?kama ndio unadhani kwa kwanini ?
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nimesema una hila ovu kwenye mada yako.Huna lengo lolote la kumsifu mbunge wa CDM.Lengo lako kuu ni kuleta fitna CDM.Mada zako zote hapa JF ni kwa lengo la kiuvuruga CDM.Nina uhakika humpendi mtu yeyote ndani ya CDM bali una hila chafu dhidi ya viongozi wa CDM
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo kama hii issue ulitaka niiweke vipi ili ulidhike na kuona nina nia njema na chadema???tatizo watu wa chadema mnadeka sana humu ndani kwa kuwa mnadekezwa na jf,mnapenda kusikia mnayoyataka tu,sisi wengine tuna fair mtu akifanya vizuri tutamsifu bila kujali anatoka upande gani akichemka halikadhalika,hatuna mapenzi kupita kiasi na vyama na kulisahau taifa ndio mana tuko pamoja na wabubge wanyonge waliojotoa muhanga kupinga unyonyaji wa kodi zetu kufaidisha wachache,namzomea mkamia na genge lote la wapenda posho,wewe kama unampenda mbowe au mnyika au juma nkamia kuliko taifa huo ni udhaifu wako,siwezi kukubadilisha.
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Narudia tena una hila ovu dhidi ya CDM.Mbinu yoyote ya kuivuruga CDM haitafanikiwa.Watu wote hapa JF wanakujua wewe ni gamba.CDM iko imara chini ya Mbowe,Slaa na Zitto.Mbinu yako ya muda mrefu kuvuruga watu hawa asilani hutafanikiwa
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kuijadili cdm au ccm sio lazima uwe mwanachama wa chama husika ndio mana unaona tunavijadili vyama mbalimbali humu kuanzia cuf,ccm cdm,tlp mpaka tpp kwa kuwa hili ndio jukwaa husika na sisi ni wachambuzi wa mambo ya siasa kwa vyama vyote japo kila mtu wengi wetu tunavyo vyama hata marekani unaona mchmbuzi wa anaichambua republican hata kama yeye ni democrat and vice versa na wanakaa pamoja wanajadili wanatoa mapendekezo yanayofaa yanachukuliwa bila kujali yametoka kwa mchambuzi shabiki wa chama gani,tubadilike,hakuna mambo ya hiki chama changu wewe huna ruhusa kukijadili,hatutafika.
   
 12. M

  Molemo JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo uchambuzi wako wa siasa kila siku unalenga tu CDM? Mbona hujadili CCM,CUF,TLP au UDP? Narudia tena tumechoka na hila zako
   
 13. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  kim kardashian(original) anaweza kutoa uchambuzi mzuri kuliko anavyochambua nguo nzuri za kuvaa,..msimamo wa CDM wa kupinga posho upo hadi kwenye ilani yao,..unapong'ang'ania zitto peke yake ndiye anayepinga posho tunakuwa tuna wasiwasi na wewe kwamba unajaribu kumjengea ushujaa zitto peke yake as if swala la posho ni lake binafsi na sio la chama.
   
 14. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbona nachambua mambo mengi sema wewe tatizo lako ukiingia humu husomi thread yeyote isiyo na jina la slaa au chadema ndio maana nakusumbua otherwise ukitaka nitakuwekea thread zangu toka nijiunge then upime...
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwa hiyo wewe kwa kuwa sio dini moja na mimi ndio maana unaunga mkono posho ya kukaa tu kitako ya wabunge wetu au?
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Posho haipingwi kwa mdomo au kwenye makaratasi huku mkono mwingine unaupenyeza kwa nyuma na kuichukua,huo ni ulaghai mkubwa kwa watanzania walipa kodi na wapiga kura,tunataka posho ipingwe kwa vitendo ndio maana tun awapongeza hawa vijana sio kwamba tunawapendelea bali wameonyesha uzalendo na kuizidi nguvu tamaa ya kujilimbikizia mali ambayo imewazidi nguvu wanaonena mengine kwenye ilani na mdomoni lakini wantenda vingine kabisa.Zitto hayuko peke yake huko chadema kama ilivyo januari ccm,kuna sapoti kubwa nyuma yao kutoka kwa wanachama wa vyama hivyo wenye uzalendo na uchungu na kodi zetu,nyie mlio na uchungu na wanasiasa maarufu kuliko taifa na walipa kodi mko wachache sana..na mnajidanganya kwamba mko wengi.
   
 17. L

  Ludewa JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli wabunge wote wa CDM wanapinga posho? Joseph Selasini je?
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mzee achana nao hawa waswahili watakuchosha tu bure,hawa ni kama mang'ombe tu wanaswaga wanakwenda bila kuhoji wanakopelekwa,wanakitegemea kichwa cha mchungaji kufikiri kwa niaba yao,suala liko wazi lakini hawalioni kisa,wabunge wote wa cdm akiwamo bwana mkubwa wanalamba posho ya kukaa kitako pale mjengoni kama kawa,shukrani pekee kwa mh.zitto kusimama pamoja na umma katika hili
   
Loading...