Ufipa-Kinondoni
JF-Expert Member
- Jan 3, 2012
- 4,582
- 2,783
WanaJF salam,
Mimi ni moja ya wale ninayependa hoja za Mh. ZZK na siku zote nimekuwa naye. Pale bungeni sijawahi sikia ameongea tusi au kejeli, zaidi ya hoja. Amekuwa anafundisha na anasimamia fikra zake kwa hoja. Tangu akiwa CHADEMA nilikuwa nafuatilia hoja zake.
Katika siku za hivi karibu ameamua kusimama pekee yake katika siasa. Binafsi naona haya ndo yanamsukuma ZZK kufanya anayofanya. Ninachoona ni kuwa anataka kusimama peke yake katika siasa.
Anataka kuinua chama chake pekee yake. Anakitanganza kwa nguvu. Anataka kila siku kisikike katika media. Amekuwa kinara wa kutoa chambuzi za upotoshaji katika mitandao. Kwa siku amekuwa anapost maandiko zaidi ya 10. Katika yote huwa anamtaja Magufuli zaidi ya 4 mpaka 10. Hii ni hatari kwa vile anatafuta kupanda kwa nguvu.
Kama kweli anaona haki zinaminywa angetafuta njia mwafaka kabisa, kabla ya kuja na hayo. Aungane na Mbowe aliyetafuta njia ya haki ya kimahakama ili apate ufafanuzi wa demokrasia ya kufanya mikutano. Anachofanya kwa sasa ni kupima kama kweli polisi wasumbua kama Mtikila alivyokuwa anajaribu sheria mahakamani.
Ila kwa vile lengo lake ni kujulikana hata akipigwa na polisi itakuwa zao la umaarufu. Huwezi kusema kwa vile wao wanaharibu basi na wewe unaharibu. Kwa nchi za Kiafrika shida demkrasia ni ya kuokoteza. Hata Marekani, si kila kitu ni huru. Kila mtu anaona yanayotokea sasa kwa Trump. Wamejipanga na watamng'oa tu. Kwa sababu anayofanya hayapendezi serikali ya Obama hata wengine.
Hili si jambo jipya katika siasa duniani. Ikumbukwe kuwa Waziri Mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras wa chama cha Syriza alipata nafasi ile kwa kutumia mitandao ya kijamii kama ZZK anavyofanya Kwa sasa. Alipotosha sana na akafanikiwa kuwa Waziri Mkuu kijana kuwahi kutokea Ulaya yote. Lakini kila mtu anajua kilichomkuta katika miezi minne tu ya utawala wake na sasa yuko wapi. Hapa ndo unaweza jua, mitandao ina faida sana kama tutakuwa na ujuvi wetu kabla ya kuambiwa.
ZZK anajua weakness kubwa aliyonayo kwenye chama chake. Hana hata Katibu Mkuu au watu walio na uelewa wa kiuongozi anaoweza shiriki naye katika siasa.
Binafsi namshauri aangalie jinsi ya kuongeza nguvu katika chama. Atafute safi ya kuaminika kisiasa na ashiriki nao. Kwa sasa maneno anayotoa kukejeli Magu, hayatasaidi. Aandae sera zuri zitakazopambana naye 2020 kutokana na madhaifu haya.
CHADEMA ilipo hapa hata CUF hazikujengwa na mtu mmoja. Ishirikisha watu wengi. Walikuwepo wanaotafuta rasilimali fedha, wanaofanya tafiti za kisiasa na waliokuwa wanapanda majukwaani. Hawa hawapo ndani ya ACT mpaka sasa.
Kwa maana hiyo, hataweza kutoka peke yake katika wakati huu bila kuwa na safu inayoweza kushiriki anachofanya.