Zitto ataka hatua kali zichukuliwe dhidi ya askari polisi aliyemtishia bunduki Malima

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Katika hali isiyokuwa ya kawaida iliyotokea mapema hii leo jijini Dar es salaam kwa kitendo cha cha aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha katika utawala wa awamu ya nne. Adam Malima kutishiwa bunduki na askari mmoja aliyekuwa doria kimewashangaza wengi na kupelekea Mbunge wa Kigoma Mjini, Zuberi Zitto Kabwe kuonyesha masikitiko yake hadharani kwa kitendo alichofanya askari huyo.

Zitto Kabwe ameonesha masikitiko hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii Facebook akihoji kama polisi wanafundishwa kuwafanyia hivyo raia wasiokuwa na hatia kiasi cha kuibua hofu katika jamii inayowazunguka na kupoteza imani na jeshi la polisi.

"Hivi ni nini? Askari wetu wanafundishwa kufanya hivi? Waziri Mwigulu Nchemba Huyo yupo wazi na ni wa kutoka kwako. Unahitaji uchunguzi "? . Ameandika Zitto.
 
soldier acted wisely,propotionaly and his mind was of common man test,infact if you look the clip critically you may observe the gun is not targeted to any civilians but what can be seen is to observe the principle of propotionality
Moreover,the act of discharging bullet can be retionalize as the threat of the mob who were presurized by the retired honorable malima.
Its my own views my felow soldier acted reasonably to protect his life and to secure his job as the mob were seen to have overt acts to indanger peace.
lastly, the act of discharging bullet should not be intepreted as unnecessary exessive force but it was the initiative measures to calm down the situation
MY OWN OBSERVATION
 
polisi wanapaswa kuogopwa kama majeshi majeshi, hii ni namna ya kuyafanya yaogopwe.! huyu askari atapandishwa cheo.

i don wish again to be like IGP

Tahadhari mtu akiwa na bunduki namna ile sio vema kuendelea kubishana naye ukimlazimisha ajue wewe ni nani kama Mr SMG alivyofanya
 
A
Huyu naye hakuna kinachompita kila kitu lazima afungue mdomo tumekuchoka.....Askari nao wamechoka dharau zenu na maneno ya kejeli.Mjirekebishe kwanza ndio muanze kuongea.Foolish
Acha ujinga nawewe umeona ni sahihi? Ndio maana mtaishia kuonewa siku zote. Ingekuwa wewe umefanyiwa vile mkuu naona hadithi ingebadilika. Muandike vitu endelevu vyenye kusaidia sio kuandika tu for the sake of writing
 
Zito yuko vizur sana, watu wenye kufkr mambo kwa kina wanaelewa!, tatizo yupo kama jesh LA mtu mmoja kwenye chama chake! Hatengenez watu wengine kuonekana ndan ya chama! Saut mmoja kilasiku raia wanaichoka
 
Japokuwa mnamponda

ZZK anahoja ya msingi kabisa

kulikuwa na ulazima wowote kutumia silaha?

Hawa polisi wanakoendea siko kabisa

Na serikali isipoziba ufa......itajenga ukuta.
 
soldier acted wisely,propotionaly and his mind was of common man test,infact if you look the clip critically you may observe the gun is not targeted to any civilians but what can be seen is to observe the principle of propotionality
Moreover,the act of discharging bullet can be retionalize as the threat of the mob who were presurized by the retired honorable malima.
Its my own views my felow soldier acted reasonably to protect his life and to secure his job as the mob were seen to have overt acts to indanger peace.
lastly, the act of discharging bullet should not be intepreted as unnecessary exessive force but it was the initiative measures to calm down the situation
MY OWN OBSERVATION
Heeee heeee hicho kiinglishi cha wapi? Heeee heeee uwiiiiii jamani jamani si utumie tu hiki chetu mkuu??? Mama mia
 
jinsi zitto alivyo mzito,kama yeye ndio angekuwa huyo bwana malima,kitendo cha askari kuonesha ile bunduki angegandishwa fasta na kuwa kama lile sanamu la askari la posta.
 
Yule askari kafanya kitendo cha kihuni....
Askari wanatakiwa wapewe course za anger management.
Ipo siku watakuja kuua watu.
Ile bunduki alikua kaishikilia kihasara hasara sana na safety alikua ameisha itoa. katika kuirusha rusha ange bonyeza trigger kwa bahati mbaya yangekua mengine pale.
Askari wote walio kuwepo hapo wawajibishwe.
Back to malima nae achukuliwe hatua za usalama barabarani za kupaki gari yake vibaya.
 
soldier acted wisely,propotionaly and his mind was of common man test,infact if you look the clip critically you may observe the gun is not targeted to any civilians but what can be seen is to observe the principle of propotionality
Moreover,the act of discharging bullet can be retionalize as the threat of the mob who were presurized by the retired honorable malima.
Its my own views my felow soldier acted reasonably to protect his life and to secure his job as the mob were seen to have overt acts to indanger peace.
lastly, the act of discharging bullet should not be intepreted as unnecessary exessive force but it was the initiative measures to calm down the situation
MY OWN OBSERVATION

Wewe ni askari kweli? Yule jamaa anaongea kama anataka kulia halafu unasingizia hali?

He was trying to calm his nerves hakukua na threat ya kupanic kias kile

Sijui kwa daktari naye akijibiwa vibaya afanyaje. Anashoot sindano hewani?

Mwalimu je?

Ukishakua katika "line of work fulani" lazima uwe na weledi wa kujizuia emotions over rational thinking
 
Back
Top Bottom