Zitto ataja mawaziri mizigo

Mkuu wewe ni mtungaji na msimamizi wa hizo sheria na sera hivyo ni wajibu wako kuwasilisha rasimu ya marekebisho ktk ngazi husika.

Kuhusu bei za viwanja, inakuwaje gharama za kupima mtwara ziwe tofauti na zile za dar?

Mimi naona bado unatakiwa kuufanyia kazi ushauri huu hata kama umeletwa kwa style ambayo kwako itakuwa sio sahihi.
 
Hao tunawafahamu Zitto tutatie walificha mabilioni Uswis ....hii aiuzi!
 
Hawa Mawaziri wa Ardhi ndo mizigo namba moja.

Makazi bora ni kwa matajiri tu, masikini wataishia slams tu.

Hata postal codes wameshindwa, maana hakuna mipangilio ya makazi.

Ardhi ni zawadi ya Mungu kwa watanzania, kwanini iuzwe ghali ivo.?

Refer: Link- Waziri wa Ardhi na makazi challenges
 
Kuna Mwalimu wangu mmoja wa Psychology alitusimulia hadithi hii "Kuna jamaa alikwenda mtoni kufua nguo,sehemu aliyokuwa anafulia nguo ilikuwa ni upande wa chini wa mapolomoko ya mto,ghafla akaona mtoto akiporomoka kutokea sehemu ya juu ya mto na kuangukia kwenye bwawa,akamuwahi kumuokoa,mara akatokea wa pili akafanya hivyo hivyo,akatokea wa tatu akafanya hivyo hivyo hali kadhalika".Kwa kuangalia tukio hili utaona kwamba jamaa (mwokoaji) alikuwa anatumia DOWN-STREAM STRATEGY kuwaokoa hawa watoto mtoni jambo ambalo halikuwa sahihi kabisa kwani alichopaswa kufanya ni kuitumia UP-STREAM STRATEGY yaani kwenda kule juu maji yanapotiririka kutokea kuona ni nini kinasababisha wale watoto kuporomoka mtoni ili azuwie.Nimetoa mfano huu mdogo ili nilinganishe na kinachoendelea katika Serikali ya Kikwete hususani Baraza la Mawaziri.Kuwalaumu Mawaziri pekee hakutoshi ebu tuangalie na mfumo mzima wa kiutawala na kiserikali huenda madhaifu mengi yanayosababisha Mawaziri na Watendaji wengine wa Serikali waonekane hawafai.
 


Shule hii ya Down Stream na Up Stream umeinyumbulisha vizuri sana. Many kudos for your enlightment.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…