Zitto anusurika kipigo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto anusurika kipigo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, juzi alikuwa miongoni mwa abiria walionusurika kupigwa baada ya wananchi katika eneo la Kabuku, wilayani hapa kufunga barabara kwa muda wa saa tatu...

  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 12 jioni katika Kijiji cha Komkonga, Kata ya Kabuku, Barabara ya Chalinze-Segera, baada ya wananchi kuzuia magari yanayopita barabara hiyo, na kutishia uhai wa yeyote ambaye angethubutu kuingilia harakati zao.

  Akizungumza na Tanzania Daima ofisini kwake jana, Ofisa Upelelezi wa Mkoa wa Tanga, Japhari Mohamed, alisema hali ilikuwa tete mahali hapo baada ya gari kumgonga na kumuua mtembea kwa miguu aliyejulikana kwa jina la Mohamed Idrisa (30).


  Alisema Idrisa aligongwa na basi aina ya Isuzu, mali ya Kampuni ya Tahmeed, yenye namba za usajili KAY 177 A iliyokuwa ikiendeshwa na Athuman Abbas (34).


  Ofisa upelelezi huyo alikiri Zitto kunusurika na kipigo, lakini akasema haikujulikana mara moja mwanasiasa huyo alikuwa anaelekea wapi.


  Alisema kilichotokea ni kwamba baada ya Zitto kufika eneo la tukio, alishuka kwenye gari alilokuwamo, akaanza kuwasihi wananchi hao waliokuwa na hasira na jazba.


  “Ni kweli Zitto alikuwa mmoja wa abiria waliokumbana na adha ya wananchi kufunga barabara… aliamua kushuka kwenye gari lake na kwenda kuwasihi, jambo ambalo hakufanikiwa hata kidogo, huku wananchi wakikataa kumsikiliza.


  “Kutokana na hali hiyo, wananchi walimwambia hawataki siasa bali wanamtaka Rais Jakaya Kikwete au Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Meja Jenerali mstaafu, Said Kalembo,” alisema Mohamed.


  Alisema baada Zitto kuelezwa maneno hayo, aliamua kuondoka na kwenda moja kwa moja kwenye gari lake kwa ajili ya kujiokoa na dhahama hilo.


  Alisema wananchi hao walikuwa wanashinikiza kuwekwa matuta katika eneo hilo kwa madai kuwa wamechoshwa na ajali za mara kwa mara zinazotokea eneo hilo.


  Alisema polisi wa kituo cha Kabuku walishindwa kuwatawanya wananchi hao na kulazimika kuomba msaada kutoka mkoani ambako askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) walifika na kutumia mabomu ya machozi.


  Katika ghasia hizo mtu moja alijeruhiwa, baadhi ya magari kuvunjwa vioo huku watu 35 wakikamatwa kuhusiana na tukio hilo.


  Kamanda huyo alisema ni kosa la jinai wananchi kufunga barabara kuu kinyume cha sheria.


  Gazeti hili lilipomtafuta Zitto kuhusu tukio hilo jana, hakupokea simu; mwandishi akamwandikia meseji kumuuliza habari za tukio hilo; mbunge huyo naye akajibu kwa kifupi: “nimenusurika kupigwa mawe wapi?”


  Mwandishi akamjibu kwa meseji: “Imetumwa stori kutoka Kabuku, Tanga.” Zitto hakujibu tena.


  Hata hivyo, mmoja wa watu waliokuwa na Zitto katika safari hiyo, aliliambia gazeti hili kwa simu jana kwamba kina Zitto walipofika eneo la tukio walikuta foleni ndefu ya magari yapatayo 400 yaliyokuwa yamezuiwa na wananchi hao kwa mawe na magogo.


  Ndipo Zitto akashuka kwenye gari lake, akitaka kuzungumza na wananchi hao. Akamwendea mkuu wa kituo cha polisi cha Kabuku kumsihi amruhusu ahutubie wananchi hao, lakini mkuu wa kituo alikataa kwa kuhofia usalama wa Zitto.


  Kwa mujibu wa mtu huyo, vile vile, wananchi wenyewe waligoma kumsikiliza Zitto, ambaye alijitambulisha kama waziri kivuli; wanakijiji wakasema wanamheshimu, lakini wanataka kumsikiliza mkuu wa mkoa. Wakamtaka Zitto arudi kwenye gari lake alale. Polisi nao wakamshauri Zitto aondoke.


  Chanzo hicho cha habari kilisema hata hivyo Zitto aliweza kuzungumza na wananchi wachache waliokuwa karibu naye, huku akiwa amezingirwa na polisi, lakini walimpa ujumbe huo huo.


  Mnamo saa nne za usiku ndipo askari wa FFU walipowasili mahali hapo na kutawanya wananchi kwa mabomu na kuondoa vizuizi ili magari yaweze kupita.


  CHANZO: TANZANIA DAIMA
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  duh!
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Ni dalili nzuri ya kuonesha ni jinsi gani Watanznia walivyochoka, maana Ajali za uzembe kabisa zinatokea na serikali haifanyi chochote cha maana

  hizo hasira zisiishie hapo tu nadhani hata kwa mafisadi ilitakiwa na wala rushwa wakuu washughulikiwe kwa njia hii
   
 4. R

  Renegade JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,766
  Likes Received: 1,069
  Trophy Points: 280
  Nilifikiri Zito Kabwe peke yake kumbe Abiria wanusurika kipigo, akiwemo zito kabwe. Umaarufu bwana kumbe mtamu.
   
 5. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hasira na umoja kama huo wangeuhamishia kwenye ballot boxes .........
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa,

  Alitaka opportunity ya kujizolea maujiko lakini ikashindikana,
  .... kwe msiba bwana heri kuwa na tahadhari sana.
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Off topic kidogo; Nilifungua hii page nikaiomba Google ifnye translation... hiyo translation iliyotokeas mh! jaribu uone mwenyewe jinsi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo invyokuwa association for Democracy and Developmentau kwa kifupi CCM!!!!
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii ni habari mchanganyiko sio sehemu yake hapa
   
 9. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Watu tumechoka na mambo ya ajali haya na pia ajali nyingi sana zimepoteza maisha ya watanzania wenzetu
   
 10. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwa nini kutumia mabomu ya machozi? kwanini usiite viongozi ukaongea nao na kuwaahidi kipi kitafanyika nao wawaeleze wenzao? I hate kila kitu kutumia mabomu ya machozi hata kwa kitu kinachoweza kuongeleka na kufanyia kazi.
   
 11. Fugwe

  Fugwe JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,680
  Likes Received: 230
  Trophy Points: 160
  Pole Mhe. Zitto lakini umetekeleza wajibu wako
   
Loading...