Zitto amtembelea Lema gerezani baada ya kunyimwa dhamana

Hii kesi kutakuwa na tatizo, sijawahi kusikia kesi inaahirishwa kwa muda wa miezi 2. Ngumu kumeza
 
Hakuna anayefurahia kukaa ndani ya selo huu ni uongo kabisa.Kwa kitu gani hasa ?
Sijui watu wa CCM mkoje kwenye kuelewa mambo madogo tu wala yasiyohitaji mantiki kubwa. Wapi nimeweka neno "Kufarahia" Kutokujuta siyo lazima uwe unafurahia. Haya Magereza yetu ya kujisaidia kwenye mtondoo ndiyo mtu afurahie kukaa huko?
 
Huyu Msaliti nae,mbona yeye nae akamatwi kamatwi?
 
Mfumo wa utawala wa kimabavu katika nchi hii una mwisho. Lema anatufundisha kuwa hakuna hakuna haki katika nchi hii.
Utatoka tu muda si mrefu.
 
Amemuomba "MUNGU" kwa kumpa "MKE" jasiri ambae ndio "NGOME" yake kwa sasa....[emoji15] [emoji15] [emoji15]
Hapo nilitarajia angesema:-
Amemuomba "MUNGU" kwa kumpa "CHAMA" jasiri ambacho ndio "NGOME" yake kwa sasa
 
Kweli Lema alikosea lakini kitendo cha mahaka kuingiliwa huu ni mwendelezo wa mfumo mbovu ambao watendaji wakuu wa vyombo muhimu Kama hivi kuteuliwa.

Makosa ya Lema kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yatathibitishwa na mahakama tu. Kwa sasa Lema ni mtuhumiwa tu.
 
Mie natamani lema akae huko walau mwaka mmoja tu
Huyu kazidisha upuuzi
Hivi Harry Kitilya aliwahi kufikiria atakaa mahabusu, achana na siku moja kupita tu karibu na gereza? Huyo hakimu na wamshurutishao zamu yao yaja.
 
Angalau sasa tunajua kwamba kumbe Lema mwenyewe hajutii kukaa ndani bali anaona anakaa ndani kwa dhuluma. Yana mwisho haya!!
Nikweli Lema sasa anaona kwamba amewekwa mahabusu kwa shinikizo la dola, sio kwa maamuzi ya mahakama.
Lakini........
Mbona Lema amekua mtegemezi mkubwa kwa mke wake na Mungu wake tu.
Sijaona Lema akiwa na mtazamo wa kwamba Chama chake na Mungu ndio kimbilio lake kwa sasa
 
Reactions: MC7
Zitto ni mnafiki tuu ametumia vizuri fursa hiyo kujitangaza yy kisiasa yaan daah kweli kuna fursa za aina nyingi lkn je amemshauri vizur mb lema kwa mizuka yake anapokuwa jukwaan
 
Hivi lipumba bado analindwa na policcm
 
Nipe CV yako kwanza
 
Mbona Lema amekua mtegemezi mkubwa kwa mke wake na Mungu wake tu.
Sijaona Lema akiwa na mtazamo wa kwamba Chama chake na Mungu ndio kimbilio lake kwa sasa
Hujiulizi ni kwa nini Mandela alipotoka Gerezani alipokelewa na Winnie Mandela na siyo kina Oliver Thambo. Vitu rahisi namna hii kueleweka vinapokuwa vigumu kwenu ndiyo inayotufanya tujue ni kwa nini mnawashabikia wale jamaa!!
 
Acha unafiki. Toka mwanzo wa hili sakata la Lema msimamo wako umekuwa hasi sana juu yake.
Sasa hivi umeona kiongozi wa chama chako ameenda kumjulia hali nawe unajifanya muungwana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…