..wakati mwingine wenye matatizo ni waandishi wetu wa habari. hapa palihitajika pawe na follow up questions.
..labda angeulizwa atamsaidia in what capacity and level.
..pia angeulizwa kama atamuunga mkono na kumsaidia mgombea atakayesimamishwa na Chadema Kigoma Kusini.
NB:
..Mkapa alipowaponda hawa ndugu zetu hakuwa amekosea sana.
1. Kama chama cha chadema wanaona Zito kawakosea na yuko kinyume nao, solution ni kumfukuza-Ukimfukuza unaleta sense ya chama kama watu na sio chama kama individual!
2. Chadema kutomchukulia hatua zito, kunaonyesha kuna udhaifu wa chadema kama chama, humo ndani inaonyesha kuna makundi makundi na pengine wanaona wakimfukuza Zitto basi kuna kuvunja chama! kesho atatokea Zito mwingine na kumchukulia hatua itakuwa haiwezekani kwani kuna wengine hawachukuliwi hatua!
4. Kumpa uongozi mkubwa kama huo Zitto na kuonyesha utovu wa nidhamu(kama unavyomuona wewe!) kunaonyesha chama kizima hakina nidhamu, intelligence, wala hakiwachunguzi watu kabla ya kuwapa uongozi, hatari yake ni kuwa kesho kama kuna pandikizi la CCM litaingia na kukiharibu chama na kutokomea, hii ni hatari na si kitu cha kuchezewa mkuu!
1. Kwa nini mtu anang'ang'ania kuwa lazima we mwenyekiti wa chama? refer Mrema, Mbowe n.k
2. Kwa nini hamna demokrasia ndani ya hivi vyama?( refer uchaguzi wa chadema)
hold on...
Zito, chadema, mbowe wenu , slaa....nccr, mrema...cuf, name it..... I real doubt naona hakuna seriousness katika vyama na watu, kiasi cha kusema why dont we think another option! utasema na kuvitetea hivi vyama mpaka unatoka mvi nyeupe kwapani wapi!!!
Mzee Waberoya imebidi nirudie post zako zote kumhusu Zitto nimeelewa msimamo wako kwamba,
-kwa mwenendo ulivyo sasa anasitahili kufukuzwa Chadema tena haraka,
-Chadema ni tatizo kwa nini wanaogopa kumfukuza,
-Hakuna demokrasia ndani ya vyama nk.
Kimsingi kuna mengi nimeyakubali lakini tunatofautiana kwenye utekelezaji wake. Nakubaliana na wewe Zitto kufukuzwa lakini kufukuzwa inategea unamfukuza nani Zitto kwa sasa is a public figure ingawa mbele ya chama wanachama wote ni sawa lakini impact ya kufukuzwa mimi mwanachama wa kawaida na Zitto inatofautiana. Kwa hiyo inatakiwa busara ya hali ya juu ndiyo maana Chadema wanachelea kutoa maamuzi na kuchelea kutoa maamuzi si kwamba wanamuogopa au kina udhaifu ni mambo ya kiufundi tu ndugu yangu. Kinaonyesha uvumilivu na ukomavu badala ya udhaifu unaousema.
Kuhusu wenyeviti umewataja Mbowe, Mrema nk nilishasema uongozi ni kazi sana jaribu wewe kuwa hata mwenyekiti wa kwaya uone kama si kila siku wanakwaya wanatwangana makonde.
Mwisho umesema Zitto alitaka kuiangusha serikali yako ya Daruso 2003-2005 kwani tatizo lilikuwa nini hebu tumegee basi kidogo ili tumjue zaidi kwasababu ni kiongozi wetu sote. Na mimi pia nitakupeni uzoefu wangu ndani ya Daruso wakati wa kunji kubwa la 1990 hadi chuo kikafungwa mwaka mzima wanafunzi wote ilibidi turudie mwaka ukaitwa mwaka wa Mwinyi eti tumemtukana Rais matusi ya nguoni. Enzi za kumbeba Mtikila Nkhruma kusukuma gari la Mrema baada ya kumwaga sera Nkhruma nk.
Ok, kama ni busara kumwacha Ok,
Mbowe, Mrema, Zito, Mwakyembe,Kubenea etc kwa nyakati tofauti wametoa au kuandika statement ambazo zinaelekea kumpa sifa JK! I am against it!
Yes, Zito,Omarlysa, Ridhwan Kikwete etc, waligomea matokea ya urais, wao walikuwa wanamtaka mtu wao na sisi katika kambi yetu ya wahandisi tulisimama kuichukua Daruso, nilikuwa ndani ya chamber wakati kura zinahesabiwa, na kwakweli tulishinda.Mitazamo ya akina Zitto walijua tumebebwa na kwa sababu muda huo VC alikuwa mhandisi basi moto ukawaka.Vurugu zilikuwa kubwa kiasi cha kufungiwa ofisini na kuna wakati askari walikuja kutulinda ili tuendelee na kazi.
Baadaye walikubali tuendelee na uongozi baada ya kupewa onyo kali, na kipindi hicho Marehemu Chachage aliplay major role ya kutupatanisha kambi ya Zitto na yetu.
Kitu ambacho nitamtetea siku zote Zitto ni kuwa sijapata sababu ya wazee wa chama kumtaka asigombee uenyekiti, to me democracy hapa haipo
Waberoya
Sijasema wamwache nilichosema wasikurupuke kumfukuza kama wananifukuza mimi nisiye na mfusi hata mmoja yeye ana jimbo, ila kwa anachofanya sasa si u-gentleman kwa kiongozi yeyote akitaka kuondoka aondoke mwenyewe asipojitoa awepoawepo tu kama waziri asiye na wizara maalumu.
Kuhusu Mbowe, Zitto,Mrema,Kubenea, Mwakyembe kumsifia JK ni kweli ila sijui ni statement gani Mbowe aliyoitoa ila wengine zipo wazi.
Kuhusu DARUSO ndugu yangu kwa macho ya nje utasema kinatetea maslahi ya wanafunzi lakini kimegeuzwa kuwa cha kisiasa zaidi, viongozi wake wako kwenye payroll ya serikali ni kitengo cha kisiasa kama ilivyo REDET sijui kama na wewe ulikuwa kwenye hiyo payroll.
Hilo la kina Zitto kugomea matokeo ya Daruso siwezi kuthibitisha ni yupi alikuwa sahihi inawezekana waliokuwa wanalindwa na polisi ndio walikuwa na makosa sijui. Mfano huu unanipa picha kuwa Zitto yuko serious zaidi wakati hasa wa kuhesabu kura yuko tayari kwa lolote hata kama anavunja katiba mfano uchaguzi Mkuu wa UVCHADEMA mbali ya kura kuzidi wapiga kura still yeye alitaka matokeo yahalalishwe wakati yeye alitakiwa ndiye awe chachu ya kuilinda katiba.
Hivyo alivunja katiba waziwazi bado anataka wamuone kuwa anamsimamo hataki kukiri alivunja katiba aonekane anamsimamo, kweli watani zangu Waha wabishi. Huyu ndiye kiongozi tunayemtetea.
Na mimi pia nitakupeni uzoefu wangu ndani ya Daruso wakati wa kunji kubwa la 1990 hadi chuo kikafungwa mwaka mzima wanafunzi wote ilibidi turudie mwaka ukaitwa mwaka wa Mwinyi eti tumemtukana Rais matusi ya nguoni. Enzi za kumbeba Mtikila Nkhruma kusukuma gari la Mrema baada ya kumwaga sera Nkhruma nk.
Mimi nilishasema huyu tangu aingie ile kamati ya madini alilishwa limbwata!!! ni mnafiki wa kufa, hafai kabisa. Chadema achaneni na huyu fisadi wenu ila mwacheni atoke peke yake. Anatapatapa huyu, anajua umaarufu wake ni kwisha kabisa.
Kama kweli ni jasiri kwa nini aandike barua za kauchana na siasa au chadema na asite kuziwasilisha?? Hajiamini huyu ndiyo maana mguu nje ndani tu. Wewe toka Chadema na Chadema itaendelea kupeta kama kawaida. Wewe siyo Mungu wa Chama.
Hata leo mini au mwingine akiamua kujishughulisha na siasa, si kwamba ni first priority, it is the second or third kabisa. Sasa kwani hilo linahitaji mjadala? Ondoka leo tena naona umechelewa sana.
Hivi unakumbuka na kufikiri maovu yote na siri za chama cha chadema ulizomwaga nje?? Ni nani katika Chadema anakupenda kwa sasa? Labda wale wanaokupenda ni wale wanafiki na wasaliti kama wewe. Wewe mpayukaji, mdomo hauna speed governor. Hata kama vyama vingine watakuchukua, particularly SSM bado watakuona wewe ni loose fulani na huna nidhamu ya mdomo. Ulianza vizuri siasa, usipokuwa makini utamaliza siasa vibaya. Pole young boy/politician.
Kabla ya serikali yetu alikuwepo Rugemarila, he is the one who signed agreed with loan board watu kupewa loan kwa asilimia, serikali zetu na iliyofuata tulipinga na utekelezaji wako umekuja kuanzia 2008! wakati ulitakiwa kutekelezwa 2003!
Umeeleza swala la DARUSO pengine mimi ninamfahamu vizuri Zitto kuliko nyie wote, kwani ndiye aliyetaka kuipindua serikali yangu ya DARUSO(2003-2005)!
Kitu ambacho nitamtetea siku zote Zitto ni kuwa sijapata sababu ya wazee wa chama kumtaka asigombee uenyekiti, to me democracy hapa haipo
Kaka acha upotoshaji wa historia...
Kaka jibu lake ni rahisi tu. Kama Zitto aliamua kukubali ushawishi/maoni/shinikizo ama ushauri wa wazee hawa na akajitoa lakini wenzake wameendela kufanya haya mnayoyaona na msiyoyaona bila ya kujali hatima ya chama chao na matamanio ya watanzania waotao mabadiliko, unadhani angekataa ushauri huo na kuelekea kwenye uchaguzi wangelifanya nini?
Waberoya
ila sijui ni statement gani Mbowe aliyoitoa ila wengine zipo wazi.
.
.
Chadema is dead! from he first day Mtei aliposema na waandishi wa habari kuwa kuna watu wamepewa hela na CCM kuharibu uchaguzi. That statement ilichukuliwa kwa mitazamo tofauti, lakini ndani ya chama ilionekana kama Zito msaliti. walifanya hivyo makusudi kuharibu jina la Zito na influence yake, very same people wakampa unaibu katibu mkuu, mtu ambaye viongozi wamemfanya mpaka mwanachama wa kawaida amwangalie Zito kama msaliti!
Naamin yote hayo ni blessing in disguise kwani yanaendelea kumjenga kama kiongozi na kumpa nafasi ya kufanya self reflection kwake kama kiongozi wa chama kinachopaswa kuwa tofauti na CCM na chenye jukumu la kujenga taifa la kidemokrasia, kitu ambacho amekuwa akikifanya sana.It is hard and believe I can feel the pain that Zito is bearing, kuwa kiongozi ndani ya cham chako at the same time kuwa excommunicated from that very same group is not easy to live with!
Ni wazi mpo wengi sana.....msikate tamaa. Nafasi bado ipo ya kukirudisha kwenye mstari na haswa umuhimu wa kuwa waumini wa kweli wa DEMOKRASIA na MAENDELEO yenye kujali TANZANIA zaidi kuliko personal ambitions na UKADA FEDHULI unaojijengaI have lots of friend who have lost their faith on Chadema, as I speak today, Chadema is not the same, and I will not stand to see the very same Chama I loved most doing things that are exactly the same as CCM.
Kaka jibu lake ni rahisi tu. Kama Zitto aliamua kukubali ushawishi/maoni/shinikizo ama ushauri wa wazee hawa na akajitoa lakini wenzake wameendela kufanya haya mnayoyaona na msiyoyaona bila ya kujali hatima ya chama chao na matamanio ya watanzania waotao mabadiliko, unadhani angekataa ushauri huo na kuelekea kwenye uchaguzi wangelifanya nini?
Chadema is dead! from he first day Mtei aliposema na waandishi wa habari kuwa kuna watu wamepewa hela na CCM kuharibu uchaguzi
I have lots of friend who have lost their faith on Chadema, as I speak today, Chadema is not the same, and I will not stand to see the very same Chama I loved most doing things that are exactly the same as CCM.
Unaweza ukatujuza? Omar tatizo langu mimi na Zitto ni KUROPOKA kwenye vyombo vya habari kwa maamuzi ya vikao halali. Wewe unaona sawa? Mbona Mbowe na Slaa wako kimya? Ingesaidia pia. Nisaidie kuhusu hili, wengi hatujui yanayotokea humo CHADEMA. Zaidi ya Kafulila na Danda kuvuliwa nyadhifa?
Nina maswali
Kabla ya Kafulila kijivua Uanachama wa CHADEMA, je nini ilikuwa mipango ya CHADEMA? kusimamisha mgombea Kigoma Kusini au Kuunga mkono NCCR-Mageuzi?
Swali la msingi kabisa.Nina maswali
Kabla ya Kafulila kijivua Uanachama wa CHADEMA, je nini ilikuwa mipango ya CHADEMA? kusimamisha mgombea Kigoma Kusini au Kuunga mkono NCCR-Mageuzi?
Swali la msingi kabisa.