Zitto aipa Tanzania jina jipya

Zitto aipa Tanzania jina jipya

John W. Mlacha

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2007
Posts
3,504
Reaction score
1,343
"Rushwa inavyotembezwa katika uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki inatia simanzi sana. Haingii akilini kwangu kabisa kwamba Mbunge anahongwa ili kuchagua Mgombea fulani. Nchi hii inanuka uvundo. Uvundo wa Ufisadi. Sasa ni sahihi nchi hii kubatizwa jina jipya FISADISTAN 'The Land of The Corrupt'"- Zitto Kabwe
aiita FISADISTAN The land of the corrupt
 
Kwahio members of Posho's (wabunge) wanaongwa ili kuchangua other members of Posho ?

This can only happen in Fisadistan
 
Siungi mkono ! Yaani watanzania wote ambao wanapigana kuhakikisha wanatokomeza ufisadi nao sasa waitwe wafisadistan. La hasha hawezekani kama yeye anataka kuitwa mfisadistan ajiite hivyo. Mimi ni mwafrika wa Tanzania.

Ukisha aanza kujiaminisha kuwa wewe ni fisadi na mtoto wako ukaanza kumwita fisadi na kumonjesha 'utamu' wa ufisadi nakuhakikishieni katu hamtakaa muung'oe ufisadi katika kizazi chenu.

Hivyo tujenge tabia ya kuuchukia ufisadi tusijipe sifa mbaya machoni pa ulimwengu, tujione kujiita mafisadi ni sawa na kutumia kauli mbiu za "Mh". Lusinde.

Viongozi wa ngazi za juu kichama na kiserikali wanapaswa kupima athari za maneno yao wanayoyatoa mbele ya hadhara.
 
Zitto mwenyewe hatumuamini, anahongeka kirahisi mno

Thibitisha tuhuma hizo kwamba anahongeka kirahisi mno. Kwa muono wangu siyo rahis kwa Zitto kukemea rushwa hadharani au kusema rushwa hadharani kama alishawahi kula mlungula na magamba wakamuacha wasimuuombue.
 
aiita FISADISTAN The land of the corrupt

Point ya msingi Zitto anatuhumu wabunge wa chama gani ambao wanahongwa kwa ajili ya kupigia baadhi ya wajumbe kura? Sidhani kama anaweza akakibomoa chama chake, hao nadhani ni magamba tu kama ilivyokuwa Arumeru wakampitisha mgombea ambaye hakuwa na mvuto kwa nguvu ya pesa
 
Ama kweli! Inatia kichefuchefu. Hivi Mbunge ana shida hadi ahongwe? Halafu wanahongwa nini? hela? ngono? ucameron? sh*t!
 
Si jina zuri kbs itakuwa tunawapa kichwa mafisadi na kuhalalisha,kinachotakiwa ni umoja kutokomeza ufisadi mbona mataifa mengine yameweza sisi tunacheka na magamba kuwafanya km wafalme,tukiendelea hivi kweli tutaitwa fisadistan
 
swala la rushwa hili ni gumu kuisha manake kama mtoto anayezaliwa anapokelewa na mikono ya rushwa na alupokwepo tumboni alikuwa kwenye nyumba ya rushwa unategemea kweli iishe? hii ni laana kwa hili taifa
 
Wadau, mna hakika Zitto alishawahi kuhongwa? Sometimes tunamuonea tu.
 
swala la rushwa hili ni gumu kuisha manake kama mtoto anayezaliwa anapokelewa na mikono ya rushwa na alupokwepo tumboni alikuwa kwenye nyumba ya rushwa unategemea kweli iishe? hii ni laana kwa hili taifa

tuwaue wabunge wote basi
 
Yeye mwenyewe je siyo fisadi na kama siyo mbona yuko kwa magamba saaana wakati chama chake ni chadema M4C
 
hao ndio wawakilishi wetu,
  • wala rushwa
  • watoa rushwa
  • wananunua watu
  • wananunulika kirahisi
na Zitto kasema ukweli kabisa

swali - je, tuna haja ya kuwa na bunge????
 
Back
Top Bottom