Zitto agwaya walioficha mabilioni Uswisi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,842
2,000
Zittopozi(1)(8).jpg

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema)


Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amegwaya baada ya kusema kuwa hatataja orodha ya vigogo walioficha fedha nje ya nchi kwa shinikizo kama ilivyokuwa kwa watuhumiwa 11 wa ufisadi, lengo likiwa ni kuwezesha uchunguzi wa kina kufanyika.

Akizungumza jana katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV, Zitto, alisema badala ya kutaja majina hayo kwa lengo la kupata umaarufu wa siku chache, atalisaidia taifa kufanya uchunguzi utakaosaidia kuondokana na kitendo hicho cha kuhujumu uchumi wa nchi.

“Hili si jambo dogo hata kidogo, nashangaa limepunguzwa uzito kwa watu kutaka nitaje majina ya watu waliohifadhi fedha nje ya nchi, mwaka 2007 tulitaja orodha ya mafisadi 11 ni hatua gani zimechukuliwa?” alihoji Zitto na kuongeza: “Safari hii hatutataja majina ya watu hawa kwa mashinikizo.”

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam mwaka 2007, alitaja majina ya watu 11 ambao chama hicho kilidai kuwa ni mafisadi.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alisema kwa bahati nzuri Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, ameshaunda kikosi kazi cha kuchunguza tuhuma hizo.

Alisema yeye yuko tayari kushirikiana na kikosi kazi hicho katika kubaini ukweli wa tuhuma hilo.

Aliwataka Watanzania kusubiri taarifa ya uchunguzi huo ambayo serikali iliahidi kwamba itaiwasilisha bungeni katika Mkutano wa 11 utakaofanyika Aprili mwakani.

Zitto alisema kuwa anamshangaa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, kusema kuwa Uswisi ambayo ni miongoni mwa nchi ambazo benki zake zinadaiwa kuhifadhi fedha hizo, imetoa masharti mazito ikiwamo ya kupelekwa kwa majina ya watu wanaodaiwa kuhifadhi fedha hizo.

“Mimi namheshimu sana Mkuchika, najua kuwa ni komredi na ni mjamaa anayefahamu jinsi baadhi ya mabepari wanavyoziibia serikali za Afrika,” alisema.

Alisema maneno hayo yaliyotolewa na serikali ya Uswisi ni ya kawaida na yamekuwa yakitolewa kila mahali na kutolea mfano kwa aliyekuwa Rais wa iliyokuwa Zaire (sasa DRC), Mobutu Seseseko, ambaye alificha mamilioni ya Dola za Manchini nchini Uswisi.

Zitto alisema kuwa serikali ya Uswisi iliwataka waliokuwa wakimlalamikia Mobutu watoe ushahidi kuhusiana na tuhuma hizo wakati ilikuwa wazi kabisa kwamba kwa mshahara aliokuwa akilipwa na serikali asingeweza kuwa na kiasi hicho cha fedha.

Alipoulizwa kuwa haogopi watu hao wenye fedha ambao wanajua wazi kuwa anawafahamu, Zitto alisema kuwa haogopi kwa kuwa wajibu wa mbunge ni kulisaidia taifa.

Alisema yeye amekuwa na rekodi ya kusimamia rasilimali za nchi na wakati mwingine kupiga kelele na kukumbusha jinsi alivyosimamishwa ubunge baada ya kuwasilisha hoja ya mkataba uliosainiwa na serikali kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Naziri Karamagi kuhusu mgodi wa Buzwagi.

Alisema ingawa alisimamishwa ubunge, lakini leo hii Watanzania wameweza kunufaika kwa kutengenezwa sheria mpya ya madini ya mwaka 2010.

“Sioni hapa kama ni suala la umaarufu wa kisiasa, bali hapa ninaliona ni suala la kiutendaji, mimi nazungumza kitu ambacho ninakiamini,” alisema.

Kuhusu gharama za uchunguzi wa sakata la ufichaji wa fedha hizo nje, Zitto alisema kuwa hakutumia fedha katika uchunguzi huo uliosababisha kuwakilisha hoja binafsi bungeni.

Alisema katika uchunguzi huo alisaidiwa na chama chake, wabunge wenzake na waandishi wa habari za uchunguzi ambao walikuwa na mawasiliano na baadhi ya watu katika nchi za Uingereza, Afrika Kusini na Uswisi

Aidha, alisema atakwenda nchini Ujerumani na kwamba pamoja na shughuli nyingine, atawasiliana na watu waliomsaidia katika uchunguzi huo ili kuwaomba kukisaidia kikosi kazi kilichoundwa kuchunguza sakata hilo.

Katika hoja yake binafsi aliyoiwasilisha katika mkutano wa Bunge uliopita, Zitto alilitaka Bunge liazimie serikali kupeleka bungeni muswada wa kupiga marufuku kiongozi yeyote wa umma au familia yake kuwa na akaunti nje ya nchi.

Alitaka muswada huo uwasilishwe katika mkutano wa 11 wa Bunge, utakaofanyika Aprili mwakani.

Aidha, alitaka Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje ya nchi waeleze wamezipataje na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (Takukuru) ichukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali.

Hoja hiyo kwa mara ya kwanza iliibuliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), katika Bunge la Bajeti la mwaka wa fedha 2012/ 2013 ambapo alikabidhi tafiti za utoroshaji wa fedha nje ya nchi.

Hata hivyo, Bunge liliazimia serikali ifanye uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo na kuwasilisha ripoti yake katika mkutano wa Bunge wa Aprili mwakani.

Zitto anadai kuwa jumla ya fedha zilizototoshwa nchini na kufichwa nje ya nchi ni zaidi ya Sh. bilioni 300.
CHANZO: NIPASHE

 

Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
559
0
Hakuna haja ya kuwataja majina kwa sababu kwa nature ya serikali yetu ilivyo hata majina yangetajwa bado wasingechukua hatua zozote zile na mfano mzuri ni pale yalipotajwa majina ya mafisadi 11 ktk viwanja vya Mwembeyanga mwaka 2007 na hakuna lolote lililofanyika,serikali ina vyombo vingi tu vya uchunguzi kuanzia TAKUKURU,POLISI,JESHI,USALAMA WA TAIFA etc kwa nini wasitumie vyombo hivyo kudadisi na kujua hasa hao vigogo walioficha hizo fedha huko Uswis badala ya kumkomalia Zitto Kabwe tu kuwa ataje majina? Je ni kweli kuwa serikali imeshindwa kujua hawa watu au inataka kutufanyia usanii mtupu?????
 

Mwali

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
7,018
0
Bora asiwataje kwanza ili serikali ilazimike kujenga capacity ya kutatua matatizo kama haya.
Ikiwa wabunge ndio wanalazimika kutoa pesa zao binafsi for private investigation,
Serikali itakua slow ku-react, na inaweza hata kukatwaa ushahidi kua uko biased.
Ila wakiwezesha tume lao au institution yoyote dealing with this, itakua bora
maana hata future cases (coz there will be future cases) will be dealt with promptly
However, serikali ikiendelea na hii lack of political will, basi alazimishe tume la bunge kuundwa
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,106
2,000
mi naona ayataje tu hata wasipochukuliwa hatua hali ya hewa ndani ya ccm itaendelea kuchafuka...can't y'all see this?
 

+255

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
1,940
1,500
Kama ana orodha ya wenye fedha huko Uswisi, sasa safari yake ya kwenda huko ni ya kutafuta nini? au ndo anaenda kufanya mipango zirudishwe?
 

Mbayyo

Member
Dec 2, 2012
22
20
Haya mambo ya rushwa ni Magumu usipokuwa makini unaweza poteza maisha
hivyo zito ana haki ya kuwa makini asikurupuke na kuanza kutaja majina anatakiwa awasilishe kwenye Vyombo
vya Dola ndio Kazi ya hasa
 

Takalani Sesame

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
588
170
Mheshimiwa Zitto,
Uchunguzi huu utakuwa sio wa kwanza kufanya na Serikali kwa sakata za kifisadi kama hizi. Muhimu ni hatua gani zitakazochukuliwa kama ikibainika ni kweli kuna mabilioni yamefichwa Uswisi. Na kwenye kuchukua hatua, serikali yetu haina la kujivunia. Jiandae kwa sarakasi nyingine kama ya EPA, Richmond, Dowans, Jairo n.k. n.k. n.k.
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,490
2,000
Jembe letu tunaliaminia, mi namshauri awe makini make yale yaliyo wapata mwakyembe na professor Mwandosi yasimkumbe.
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,170
2,000
Hakuna haja ya kuwataja majina kwa sababu kwa nature ya serikali yetu ilivyo hata majina yangetajwa bado wasingechukua hatua zozote zile na mfano mzuri ni pale yalipotajwa majina ya mafisadi 11 ktk viwanja vya Mwembeyanga mwaka 2007 na hakuna lolote lililofanyika,serikali ina vyombo vingi tu vya uchunguzi kuanzia TAKUKURU,POLISI,JESHI,USALAMA WA TAIFA etc kwa nini wasitumie vyombo hivyo kudadisi na kujua hasa hao vigogo walioficha hizo fedha huko Uswis badala ya kumkomalia Zitto Kabwe tu kuwa ataje majina? Je ni kweli kuwa serikali imeshindwa kujua hawa watu au inataka kutufanyia usanii mtupu?????Eti wasitajwe? Mi naona ni vema tu wakatajwa na tuwajue ni nani na nani wamejilimbikizia mashilingi hapo majuu!

FUATILIA HAPO DOWN! HATUKUBALIANI NAO HATA PUNJE!

MAMBO NI HAPA
 

Njowepo

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
9,619
2,000
Serikali ndo inapaswa wataja waliokwapua ela na kupeleka nje bse inawajua fika
apo zitto mnamuonea tuu
 

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
4,466
2,000
Bw.Zito Kabwe anawapigia muziki na nyie mnacheza, na kila akibadilisha tune na nyie mmo!
Huyu jamaa hayo majina hana, hajawahi kuwa nayo na wala hana jeuri ya kuyapata!

Ndio maana nasema CCM ina uhakika wa kuongoza Tanzania kwa miaka mingine zaidi ya 20, kwa maana Watanzania ni rahisi sana kuwadanganya, sisi ni kama watoto vile, akililia kitu unamdanganyia na pipi ananyamaza na anaanza kukuchekea tena, Bw. Zito Kabwe, CHADEMA na CCM wanalijua hilo na ndicho wanachokifanya!
 

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,170
2,000
Bw.Zito Kabwe anawapigia muziki na nyie mnacheza, na kila akibadilisha tune na nyie mmo!
Huyu jamaa hayo majina hana, hajawahi kuwa nayo na wala hana jeuri ya kuyapata!

Ndio maana nasema CCM ina uhakika wa kuongoza Tanzania kwa miaka mingine zaidi ya 20, kwa maana Watanzania ni rahisi sana kuwadanganya, sisi ni kama watoto vile, akililia kitu unamdanganyia na pipi ananyamaza na anaanza kukuchekea tena Bw. Zito Kabwe, CHADEMA na CCM wanalijua hilo na ndicho wanachokifanya!


Hapo kwenye red Kijakazi nakwambia mwisho umefika!
 
Last edited by a moderator:

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
4,466
2,000
Hapo kwenye red Kijakazi nakwambia mwisho umefika!

Waswahili tunasema usiandikie mate wakati wino upo, hivyo tusuburi, uchaguzi unakuja, tutaona kama wewe uko sahihi au mimi!

Na kama kweli mwisho wa kudanganywa ungekuwa umefika Bw. Zito Kabwe asingewachezea hivi watu, yeye alisema ana majina atayataja na akasema Bungeni kama serikali isipotaja yeye atataja, akapata umaarufu, watu wakasahau matatizo yake na chama chake, wakaanza kushabikia, muda umefika sasa hivi anasema hatawataja kwa maana hakuna maana yoyote, sasa kama alilijua hilo kulikuwa na haja gani ya kuahidi, tena Bungeni kwamba atayataja majina, kama sio kuwaahidi Watz pipi kwa maana walikuwa wanalialia ili wanyamaze, halafu pipi hawapi, anawaambia Dukani wamefunga lakini kesho msijali nitawaletea na biskuti pia, nyamazeni watoto wazuri, na kweli wamenyamaza sasa wanasubiria biskuti!

 

Deo

JF-Expert Member
Nov 10, 2008
1,215
1,250
Eti wasitajwe? Mi naona ni vema tu wakatajwa na tuwajue ni nani na nani wamejilimbikizia mashilingi hapo majuu!

FUATILIA HAPO DOWN! HATUKUBALIANI NAO HATA PUNJE!

MAMBO NI HAPA

MAMBO NI HAPA jamani nimeinakili kama tulivyoagizwa

Orodha kamili ni:
Jakaya M. Kikwete, January Makamba, Abdalla Kighoda, Nimrod Mkono, Nazir Karamagi, Andrew Chenge, Yusuf Makamba, Edward Lowassa, Rostam Aziz, Yusuf Manji, Ridhiwani Kikwete, Mohamed Dewji, Bernard Membe, Paul Chagonja , Zitto Kabwe, William B. Mkapa, Said Mwema, Abdulrahman Shimbo, Edward Hosea, Daudi T.S Balali, Basil Mramba,Mustapha Mkullo, Grey Mgonja, Patrick Rutabanzibwa,Tanil Somaiya, Jeetu Patel, Onoko Okesukwu mwenye asili ya Kinigeria, Awadh Mohamed (mwenye uraia wa msomalia) na Subhash Patel
Orodha ya wanaoingiza pesa chafu/haramu na kuzitakatisha ni ndefu nitawawataja kadiri muda utakavyo niruhusu.

Kufuatana Jason Bourne hayo ndiyo majina.

Zito yumo. Je lengo la Zito ni nini? Je kunakupona? Tutafika? Mjadala mwema
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom